Kesi ya Uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. @TunduALissu imepangwa kuendelea katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam tarehe 09 Februari 2026.
Zimebaki siku sita tu — tujitokeze kwa wingi kupata darasa la sheria kutoka kwa Mhe. Lissu.
#FreeLissu
Nabii wa chadema @godbless_lema akiwa bungeni alitabiri kifo cha Jenista Mhagama kwakusema kuwa "siku ukikosa uwaziri, utakufa" sina hakika sana na quotation yangu ila maana ilikuwa ni hiyo. Leo hii maneno ya Lema yametimia.
Nachoka mimi🙈
#tutaelewana tu
#free TAL
Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Geita vijini #MbeshiPaulo Ametekwa, Jana ilikuja Gari ikambeba na kujatambulisha kuwa ni Askari Polisi, mpaka leo familia haijui alipo Ikumbukwe Bw. Mbeshi amekuwa mkosoaji mkubwa Wa serikali hii.Hii hali haivumiliki haivumiliki haivumiliki.
"Mhe. umeambiwa kwamba naomba huruma ya Mahakama. Mimi siombi huruma ya Mahakama. Siombi, sijaomba na sitaomba.Ninachotaka, utaratibu wa Mahakama usichezewe. Mawakili wa Serikali na DPP wanachezea utaratibu wa Mahakama. Mimi siyo aina ya watu ambao wataomba huruma ya Mahakama."
#updates
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi Bi. Brenda Rupia, jioni ya leo Jumapili, Julai 13, 2025 amehojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuhusiana na taarifa kwa umma aliyoitoa Julai 2, 2025, iliyoeleza kuwa kuna mipango ya kumuwekea sumu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Tundu Lissu akiwa gerezani.
Nikiwa mkubwa nataka kuwa kama wewe, kiongozi thabiti na mwenye msimamo. Kuna kiongozi angekuwa wewe angebaki kwaajili ya maslahi yake binafsi. Hakika unevipiga vita vilivyovizuri na mwendo umeumaliza @balozipolepole
📍VIDEO:
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana @bavicha_taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTz, Deogratius Mahinyila @AdvMahinyila, amemuomba Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho John Heche, kutowajibu waliokuwa wanachama wa CHADEMA ambao hivi karibuni walianzisha kundi lao linalojiita G-55 kwakuwa kuna kiongozi yupo ndani ya chama ndiye anawatuma hivyo asubiri siku akijitokeza huyo ndio anapaswa kumjibu.
Mahinyila ameysema hayo leo Mei 8, 2025 wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera kwenye mkutano wa hadhara ambapo Makamu Mwenyekiti Heche anaendelea na kampeni yao ya 'No Reforms No Election'