โ๐ปUS and Israeli forces have struck Iranian energy infrastructure, targeting a gas pipeline linked to a power plant in Khorramshahr and facilities in Isfahan. The attacks reportedly hit a natural gas administration building and a gas pressure reduction station in Isfahan, causing damage to parts of the facilities and nearby homes. In Khorramshahr, a natural gas pipeline belonging to a power plant was targeted, with no casualties reported .
โ๐ปThis comes after US President Donald Trump warned Iran to fully open the Strait of Hormuz to commercial shipping within 48 hours or face destruction of its power plants. Iran has retaliated with threats to attack US and Israeli energy and infrastructure assets in the region .
๐Ofisi za Nguchiro makao Makuu tabora imeionya ubalozi wa Nguchiro nchini Iran kwakuchelesha kipigo Kwa wazayuni na Marekani
๐ Ubalozi ya Nguchiro nchini Iran msitake ofisi za Nguchiro makao Makuu tabora zifanye maamuzi magumu ya kulipua balozi Hiyo, wazayuni na Marekani hawatakiwi kupumua.
๐ Ubalozi wa Nguchiro nchini Iran ni lazima irushe makombora ya hypersonic kwa wakati dhidi ya maadui zetu Wazayuni na Marekani. Hatutaruhusu ucheleweshaji wala kutochukua hatua kali.
๐ Hali ya mvutano Mashariki ya Kati ni hatari na inahitaji hatua za haraka. Makombora ya hypersonic ni silaha za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kuvunja mifumo ya ulinzi wa anga na kushambulia malengo muhimu ya wazayuni na Marekani
๐ Kutumia makombora ya hypersonic ni kulinda heshima, usalama na masilahi ya united state of Nguchiro, Hatua yoyote ya kuchelewesha itachukuliwa kama ukiukaji wa moja kwa moja wa maagizo ya united state of Nguchiro
๐ Ofisi za Nguchiro Makao Makuu Tabora zinataka kuona utekelezaji wa maagizo haya haraka, bila masharti yoyote na bila kuchelewesha. ni wajibu wa ubalozi wa Nguchiro kuhakikisha ushirikiano kamili na kutekeleza agizo hili.
๐ Ubalozi wa Nguchiro nchini Iran inatakiwa irushe makombora ya hypersonic Ili wazayuni na Marekani wajue Kuwa ubalozi wa Nguchiro nchini Iran ni hatari mno kuliko walivyokuwa wakifikiria.
๐ Ubalozi wa Nguchiro nchini Iran ni tishio kubwa mno Kwa wazayuni na Marekani โ๏ธ๐ฎ๐ท๐บ๐ธ๐ฎ๐ฑ
In the last 24 hours
Important: Iran sent a message to the US that they are ready for talks.
The leader appointed to succeed Khamenei says he didn't want the positionโhe prefers science and religion over politicsโbut they forced him.
Azerbaijan: Azerbaijan's airport was attacked by Iranian missiles.
France: France allowed the US to use its areas to attack Iran.
Spain: After being threatened by the US President, Spanish leaders agreed to let their airspace be used to attack Iran.
Iran: The Iranian Army spokesman differs from the supreme leader, saying they will fight to the final stage.
Tanzania: The JWTZ army spokesman (those threatened by mafwele on 29/10/2025) said it's the world's 6th best army. Mkunda added: don't think we just search for uniforms in streets and our power ends thereโno, we have the same weapons as the US and Iran but don't like showing off.
Hii page inapoteza mvuto haina weledi tena kama zamani soon nitaihama mtu kapigwa sema kapigwa Wote tunajua Iran anashambuliwa sana lakin pia tunajua israel anateseka sana
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 201
Anasimama Wakili wa Serikali Mkude anasema tunashahidi mwingie wa kulindwa ni P3,
Mpaka sasa huyu ni shahidi wa 13.
Shahidi ameingia kwenye kijumba cha mbao tayari.
