@HildaNewton21@mhabukat@HecheJohn submission ya Katuga haina ata mpangilio, njegere maharage kunde njugu hahahaaa, au kuna submission walikuwa nayo wameandaa ila baada ya lissu kufanya submission wakaona wamepwayaa
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 480
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
Mhe. Lissu anasema Kesi za uhaini sio kesi nyepesi ni kesi ngumu, kunaweza kuwa na presha kubwa na magumu lakini pamoja na ugumu wa kesi hii naona mmefanya kazi nzuri sana, mmetusikiliza, mmenipa nafasi ya kujitetea, hamkunikwaza, mmekuwa wavumilivu sana, mmefanya kazi kubwa, mmefanya kazi nzuri, nilitaka nisimalize bila kusema hayo pengine tusiweze kukutana maana hakuna anayejua kesho
Mawakili wa Serikali nao wamefanya kazi kubwa sana, they had a hopeless kesi, wamepambana, sio mbaya kuwaoa pongezi whichever way you will decide, nawatakieni kila la heri Waheshimiwa Majaji katika tafakari yenu.
Hayo ndio nilitaka yaingie kwenye record waheshimiwa Majaji, msispoyaingiza mtanikwaza,
Watu wamecheka sanaππππππ
Jaji Ndunguru anasema kesi inaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi. Naamini mawakili wa Serikali mtamaliza kesho
Katuga: Sisi tunafocus kwenye kesi naamini tutamaliza kesho sisi hayo maneno ya uzalendo hatuna
Jaji Ndunguru: Shauri litaendelea kesho saa tatu asubuhi kwa upande wa mashtaka kuwasilisha Mawasilisho yao ya mwisho.
Imepigwa High Cooooouuuurrrrtttt
Majaji wanatoka
Watu wamesimama wanapiga makofi mengi sana huku wakiiiimba Mwambaaaa!β¦ Mwambaaaaa!β¦, Mwambaaaa!β¦.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 479
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
Kesi ya Pili ni ya Mahakama Kuu: Saed Kubenea dhdi ya AG Misc Civil Cause No 28 of 2014 HC at DSM 7th October 2014. Mr. Justice Twaib ukurasa 17-21 Mahakama haiwezi ikaingilia migogoro ya kisiasa.
Ni kweli kwamba maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye kesi ya Mtikila na Kubenea yalihusu kesi za jinai yalihusu kesi za madai, swali langu ni je migogoro hiyo ya kisiasa ikigeuza kuwa ya kijinai, Mahakama itakubali kuingilia kisa tu imepakwa rangi za kijinai?
Mimi naiambia Mahakama isikubali kuingizwa kwenye migogoro ya kisiasa haitatoka salama, msimamo ule ule wa kwamba migogoro ya kisiasa isije Mahakamani iendelee na msimamo huo huo vinginevyo wale ambao wanahusika na kufungua kesi wataonea watu wengi sana kama ambavyo wamekuwa wakionea watu kutokana na ushahidi uliopo kwenye kesi hii.
Waheshimiwa Majaji hoja yangu ya mwisho inahusu aina ya mshtakiwa aliyepo mbele yenu.
Mshtakiwa ambaye kwa ushahidi wa DW2, amemuelezea mshtakiwa kwa maneno yako ukurasa wa 885, alisema amenifahamu kwa miaka 23.
DW3 ambaye amenifahamu kwa miaka 20 alisema kwenye ukurasa wa 760 wa record, the accused person is not capable of committing treason.
DW4 aliysema ananifaham kwa miaka 13, accused ni leader of democracy and human rights defender (ukurasa wa 811 wa record)
DW5 ambaye alisema amenifaham for more than 20 years β a person of integrity and honest, a courageous leader who is not afraid to speak the truth (ukurasa 817 wa record) hayo maneno sio ya machawa wangu, hao ni Viongozi na mashahidi ambao nimefanya nao kazi, nimepambana nao pamoja kwenye mapambano ya nchi hii kwa miaka mingi.
