@iammartial97@hamis_abas Sio Dodoma tu mkuu, I had been in different places where Catholics wamenunua ARDHI legally na Tena sio mjini ni porini, Lindi Iringa etc ni baadhi ya sehemu ambazo nimeshuhudia ikinunua legally na kupewa official documents.
@iammartial97@hamis_abas Kama shida ni hii njoo sasa Dodoma, nikuoneshe na legal documents na watu waliohamishwa na kupewa stahiki zao.
Hakuna Cha bure ndani ya Catholics. Kama hujui kitu ni heri unyamaze.
MFUMO WA ALAMA ZA KIKRISTO: TUNAZIELEWA KWELI?
Umewahi kujiuliza maana ya alama kama ☧, IHS, ΑΩ au INRI unazoziona kwenye mavazi ya mapadre, Altare, Misalaba na Makanisa ya Katoliki?
Tutaanza mfululizo wa kujifunza alama moja baada ya nyingine: asili yake, historia, maana yake ya kibiblia na umuhimu wake katika imani na liturujia ya Kanisa.
Lengo si kuzitambua tu, bali kuelewa ujumbe wa Kristo unaowasilishwa kupitia alama hizo.
Tumsifu Yesu Kristo.
My Mom and Dad in heaven will be proud.
This is a dream come true, nakumbuka nikiwa shule nilikuwa nasikiliza Sports Xtra but leo nasikika Sports Xtra❤️🙏🏽.
God exists 🙏🏽
Nikiambiwa niwashauri vijana huwa nawaambia: Waamini katika kile wanachofanya. Matokeo huwa ni process huwezi kuyapata kwa haraka. Usitamani mafanikio ya mwingine bila kujua njia alizopita. Weka JUHUDI kwa kile unachofanya na utaona faida yake. Mwisho achana na WANAWAKE.
Kabla haujaoa make sure unastructure vizuri mali na utajiri wako
Weka rekodi ya kila transaction unayofanya
Ukishaoa do the same
Akitaka talaka just mwambie go ahead
Kama hajachangia chochote au house wife hawez pata zaidi ya 20% ya Properties
Wanaume tujifunze kwa Case ya Mosha
MATENDO YA UCHUNGU (Ijumaa)
1. Yesu anatokwa jasho la damu kwa ajili yetu
2. Yesu anapigwa mijeledi kwa ajili yetu
3. Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu
4. Yesu anachukua msalaba kwa ajili yetu
5. Yesu anakufa msalabani Kwa ajili yetu
Moyo Mtakatifu wa Yesu, utuhurumie🙏
Salamu Maria,
Umejaa Neema, Bwana Yu Nawe,
Umebarikiwa Kuliko Wanawake Wote,
Na Yesu Mzawa Wa Tumbo Lako Amebarikiwa,
Maria Mtakatifu, Mama Wa Mungu,
Utuombee Sisi Wakosefu,
Sasa Na Saa Ya Kufa Kwetu,
Amina 🙏🏿🤲🏿.
Maria Mtakatifu, Mama Wa Mungu... Utuombee 🙏🏿🤲🏿.
Yesu mwenyewe anatuthibitishia uhalali wa kitabu cha Mwanzo
MFANO:
alipoulizwa juu ya suala la Taraka,
jibu lake, alirejelea kwenye kitabu cha Mwanzo akaonyesha kusudi la Mungu la ndoa tangu Mwanzo.
Kitabu cha Mwanzo ni very Powerful, kutokukisoma ni sawa na kusafiri bila kujua ramani ya unakotoka na unakokwenda.
Acha mwezi huu wa Rozari ukuwezeshe kurudi kwa unyenyekevu kwenye sala. Mtazamo wa utulivu kuelekea Mbinguni na Mama anayesubiri kusikiliza. Ukabidhi moyo wako kwa Maria na umruhusu akuongoze moja kwa moja kwa Yesu. Fanya hivyo hatua kwa hatua na kwa kila fungu la sala.