Sasa anajitambulisha.
Shahidi wa kificho P3 : Nina miaka 35
Shahidi wa kificho P3: dini yangu muislamu
Shahidi wa kificho P3: naishi halmashauri ya Mbeya mjini, mtaa wa Mwamtengule kata ya Syesye
Shahidi wa kificho P3: najishughulisha na kazi ya dereva boda boda
Shahidi wa kificho P3: shughuli zangu nafanyia katika halmashauri ya jiji la Mbeya.
Shahidi wa kificho P3: nina miaka nane tangu naendesha boda boda
Shahidi wa kificho P3: mimi ni mfuasi wa CHADEMA
Shahidi wa kificho P3: nimekua mfuasi tangu 2021 mpaka sasa bado ni mfuasi
Shahidi wa kificho P3: nimewahi kushiriki matukio baadhi kama kongamano la kutoka Mbalizi mpaka Kabwe tulipoenda kumpokea Mhe. Mbowe mwaka 2024.
Tukio lingine ni kongamano la vijana lakin bahati mbaya au nzuri hatukufanikiwa kwasababu serikali ilizuia.
Shahidi wa kificho P5: tarehe 4 april 2025 nakumbuka kijiweni kwangu kwenye boda boda nilikua nachezea simu yangu nikapata kuona hotuba fupi ambayo Mhe. Tundu Lissu akizungumzia uchaguzi uliopangwa kufanyika 2025.
Shahidi wa kificho P3 : hotuba niliiona youtube.
Shahidi wa kificho P3 : namfahamu Tundu Lissu kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuwa nafatilia sana chama cha CHADEMA tangu mwaka 2021.
Katika chama Tundu Lissu ni mwenyekiti wa CHADEMA, baada ya kusikiliza ile hotuba pale kijiweni nikaanza kuwashirikisha wanachama wenzangu wa boda boda na kuanza kuwashawishi wengine wenye mapenzi na CHADEMA kufanya yale mh. Tundu Lissu ameyasema.
Niliwashawishi tuwe kitu kimoja kupambana kuzuia uchaguzi 2025, tulipanga kuzuia uchaguzi kwa namna ya kwamba watu watakaoenda kupiga kura kuwafanyia fujo ikiwepo kupigwa mawe, ushawishi nilikua naufanyia katika kijiwe changu cha pikipiki, baada ya kushawishi wenzangu kuna baadhi waliliridhika na ushawishi wangu na baadhi hawakuridhika.
Shahidi wa kificho P3 : baada ya hapo alitokea mtu mmoja akanipoint kwenye kijiwe na akaniomba tuongee mara moja, nikaenda kumsikiliza na akajitambulisha kuwa. Yeye ni ofisa wa polisi, akaniambia nahitajika twende kituo cha polisi kwa mahojiano yangu mimi na yeye nilivyofika kituo cha polisi wakaniambia nitoe viatu na mkanda na wakaniweka mahabusu.
Wakili: Shahidi P3 baada ya kukaa mahabusu nini kilifuata
Shahidi wa kificho P3 : baada ya muda mchache nikapelekwa kwenye chumba kingine wakaanza kunihoji kwamba nilikuwa naongea nini pale kijiweni, kwanini nilikuwa nahamasisha kufanya uasi.
Wakili: walikuuliza kwa nini unahamasisha uasi gani kama unakumbuka.
Shahidi wa kificho P3: kwanini nahamasisha uasi wa kuzuia uchaguzi wa 2025.
Wakili: Sasa shahidi baada ya maelezo hayo nini kilifuatia.
Shahidi wa kificho P3: waliniambia nitafute mtu wa kunidhamini ili niweze kuendelea na taratibu nyingine.
Wakili: ikawaje.
Shahidi wa kificho P3: nilimpata ndugu yangu akaja kunidhamini.
Wakili: nini kilifuata
Shahidi wa kificho P3: nilipata ndugu yangu akaja kunidhamini. Nikaambiwa niwe naripoti Kila baada ya siku tatu.
