HAKIKA RC MTAKA UAMINIFU umetupiga chenga. TUTATESEKA sana . Tunaambizana uongo hata kwa yale yaliyo wazi kwa wengi kwamba yalitokea. Hivyo hasira zinapanda, vidonda vinatoneshwa upya badala ya kupona. Halafu tunadanganyana tutaliponya taifa?. HOW?? Kwa kutafuta kafara badala ya KUTUBU NA KUJIREKEBISHA?
Taifa ambalo redioni asubuhi hadi mchana wanajadili michezo. Mchana hadi jua linapozama wanajadili umbea. Jua likizama wanarudi kwenye michezo. Usiku wanajadili ngono hadi pakuche. Hakuna vipindi vya taaluma, ujasiriamali, kilimo, midahalo. Hilo ni TAIFA lipo kaburini kitambo.