Mwezi Oktoba ni mwezi wa Rozari Takatifu.🌹🙏
Tusiuache mwezi huu upite bila kujenga upya au kuimarisha utamaduni wa kusali Rozari. Katika kila fumbo, tunatafakari maisha ya Kristo kwa macho ya Bikira Maria, tunaimarisha imani yetu na kujifunza kuyakabidhi maisha yetu kwa Mungu.
Kusali Rozari ni sala ya kumtukuza Mungu na kumtafakari Yesu Kristo kwa kuzingatia matukio muhimu ya maisha yake pamoja na kumuomba Bikira Maria atuombee
Rozari inahusisha:
>Kumweka Mungu katikati — Rozari sio kumuabudu Maria; ibada ni kwa Mungu pekee
>Kutafakari maisha ya Yesu kupitia mafumbo ya Rozari: Furaha, Mwanga, Uchungu na Utukufu
>Kumuomba Mama Maria atuombee kwa sababu yeye ni Mama wa Yesu na Mama wa waamini katika mapokeo ya Kanisa
>Kutafakari Injili — kila fumbo linatukumbusha tukio fulani katika maisha ya Kristo
>Kuomba neema, ulinzi, msamaha na msaada wa Mungu katika maisha yetu
>Kukuza imani na ukaribu na Mungu kwa kurudia sala kwa utulivu na tafakari
Leo Shirika la Mitume wa Yesu (Apostles of Jesus Missionaries - AJ) wanasherehekea miaka 25 ya Upadre (Silver Jubilee) ya Padre Henry Rimisho, AJ wa shirika hilo.
Padre Rimisho alizaliwa January 26, 1969 huko Jimbo Katoliki Moshi. Baada ya kuhitimu kidato cha sita alipata wito wa Upadre na kujiunga na Shirika la Mitume wa Yesu (Apostles of Jesus Missionaries - AJ).
Baada ya malezi alitumwa Chuo Kikuu Urbaniana, Italy kwa Shahada ya Kwanza ya Falsafa (Bachelor Degree in Philosophy) na kuhitimu 1996. Aliendelea na masomo chuoni hapo na kuhitimu Shahada ya Theolojia (Bachelor Degree in Theology) mwaka 2000.
Mwaka 2001 alipata daraja takatifu la Upadre na akahudumu katika Jimbo Katoliki Moshi na Jimbo Kuu DSM kabla ya kutumwa Darfur, Sudan kutoa huduma za kiroho katikati ya vita. Kutokana na unyeti wa huduma hiyo alilazimika kupata mafunzo ya kijeshi ili kujilinda akiwa vitani.
Katika mahojiano na gazeti la Mwananchi la Desemba 07, 2021 alisema alipata mafunzo kupitia Jeshi la Sudan. Baadaye aliendelea na mafunzo zaidi ya kijeshi nchini Kenya na Cuba hadi kufikia cheo cha Kapteni.
Baada ya miaka mingi nchini Sudan, hatimaye mwaka 2007 alitumwa Chuo Kikuu Ardhi kwa Shahada ya kwanza ya Usanifu Majengo (Bachelor Degree in Architecture) na kuhitimu 2011. Kutokana na ufaulu mzuri alibakizwa chuoni hapo kama Msaidizi wa Mihadhara (Tutorial Assistant).
Mwaka 2012 alitumwa tena kwa Shahada ya Umahiri ya Usanifu Majengo (Master’s Degree in Architecture) na kuhitimu mwaka 2014. Aliajiriwa chuoni hapo kama Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer) katika Idara ya Usanifu Majengo, Uchumi na Ujenzi.
Mwaka 2016 alitumwa tena masomoni kwa Shahada ya Uzamivu ya Usanifu Majengo (PhD in Architecture) na kuhitimu mwaka 2021. Kwa sasa ni Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) wa Chuo Kikuu Ardhi. Amesajiliwa na Bodi ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) na amesanifu majengo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo majengo ya Kanisa.