Wakili: ulikuwa unaripoti wapi.
Shahidi wa kificho P: nilienda kuripoti Kituo cha Polisi Ilonga.
Wakili: ulivoenda kuripoti ikawaje.
Shahidi wa kificho P3: nikaingia ndani kituoni na kukutana na huyo askari aliyeniandika maelezo toka mwanzo.
Wakili: huyo Askari aliyekuandika maelezo kutoka Mwanzo anaitwa nani kama unakumbuka.
Shahidi wa kificho P3 : namkumbuka kwa jina moja anaitwa Amani.
Wakili: baada ya kukutana na Amani mlifanya nini.
Shahidi wa kificho P3: aliniandika maelezo tena na kuniambia naendelee na utaratibu wa kuripoti.
Wakili: waheshimiwa Majaji wa Mahakama kuu kwa Shahidi huyu ni hayo tu
Part 202 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 177
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Koplo Michael.
Mhe. Lissu: Kwahiyi P8 alikuwa amefanya kosa?
Koplo Michael: ni kweli alikuwa amefanya makosa
Mhe. Lissu: Kwahiyo maelezo yake hayapo?
Koplo Michael: Sijayaleta
Mhe. Lissu: Je mlifungua kesi?
Koplo Michael: Hatukufungua kesi.
Mhe. Lissu: hadi leo hamjafungua?
Koplo Michael: Sijui kwakweli.
Lissu: RCO ndio alikwambia chukua maelezo ya shahidi kwenye kesi ya Lissu.
Shahidi: Hapana sio hivyo.
Mhe. Lissu: anamsomea alipoandika kuwa shahidi kwenye kesi ya lissu.
Koplo Michael: Ni kweli nilisema kumbe.
Mhe. Lissu: Kwahiyo mlikuwa mnaandaa kesi ya Lissu?
Koplo Michael: Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kwahiyo mlikuwa mnaandaa nini?
Koplo Michael: Ushahidi wa kesi.
Mhe. Lissu: Kesi gani?
Koplo Michael: hii ya kwako.
Mhe. Lissu: Kumbe ni yangu umebana umeachia.
Watu; ๐๐๐๐
Sasa tuendelee na swali lingine.
Mhe. Lissu: Nilitishia Serikali kwasababu nilisema tutazuia Uchaguzi, wambie Majaji ni wapi umesema neno lolote juu ya maneno niliyosema?
Koplo Michael : mimi nilisema aliyoniambia shahidi.
Mhe. Lissu: Umeelewa swali we polisi?
Koplo Michael: Hapana sijasema lolote kuhusu maneno gani ulisema.
Mhe. Lissu: naambiwa nilichapisha maneno mitandaoni sasa sema kama kwenye kielelezo D5 kama ulisema chochote kuhusu maneno yangu niliyochapisha.
Koplo Michael: Hapana sikuandika lolote kwenye hayo.
Mhe. Lissu: Kutaka mabadiliko ya Katiba, Tume Huru ya Uchaguzi ni kosa la jinai?
Koplo Michael: Sio kosa la jinai.
Mhe. Lissu: Kuhamasisha wananchi nchi nzima kupatikana Katiba Mpya na kuzuia uchaguzi ni kosa?
Koplo Michael: ni kosa
Mhe. Lissu: Kosa gani?
Koplo Michael: Mimi sio mtaalamu wa sheria, wanasheria watasema.
Mhe. Lissu: Huna unalojua wewe ni Koplo tu, umetaja Katiba tutajie ibara sasa?
Koplo Michael: Sijui kosa ambalo umeshitakiwa nalo.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru: Re Examination.
Ignas Anasimama anasema nina maswali mawili.
Je uliposema hakuna utofauti ulimaanisha nini?
Koplo Michael: Nilimaanisha hakuna tu tofauti maana ni ile ile.
