Kwenye hii kesi ya Tundu Lissu ndo nimejua kwamba mara kadhaa wamempeleka mjini kumkutanisha na watu wao kufanya nao deal wakimdanganya kwamba una ujumbe wako kutoka Common Wealth, mara kuna maelekezo kutoka juu! KAKATAA na WAMESHINDWA. Haongeki. Siyo Dalali
MUNGU NI MWEMA, MAHAKA KUU IMEKUBALI PINGAMIZI LA MAWAKILI WA CHADEMA- KESI YA MGAWSNYO WA MALINZA CHAMA IMEFUTWA RASMI LEO
Mahakama kuu ya Tanzania, Masijala ya Dar es salaam leo imetoa uamuzi kufuatia pingamizi la mawakili wa Chama waliloweka wakidai hati ya madai haikuonrsha lini mgogoro ulianza jambo ambo ni kinyume cha Sheria.
Awali pingamizi hili lilipowekwa Jaji Mwanga aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo alidai kwamba, wakati kesi ikiendelea itajulikana mbele ya safari ni lini hasa madai yalianza.
Ikumbukwe kwamba, Mahakama ya Rufaa baada ya kusikiliza hoja za majereo ilielekeza mahakama kuu ikaamue hoja hiyo mbele ya jaji mwingine ambapo kesi hiyo ilipangwa mbele ya Mhe Jaji D. Ngunyale.
Leo, Mahakama imetoa uamuzi na kukubaliana na hoja zetu kwamba kitendo cha waleta madai kushindwa kuonesha lini hasa madai yao yalianza kinainyima mahakama nafasi ya kujiridhisha kama kweli inayo mamlaka ya kusikiliza madai husika.
Kufuatia hali hiyo, kesi hiyo namba 8323/2025 imefutwa rasmi leo.
Nawashukuru marafiki wote ambao mumelia nasi kama chama kwa namna moja ama nyingine, hakika leo tumshukuru Mungu kwa pamoja.