Pia ni mchezaji mashuhuri wa Karate na Judo anayeshikilia mkanda mweusi (Black Belt) katika mchezo huo. Tumtakie heri ya miaka 25 ya Upadre, Rev. Fr. Dr. Captain Henry Rimisho, AJ. Roma locuta, causa finita est 🙏🏽
Cc @MalisaGJ_
Kuna jambo moja muhimu sana hapa, kwa mtazamo wangu kilichotokea leo kina implication kubwa sana kisheria.
Lissu amefika Mahakamani akiwa tayari kuendelea na ushahidi wake. Tatizo likawa kwenye wale mashahidi watatu ambao Mahakama ilikuwa imekubali waitwe Kingai, IGP Wambura na CDF Mkunda.
Lissu amesema amekutana na Kingai mwenyewe hapa hapa Mahakamani, wamezungumza, akamweleza maeneo ambayo alitaka Kingai ayatolee ushahidi.
Lakini Kingai, kwa maelezo ya Lissu, amemwambia wazi kwamba hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi kwa sababu yuko upande wa wale wanaotaka Lissu apatikane na hatia.
Na Kingai akaeleza kwamba Wambura na Mkunda nao watakuwa na msimamo huo huo.
Hapo ndipo issue ya kisheria inakuwa interesting sanaaa
Kwa sababu, mtu akiwa shahidi wa Mahakama, sio lazima awe defence witness kwa maana kwamba anatakiwa kuja kuunga mkono Lissu.
Yaani shahidi anatakiwa kutoa ukweli alionao, na qnaweza kutoa ushahidi unaomsaidia Lissu, usiomsaidia, au hata unaoweza kuathiri defence.
Lakini kama kweli shahidi aliyekuwa ameitwa na Mahakama anakataa kutoa ushahidi kwa sababu ya msimamo wake binafsi, hilo ni jambo tofauti kabisa na kusema hana ushahidi wa relevant.
Lakini pia tusikimbilie kusema Kingai amekiuka sheria. Hatujui bado msingi wa kisheria alioutoa wa kutokutoa ushahidi, kama kweli alikataa kwa maana hiyo, au kama kulikuwa na limitation nyingine.
Hayo ni mambo ambayo lazima yaonekane kwenye record kabla hatujatoa conclusion ya mwisho.
Sasa kwa Lissu, practical position imekuwa imekuwa ngumu kwa maana Mashahidi wake waliobaki hawapo nchini, mmoja ambaye amefika anasema hayuko tayari kutoa ushahidi kwa defence,
Na hivyo Lissu anaona hana tena witness wa kuendelea naye, ndio maana akaomba kufunga defence case.
Na hapa kuna jambo ambalo watu wengi wanaweza kulikosa na kutoelewa kwamba, kufungwa kwa defence case hakumaanishi burden of proof imehamia kwa Lissu.
Nawakumbusha pia jamhuri bado ndio yenye burden ya kuthibitisha kila ingredient ya offence beyond reasonable doubt.
Kwamba defence ikiwa haina shahidi mwingine, hilo haliruhusu Mahakama kujaza gaps zilizopo kwenye prosecution evidence kwa kusema, kwa kuwa defence haikuita mashahidi, basi allegation ya Jamhuri imethibitika.
Na hapa ndipo masuala kama mens rea, attribution, causal nexus, credibility, corroboration na probative value yanabaki kuwa muhimu sana.
Kwa hiyo, mimi nikiangalia sioni kama Lissu amekosa mashahidi, lakini naona defence imefika mwisho wa uwezo wake wa kupresent evidence..
Baada ya kukutana na tatizo la availability na willingness ya baadhi ya witnesses waliokuwa wamekusudiwa kuitwa.
Tukumbuke mwisho wa kesi ya jinai hauamuliwi na nani alikuwa na mashahidi wengi.
Ila unaamuliwa kama prosecution imefunga evidentiary chain yake bila kuacha reasonable doubt kwenye ingredients muhimu za kosa.
Naweza sema TAL ameshinda kwenye hili