Wakili wa Serikali: Je ulisema hujui anashitakiwa na kosa gani? Ulimaanisha nini?
Koplo Michael: Najua ni uhaini lakini uhaini ni mpana unajumuisha uchochezi na kuharibu mali.
Wakili wa Serikali ni hayo tu Mheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnasemaje?
Renatus Mkude: Tunaomba tuendelee Jumatatu.
Jaji Ndunguru: Kwanini msiendelee na shahidi mwingine atakapoishia ikifika saa 11 tunaacha.
Mkude: Mh. Jaji naomba tuendelee jumatatu tafadhali muda umeenda.
Jaji: Basi jumatatu saa tatu kamili asubuhi tukutane.
Inapigwaa Courttttttt tunatoka.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 175
Mahakama imerejea.
Anasimama Renatus Mkude na kusema tuko tayari kuendelea na tuko na shahidi wa wazi.
Muda huu tunaendelea na shahidi ambae ni H3923 Detective Coplo Michael, Mimi ni askari Polisi. Mimi ni Mristo.
Huyu Polisi mwingine ni shahidi ambae atakuwa ni PW6 Anaongozwa na Ignas Mwinuka, Wakili wa Serikali.
Shahidi ni mwemba mrefu kidogo, mweusi na amevaa miwani.
D. Koplo Michael anasema anaishi Kiusa Street, Moshi Kilimanjaro.
Ninafanya kazi Askari Polisi, naifanyia kazi yangu ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro, nimekuwa katika ofisi hiyo tangu mwaka 2015.
Nimejiunga Jeshi la Polisi mwaka 2012 na kuhitimu mwaka 2013, nilipata mafunzo ya awali katika shule ya Polisi Tanzania TPS kwa maana ya Shule ya Polisi iliyopo Moshi.
Majukumu yangu ni upelelezi wa makosa ya jinai, ukamataji wa wahalifu, kuzuia uhalifu pamoja na majukumu mengine mbalimbali ya jeshi la Polisi.
Tarehe 08/04/2025 nakumbuka majira ya asubuhi nilikuwa doria na askari wenzangu tulikuwa tunazungukia maeneo mbalimbali ya Moshi mjini.
Anaendelea Detective Koplo Michael anasema lengo ni kufanya doria, kukamata wahalifu na kulinda raia na mali zao.
Tukiwa tumefika maeneo ya Njoro hapo wilayani Moshi, tulipata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna kijana mmoja anahamasisha wenzake kuhusiana na kufanyika na Uchaguzi Mkuu uliokuwa unatarajiwa kufanyika mwaka 2025.
Baada ya kupata hizo taarifa kutoka kwa P8 ambae analindwa na Mahakama, tulimkamata mtuhumiwa na kumpeleka ofisi ya RCO kilimanjaro.
Tukampeleka ACP Abichi alinielekeza nifungue jalada la uchunguzi na nilifungua jalada lenye Kumb. No. KR/CID/PE/18/2025 ambalo ni jalada la Uchunguzi.
Afande alisema kijana huyo apigiwe simu na ahojiwe na D. Koplo Rashid na awekwe mahabusu kwanza na atatoa maelekezo baadae.
Wakili Ignas Mwinuka, anaendelea kumuhoji.
D. Koplo Michael anasema kijana huyo alitolewa kwa masharti awe anaripoti kila jumatatu hapo Polisi.
Ilipofika Tarehe 22/04/2025 Afande RCO aliniambia nimtafute yule kijana anayekuja kuripoti, nimuandike maelezo upya.
Na hayo yalikuwa ni maelezo ya shahidi aeleze ni kitu gani kilichompelekea yeye kuhamasisha wenzake kufanya vurugu katika uchaguzi uliotarajiwa kufanyika.
Nilipofuatilia kumbukumbu nikagundua siku hiyo hiyo ndio alikuwa amepangiwa aje kuripoti, alipofika nilionana nae na nikamuandika maelezo ya shahidi.