Waheshimiwa Majaji kuthibitisha maneno yao angalia ushahidi kwenye record: Makamu Mwenyekiti IDU, Mshindi wa Tuzo mbalimbali, Mbunge wa Kuchaguliwa, Rais wa TLS, angelieni kwenye record then mjiulize kama kweli huyu mtu anaweza kutenda kosa la uhaini, pia mjiulize kwanini Jumuiya za Kimataifa zinanipigania, Mabalozi kila asubuhi wanakuja hapa, UN imesema niachiliwe, Je UN inaweza kuunga mkono uhaini?
Mawaziri wa Jumuiya ya madola wamesema niachiliwe ndani ya siku 30.
Hoja yangu ni kwamba ushahidi wa Jamhuri ni kinyume na picha ya huyu mtu anayedaiwa mhaini, I am a patriotic, am not a traitor.
Waheshimiwa Majaji miaka 60 iliyopita, kuna mhaini mwingine alifungwa kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini, kabla hajahukumiwa alisema maneno yafuatayo ambayo naomba kuyafanya yawe maneno yangu leo,
βI have fought against white domination and I have fought against blood domination, and My Lords, it is an ideal I am prepared to die forβ
Nimepigania haki na Demokrasia kwa sehemu kubwa, kuwa na nchi ya Demokrasia, imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao nipo tayari kufa.
Namalizia kwa neno moja, Waheshimiwa Majaji, kosa la uhaini halina kosa dogo, halina kosa ambalo ukishindwa kuthibitisha uhaini unahukumu kwa kosa dogo, it is either death sentence or acquittal, hakuna kakosa kadogo kwenye uhaini, Waheshimiwa majaji, mzigo ambao mmekabidhiwa mabegani mwenu ni kuamua kama kwa ushahidi huu kuna uhaini, kama mkiona kuna uhaini you should nit hesitate to convict and punish me appropriately, do not hesitate, msiogope.
Kama mtaona kuna uhaini msiogope kunihukumu, kama mkiona hamna uhaini msiogope kuniachia huru, you have God before you, msije mkaletewa maneno kuna kosa dogo hakuna kosa dogo kwenye uhaini, if the evidence doesnβt fit acquit, huo ni mzigo ambao ni wa kwenu peke yenu waheshimiwa majaji.
Nimemaliza
Part 480 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 469
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
Mhe. Lissu anasema, Upande wa mashitaka umeshindwa kabisa na wala hawakujaribu kuthibitisha kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika kutokana na hayo maneno na kwa ushahidi waliouleta tuhuma hiyo haiwezi kuthibitishwa.
Kwahiyo Waheshimiwa Majaji kwenye maswali yote 7 upande wa mashitaka umeshindwa kabisa na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha tuhuma yoyote ile dhidi ya mshitakiwa kwa kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria yaani uthibitisho bila kuacha shaka yoyote.
Sasa Waheshimiwa Majaji. Je ni hayo tu? Upande wa mashitaka umeshindwa na hauwezi kuthibitisha?
Ninachotaka kusema kwa ushahidi ulioko Mahakamani kuna masuala mengine yaliyojitokeza na ambayo yametolewa ushahidi yanayothibitisha kuwepo kwa mashaka makubwa na ya msingi juu ya kesi yote ya upande wa Mashitaka, mashaka makubwa na ya msingi.
Waheshimiwa Majaji eneo la kwanza linaloonesha mashaka makubwa.
Ni kwamba kesi hii yote imetengenezwa na mtu mmoja pengine wawili, underline neno pengine. Kesi yote hii imetengenezwa na mtu mmoja au wawili. Ushahidi unasemaje kuhusu hili?
Huyo mtu ni nani na ushahidi ukoje nianzie hapo??
Huyu Mtu ni Shahidi namba 1 George Wilbard Bagyemu, huyu ndo aliyeamua ku determine kuwa hayo maneno yanatengeneza kosa la Uhaini, ni yeye peke yake.?
Nawaalikeni records ya Mahakama ukurasa wa 145 hadi 146.
Yeye anasema hivi "On 7th april 2025 in the morning i instructed Assistant Insp. Michael to Open two diffrent case files. One for the treason and the second for publication of false infirmation. That order complied with. Treason case opened with no.....
