Hatua za Kufuata Jino liking'oka bahati mbaya ili kuliokoa! ๐งต
#SundayDentalTips Retweet
Je wajua kua jino likitoka kunauwezekano mkubwa wa kulirudishia na likapona, ukaepuka adha ya kua na pengo!? Fuatana namm kwenye hatua za kufuata ili kulifanikisha hili,,,,๐
#DentalCare
Dentistry is unlocking smiles and enhancing lives through meticulous esthetic and transformative procedures.
This how far veneering can improve your smile, quality of life and overall well-being.
#Healthy smile is contagious
#Smile with confidence
#OralHealthAdvocate#Esthetic
@Dioniz__@wizara_afyatz@ummymwalimu Ifikie hatua tuboreshe mifumo yetu ituwezeshe kufanya online prescriptions ili popote mgonjwa aweze kupata huduma na dawa zake still medical records zake zieepo online itasaidia sanaa kuondoa hizi changamoto za handwriting na drug resistance
Puuza wahuni wanaosema hiyo dawa ya meno yenye fluoride Ina madhara, kama ni hivo watu wa Mwanza, Arusha na Singinda ambao fluoride ya kwenye maji imezidi hadi inabadilisha rangi ya meno ndo wangekua wa kwanza kuumwa haswaa.
Dawa yenye madini ya fluoride imethibitishwa na WHO
Waziri wa Afya, @ummymwalimu habari za jioni?
Jumla ya Polyclinics zaidi ya 150 zimekwama kusajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (@nhiftz) wakati vituo hivyo vimekidhi vigezo vyote vilivyoainishwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Baadhi ya Polyclinics vimeshafanyiwa tathmini na ukaguzi na kuonekana kuwa na sifa za kusajiliwa ili kuhudumia wanufaika wa Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya.
Baadhi ya Watoa huduma wamedai kwamba baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wamekua wakifuatilia maombi yao katika Ofisi za Mfuko na mara zote wamekua wakijulishwa na kupewa jibu moja tu kwamba kuna zuio kutoka Wizara ya Afya juu ya usajili wa Polyclinics katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Wizara ya Afya imeshindwa kutambua juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani kupitia sekta ya afya kwa kuweka zuio bila kutoa taarifa kwa wadau juu ya sababu zake na pengine zuio hilo linalenga kutatua nini, na litadumu kwa muda gani.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi ya maandishi juu ya zuio hilo na hivyo kupelekea sintofahamu kwa wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kwa wamiliki wa vituo husika.
Zuio hilo limeathiri upatikanaji wa huduma bora za afya ikiwemo huduma za kibingwa na huduma za kibobezi kama usafishaji wa damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Dialysis).
Hali hiyo inaweza kupelekea usumbufu mkubwa kwa wananchi hasa walio mbali na huduma hizo na walio maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hizo.
Kitendo cha Wizara ya Afya kuweka zuio la kusajili vituo vipya vya kutolea huduma za kibingwa na huduma nyingine muhimu za afya inaweza kutafsiriwa kama kwenda kinyume na sera ya Bima ya Afya kwa wote.
Pia ni hujuma dhidi ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wote ikiwemo wale wa kipato cha chini wanafikiwa na huduma muhimu za afya ikiwemo huduma za kibingwa.
Ni Dhahiri zuio hilo limeathiri kwa kiwango kikubwa uwekezaji mkubwa na wa kisasa uliofanywa na wengi wa wamiliki wa kliniki hizo ambao baadhi yao ni madaktari na wastaafu.
Kuna Ushahidi kuwa baadhi yao wameshaanza kufunga vituo vya kutolea huduma huku ambao wanaendelea wakitoa huduma kwa kusuasua huku wakikabiliwa na madeni makubwa katika taasisi za kifedha na mabenki.
Wakati kilio kikubwa cha wananchi na hasa vijana ikiwa ni suala la ukosefu wa ajira, inashangaza na inasikitisha kuona maelfu ya ajira kwa wataalamu wa afya wakiwemo madaktari, wauguzi, wafamasia, wataalamu wa maabara na wataalamu wengine wa kada mbalimbali wakipoteza ajira zao kutokana na zuio hilo.
Hatua ya kuzuia vituo vipya vya kutolea huduma za kibingwa na kibobezi (Polyclinic na Specialized Polyclinic) kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ni pigo kubwa kwa ukuaji na uboreshaji wa sekta ya afya kwa ujumla.
Zuio hili kwa watoa huduma hizo linafifisha juhudi za utoaji wa huduma za kibingwa na kibobezi na linaweza kupelekea kudorora kama sio kuanguka kabisa kwa uwekezaji wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma bora za afya.
Gharama za uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za kibingwa na kibobezi (Polyclinic na Specialized Polyclinic) ni kuanzia walau kiasi cha Shilingi Milioni thelathini kwa mwezi kutegemeana na aina ya huduma zinazotolewa, hali ya miundombinu na idadi na aina ya watumishi katika kituo husika.
Katika kipindi chote cha zuio Polyclinics zimehudumia wagonjwa kwa kiwango cha chini cha ufanisi unaokadiriwa kufikia 97% licha ya kutumia kiasi cha zaidi ya takribani Sh360 Milioni kwa mwaka.
Hizi ni kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara, kodi ya pango, kodi za kimamlaka na gharama nyingine za uendeshaji, ambapo gharama hii ni nje ya ile iliyotumika kufanya uwekezaji.
Kutokana na zuio hilo la kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF vituo husika vimekuwa vikifanya kazi chini ya uwezo wao na kupelekea serikali kupoteza mapato ya kodi iwapo vituo hivyo vingeweza kufanya kazi kwa uhuru kadiri ya uwezo wao.
MMM, Martin Maranja Masese.
Great recognition Doctor, imagine sorting lesions in an OPG, designing prosthesis, doing endodontic work, restorations, crown build-up and implantology. ItIt's really a fine art work in medicine.