Kwenye maelezo yake aliniambia yeye ni MwanaChadema alidai alikuwa Mwanachama toka akiwa anasoma Sekondari.
Alisema yeye ni mkereketwa wa Chadema na alikuwa anaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wake wa Chama Tundu Lissu ndio maana alikuwa anahamasisha fuko na kukinukisha.
Alidhamiria kufanya uasi kwa serikali inayoongozwa na CCM na aliongeza kwa kusema kuwa Mwenyekiti wao alisema hawatakubali uchaguzi kufanyika.
Na wako tayari kukinukisha hadi Serikali watakapofanya marekebisho ya tume huru ya Uchaguzi pamoja na Katiba Mpya.
Baada ya kumuandika maelezo nilimpa ayasaini kila page na akakubali kuwa ni malezo yake.
Waheshimiwa Majaji kwa shahidi huyu ni hayo tu. Amemaliza Ignas Mwinuka.
Part 176 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 174
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji hawako serious hawa kwanza ukisoma D4 kila kitu chake kipo hata jina lake hawajaficha lipo na taarifa zake zote zipo, hawajielewi hawa.
Katuga: Anasimama anasema Mh. Sisi ni maafisa wa mahakama aonywe mshitakiwa kwanini anasema hatuko serious.
Mhe. Lissu: Mh. Jaji ni kweli hayupo serious ila nataka niliondoe neno hilo lakini kama anasema nionywe siko tayari kuonywa naomba nifanye submission ya kuonesha ni kwa namna gani hawako serious?
Jaji Ndunguru: Basi Mshitakiwa tuishie hapo kama umesema umeliondoa.
Watu wanacheka sana. ๐๐๐
Mhe. Lissu: je umesema kokote kuwa uliwahi kutishiwa maisha?
Shahidi wa kificho P6: Sijawahi kutishiwa maisha mimi.
Mhe. Lissu: Kuna mwanachadema au kiongozi amewahi kukutishia kukupiga au kukudhuru kwa wewe kwenda kutoa maelezo haya Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo kabisa.
Mhe. Lissu: Je kuna ndugu yako ametishiwa pia?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo hata mmoja.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Kwa sasa ni saa 7 na dakika 15 mchana, huu ni huwa ni muda wa kwenda Break, ngoja tusubiri Kitakachoendelea muda mfupi ujao.
Jaji: Re Examination Jamhuri?
Wakili Cathbert: Hatuna swali lolote Waheshimiwa Majaji.
Jaji Ndunguru Kiogozi wa Jopo la Majaji watatu anateta tena ma wenzake kabla hajasema nini kiendelee.
Anawasha kipaza sauti.
Shahidi umemaliza sasa unaweza kwenda.
Renatus Mkude tunaomba ahirisho tukawaandae mashahidi, lisaa limoja.
Mhe. Lissu: Sawa sina pingamizi.
Jaji Ndunguru: Basi tukutane baada ya lisaa limoja.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 13, 2026
Jana tuliishia Part 167 so leo tunaendelea na-;
Part 168
Mahakama imeanza muda huu saa tatu na nusu.
Mhe. Lissu anaingia akiwa amevaa kombati nyeusi.
Sauti ya High Courttt inapigwa kila mtu anasimama na kelele za kumsalimia Mwenyekiti zinasimama kidogo.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema yupo na Ajuaye, Katuga, Ignas, Cathbert na Winiwa na wote tunawakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Sisi tuko tayari kuendelea na leo tumekuja na P6 yuko tayari, endapo Mshitakiwa atakuwa tayari.
Mhe. Lissu anaulizwa na yeye anasema yuko tayari.
Jaji Ndunguru: Naomba shahidi aje sasa.
Shahidi analetwa kama Bangi kule mbele kwenye kibox hatumuoni chochote tunaona milango tu inafunguliwa sijui amevalishwa baibui.๐
Mlango wa kizimba umefunguliwa muda huu.
