Zanzibar Press Club (ZPC) is a Non Government Organization which involve all members of journalism established under Zanzibar Civil Society act no. 5/1995.
A historic moment has made as four lead applicant organizations THRDC, Wajibu, Haki Elimu and IMS, officially signed grant contracts under the European Union’s Strengthening CSOs as Independent Actors of Good Governance and Development in Tanzania.
#PressFreedom@UTPCtz
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewahimiza wazee kuzidisha umakini wanapotumia mitandao ili kuepuka utapeli wa mitandaoni. Afisa Masoko TCRA, Sophia Mabada, alitoa rai hiyo wakati wa kampeni ya 'Ni Rahisi sana' kwa wazee wa mkoa wa Kusini Unguja yalofanyika Kitogani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk. Pindi Chana Oktoba 2, 2024 ametembelea shamba la Miti Mbizi, lilioko chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wilaya ya Sumbawanga, Rukwa kukagua uendelevu wa chanzo cha maji na kuona mchango wa shamba hilo kwa jamii.
MSHINDI wa jumla wa tunzo za umahiri wa uandishi wa habari (EJAT) 2023 zinazoandaliwa na @mediacounciltanzania, Mukrim MOhammed Khamis, Oktoba 1, 2024 alifika Baraza la Wawakilishi na kutambulishwa kufuatia ushindi alioupata Septemba 28, 2024 jijini Dar Es Salaam
Taasisi za Habari Zanzibar Zimeishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukamilisha mchakato wa sheria ya habari ili kuimarisha mazingira ya upatikanaji wa habari na uhuru wa kujieleza.
WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale, Mudrik Ramadhan Soraga, amewaongoza wadau wa historia na utalii zanzibar katika maadhimisho ya kwanza kitaifa ya kumbukumbu ya siku ya kukomesha biashara ya utumwa iliyofanyika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil mjini Unguja.
@ikuluzanzibar
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Allience for Democract change ( ADC ) Taifa, Hassan Doyo (pichani), ametangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti Taifa wa chama hicho kumrithi Mwenyekiti wa sasa, Hamad Rashid Mohamed katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.
"Ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari ni jambo ambalo lilikuwa halisemwi sana, UTPC tumefanikiwa kuandaa mazingira na kutoa kipaumbele katika masuala ya ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari pia tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan @SuluhuSamia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira wezeshi kwa mwandishi wa habari kufanya kazi" Deogratius Nsokolo Rais wa UTPC. @UTPCtz@ImsTanzania@PolisiTanzania@tanpol@TAMWA_@jowuta@MISATANZANIA@OJADACT2@deo_nsokolo@KSimbaya
MSANII Nasib Abdul ‘Diamond Platinum’, Balozi wa Airtel Tanzania akipongezana na Mkurugenzi Masoko wa Airtel Tanzania, Timea Chogo, baada ya kuzindua Airtel 5G Smart Box kurahisisha upatikanaji wa huduma za intaneti. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Rais Samia Suluhu Hassan (Kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland KC, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa nchi Wanachama wa jumuiya hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Zanzibar.
Pumzika kwa amani 'Mzee Rukhsa'. Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mzee Ali Hassan Mwinyi. Hakika ulikuwa hazina na kisima cha maarifa na hadithi ya kuvutia yenye mafunzo mengi kwa kila rika.
KAMPUNI ya Oryx imekabidhi mitungi ya gesi ya kupikia kwa makundi ya wananchi wa Zanzibar kutekeleza ombi la Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi kupunguza athari za kiafya na mazingira. Mitungi 2,000 ilikabidhiwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mudrik Soraga.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Namibia Hayati Dk. Hage G. Geingob, katika Ofisi za Ubalozi huo Masaki jijini Dar es salaam Februari 7, 2024.
MBUNGE wa jimbo la Morogoro Mjini, Abdullaziz Abood, akiwasikiliza baadhi ya wananchi wa kata za Lukobe na Kihonda ambao wiki mbili zilizopita walipatwa na mafuriko yaliyoharibu makaazi yao, miundombinu na kusababisha vifo.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum, amesema uamuzi wa kampuni ya Air Pay kuanzisha kituo cha teknolojia unakwenda sambamba na mkakati wa Serikali kukuza uchumi wa kidigitali na kudhibiti uvujaji wa mapato ya serikali.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ametangaza kuwa maonesho ya nane ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2024 yatafanyika Oktoba 11 - 13 na kuwataka waandaaji kujiandaa mapema na kuyaimarisha ili kupata washiriki wengi kutoka sehemu mbali mbali duniani.