Nimekusoma kwa miaka mingi. Leo, kupitia final submission yako, nimeona tena kwa nini nimekuwa nikikuchukulia kama kitabu cha kujifunza—hasa kuhusu ujasiri wa kusimama na kutetea unachoamini kuwa ni kweli.
Mungu akipenda, utaendelea kuishi na kushuhudia ukuu wake.
Tundu Lissu—si muhaini.
Wenye utu, semeni Amina.
@Baradhuli2 Nyinyi kweli mazwazwa hiyo ni hela nyie mnaichezea mgetafuta mwanasheria wangewalipa pesa ndefu kunusuru brand sasa mmekimbilia mitandaoni wajinga sana!
Bunge la UJERUMANI likijadili ukatili unaoendelea Tanzanzia.
Dikteta JIKE hizi kauli zako za kishujaa kila siku usiziache-endelea kufunguka yote unayotufanyia watanzania.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
*MUHIMU SANA✍️:* Tafadhali unga mkono wito huu wa dharura wa kupitia upya, kumvua sifa, na kumuondoa Mohamed Chande katika jukumu lake la kitaalamu ndani ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, pamoja na kuanzisha uchunguzi huru nchini Tanzania.
Kwa mshikamano na watu wa Tanzania waliotayarisha mawasilisho haya, tunatoa wito kwa watetezi wa haki za binadamu, mashirika ya kiraia, harakati mbalimbali, na kila anayejali ukweli, haki na uwajibikaji kusimama na kuongeza jina lake kwenye barua hii.
Tunakataa kukubali ukimya, upotoshaji na hali ya kutowajibika mbele ya mauaji ya halaiki. Hatuwezi kuruhusu walioko madarakani kubadili simulizi au kuondoka bila kuwajibishwa.
Haki haitolewi bure—hupiganiwa kwa pamoja na kwa uthabiti. Ongeza sauti yako, unga mkono barua hii, na uwe sehemu ya msukumo unaodai ukweli, uwajibikaji na matokeo halisi.
Pitia na Uunge Mkono Hapa: https://t.co/NH260OD54v
Mwisho wa muda: Jumamosi, tarehe 2 Mei
HAKIKA RC MTAKA UAMINIFU umetupiga chenga. TUTATESEKA sana . Tunaambizana uongo hata kwa yale yaliyo wazi kwa wengi kwamba yalitokea. Hivyo hasira zinapanda, vidonda vinatoneshwa upya badala ya kupona. Halafu tunadanganyana tutaliponya taifa?. HOW?? Kwa kutafuta kafara badala ya KUTUBU NA KUJIREKEBISHA?
#VIDEO Kadri Mwenyezimungu atakavyoniongoza na kunijalia nitaubeba mzigo huu kwa ujasiri, kujiamini na tahadhari kubwa - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza akipokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 ileo. #EastAfricaTV #EastAfricaRadio #RipotiMatukioYaUchaguzi #RipotiMatukioOkt29
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wapokea mapendekezo yote yaliyowasilishwa na tume ya Oktoba 29 na watakayoyasoma na kuahidi kuyafanyia kazi.
Amebainisha hayo leo Alhamis Aprili 23, 2026 Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya tume ya Jaji Chande.
Kiongozi huyo amesema katika kuakisi mapendekezo ya tume, Serikali itachukua hatua za haraka ikiwemo kuunda tume ya maridhiano.