Shahidi anaulizwa umri wake anasema miaka 24 na ni Mkristo so anaapishwa muda huu.
Jaji anauliza nani atamuongoza? Anajibiwa ni Cathbert Mbiringe Wakili wa Serikali ndio atamuongoza.
Anamuuliza unanisikia.
Haya mkazi wa wapi?
Mimi natokea Ruvuma Songea na kazi yangu ni Afisa Usafirishaji Bodaboda, nafanyia huko huko Songea shughuli zangu.
Mwezi October 2024 ni mwaka ambao nilianza kushirikisha siasa za Chama cha Chadema.
Wakili: Ulishiriki kivipi?
Shahidi wa kificho P6: Nilianza kushiriki kwenye mikutano ya hadhara na kuwafuatilia viongozi mbalimbali wa Chadema na nikafanikiwa kuwafahamu Mhe. Lissu na baadhi ya Viongozi waliokuwepo Songea.
Wakili: wakiwepo akina nani?
Shahidi wa kificho P6: nilimfahamu Katibu wa Vijana Songea.
Wakili: Alikuwa anaitwa nani?
Shahidi wa kificho P6: alikuwa anaitwa Chiza au Mwamba wa Kigoma maarufu kwa jina hilo.
Wakili: January 2025 unakumbuka nini?
Shahidi wa kificho P6: Nilianza kuwa nimeshiriki siasa za Chadema na kuvutiwa kuwa mwanachama wa Chama hicho.
Nikaanza jitihada za kutafuta viongozi waliopo Songea, nikamfuata kiongozi wa Vijana Chiza na kumueleza nia yangu ya kutaka kuwa mwanaChama.
Wakili: Nini kiliendelea baada ya hapo?
Shahidi wa kificho P6: Alinipokea na kunisifia kwa uamuzi mzuri. Akasema napaswa kuwa na kadi ya Chama, nilifuatilia hiyo kadi na nikaambiwa nisubiri mashine bado ni mbovu na ataendelea kunishirikisha kwenye shughuli za Chama.
Wakili: Zipi hizo shughuli za Chama?
Shahidi wa kificho P6: Sisi bodaboda huwa tunakuwa kwenye misafara ya Chama na bendera.
Wakili: Tar. 04/04/2025 kilitokea nini?
Shahidi wa kificho P6: Hiyo tarehe nikiwa sehemu yangu ya kazi pia nikiwa na simu yangu ya mkononi aina ya infinix smart 8 nikiwa naangalia mtandao wa Youtube.
Wakili: Youtube ni nini?
Shahidi wa kificho P6: ni mtandao wa kijamii ambao unamuwezesha mtu kutuma video, audio na maudhui mengine.
Huyu Bodaboda wa miaka 24 anavyoelezea mambo unashangaaa ni kama anajibu essay huyu atapata tabu kwenye maswali. ๐
Anaendelea kuwa simu yake ilikuwa na internet na aliingia google kumuwezesha kuingia youtube.
Shahidi wa kificho P6: Niliingia kwenye account ya Jambo TV nilifanikiwa kuona na kusikiliza hotuba aliyokuwa anatoa Mwenyekiti wa Chama cha Chadema ambapo alionekana akihutubia watu akisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi hivyo tunaenda kukinukisha.
Tunakwenda kuvuruga Uchaguzi pia nilisikia na kuona akisema tunakwenda kukinukisha na yeyote atakayekuwa pamoja nasi tutakwenda nae na ambae hatataka tutamuacha pia alisema kama kuna mtu yeyote anatarajia kugombea asahau jambo hilo.
Wakili: Pia akasemaje?
Shahidi wa kificho P6: Pia hata mimi kugombea uenyekiti msahau pia akasema bila mabadiliko hakuna Uchaguzi.
Wakili: Kingine kipi?
Shahidi wa kificho P6: Pia akasema watasema tunafanya uasi ni kweli utakuwa ni uasi kwasababu bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Part 169 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.