Kwahiyo yeye ndio alimuaru Michael kufungua file la Uhaini na hiyo aliifanya siku nne tu baada ya kuwa ameonyeshwa ile video ya Uhaini katika hizo siku nne hakufanya yafuatayo;
a) PW1 hakuomba Mwongozo wala maekekezo kutoka kwa wakubwa wake wa kazi kabla hajafungua file la Uhaini.
Hakuuliza jamani nifanyaje na hii kitu? Hakuomba guidance from any of his superiors.
Nilimuuliza ulitoa taarifa kwa ZPC akasema hapana, huyo ZPC kamanda wa Polisi wa Kanda ndo mkubwa wake na Boss wake kiutendaji. Je aliomba guidance kwa Ramadhani Kingai ambae ni DCI hata huko hakuomba.
Baada ya kufungua file la Uhaini akasema yafuatyo ; I formed Investigation team and then communicated with DCP Ng'anzi and informed him about opening the treason file and he told me that he add DCP Amin Mahamba as part of the investigating team.
Kwahiyo hakuomba mwongozo kwa mkubwa wake yoyote. Ukurasa wa 158 wa record ndio ushahidi wa kwamba hakuomba ushauri kwa yeyote.
b) PW 1 hakuomba na wala hakupata ushauri wowote wa kisheria kabla hajafungua file na baada ya kufungua file la uhai, na hili nitalirudia kwasababu wanasheria ofisi ya DPP walitupilia mbali wajibu wao wa kisheria.
Ushahidi unasemaje?
Ukurasa wa 159 wa record from 4th/04/2025 to 08/04/2025 I did report to DPP about the treason case. Sikuripoti chochote kuhusu kufunguliwa kesi ya Uhaini na ukurasa wa 162 anasema yafuatayo: The mational Prosecution Act where the offence involve death penalty the DPP's office must be informed.
The NPS Act provide that the DPP must be informed on the investigation of the offence.
Kwahiyo PW 1 anatambua sheria inataka nini? Kwamba lazima DPP ajulishwe na mimi sikumjulisha. Halafu anasema DPP alikuwa anapata taarifa mtandaoni na kwahiyo alikuwa anaratibu.
Alikuwa anapataje taarifa mtandaoni wakati nyie hamkumjulisha? Mimi katika mashahidi 17 waliokuja sikumuona DPP wala maafisa wake kuja kusema kuhusu kusimamia upelelezi wa shauri hili.
c) Hiyo timu ya Wapelelezi haikuwa na Mwanasheria hata mmoja. The investigation team no a single lawyer involved, ambae angeweza kuwashauri juu ya matakwa ya sheria.
Part 470 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISSU
*LISSU:* Sasa naomba nimalizie.
*JAJI NDUNGURU:* Je, ni sehemu ya submission?
*LISSU:* Ni sehemu ya submission, wala si maneno mabaya.
Ni hivi, Waheshimiwa Majaji, kesi ya uhaini ni kesi ngumu sana.
Ukiachilia mbali siasa zake, ambazo pressure zake ndizo zinafanya kesi kuwa ngumu.
Pamoja na kesi kuwa ngumu, nyinyi Majaji mmefanya kazi nzuri sana.
Mmetusikiliza, mmetupa nafasi ya kujitetea.
Hamjanikwaza.
Mmekuwa wavumilivu sana.
Mmefanya kazi kubwa sana na mmefanya kazi nzuri sana.
Nilitaka nisimalize bila kusema haya, pengine hatutakutana tena.
Nilitaka mjue kuwa moyoni mwangu mmefanya kazi nzuri.
Hawa mawakili wangu wa Serikali na wao wamefanya kazi nzuri.
Wamepambana sana mpaka kufika hapa. Pamoja wamekuwa na kesi ya ovyo sana.
Ila wamepambana sana bila kujali nini kitatokea, wamepambana sana.
Nafikiri nawatakieni heri sana.
Asanteni sana.
Haya ndiyo nilitaka yaingie katika rekodi.
Nafikiri msipoyaingiza katika rekodi, mtanikwaza.
Kama mgongo wako uko salama na unaendelea kuulinda wivu mkubwa please mchangie pesa ili aweze kulipa hiyo faini.
Airtel Money : 0789416464 (Airtel money)
Jina: GODFREY WILLIAM
#LindaMgongoWako#HaliNiMbaya