Tangu October 29, 2025! Hatujawahi kupumzika! 😂
Hii bandika bandua ya matukio imebeba lengo gani, na inatupeleka wapi?
Mara Wema kajifungua. Punde si punde, Zuchu na baby shower. Hatujakaa sawa, mara tunasikia matangazo ya tamasha la miaka 30 ya Bongo Flavour ya wale wale wasanii wa zama za mawe! 😂
Tunaanza kukaa sawa, mara tunakutana na habari ya Dotto kaathirika, tena analeta vipimo kutoka Zanzibar. 😂
Ile tumeanza kutulia na kufuatilia kesi ya Mzalendo Tundu Lissu Mahakama Kuu, Na jinsi anavyowapelekea moto Mawakili wa Jamhuri, tunakutana na taarifa njema iliyomgusa kila Mtanzania: Makamu wa Rais, Emmanuel Nchimbi, ametoa kauli nzito akiwataka Watanzania kuungana na kudai Katiba Mpya na bora.
Wakati bado tunafurahia kauli ya Makamu wa Rais kuhusu mapambano ya Katiba Mpya na kabla hata hatujakubali kwamba Wema amekuwa single mother tunashtushwa na barua kwamba Makamu wa Rais, Mhe. Emmanuel Nchimbi, amejiuzulu nafasi hiyo na kuachana na siasa!
Tukiwa bado hatujamaliza kujiuliza: “Imekuwaje Makamu wa Rais amejiuzulu? Na kwa sababu gani?” asubuhi tunakutana na habari nyingine kwamba CCM imemfukuza uanachama Emmanuel Nchimbi. Mara kidogo hapatikani na hajulikani alipo!
Hapo hapo, kabla hata hatujapoa, Makamu mpya wa Rais anateuliwa, anapitishwa na Bunge na kuapishwa kuwa Makamu mpya wa Rais!
Ile tunasema, “Sasa basi, tutulie kidogo” tunakutana na breaking news nyingine:
Mwamposer kaangusha mchawi huko Arusha, aliyekuwa anatoka Bariadi kwenda Mbeya! 😂😂😂
Aisee… What a Controversy 😂
Muda huu nikiwa naandika post hii jamaa yangu amenionyesha video ya Chidi Benzi wa bei za jioni asiye na kitambi akitambulika kwa jina la kisanii kama "King Basta Mnyama" Nimeshindwa kuendelea kuandika zaidi ya kuanza kumsikiliza!
Again "When they cannot answer the argument, they change the agenda; when they cannot solve the problem, they create noise. Diversion is not a solution; it is a tactic to steal the public’s attention, distract from the real issue, and leave the actual problem unresolved".
"Nawaomba watanzania wampuuze mzee Butiku, nafiki Mwl. Nyerere angekuwepo angesikitika sana kama mzee ambaye amewahi kuwa msaidizi wake. Amesema chama chetu kinapokea fedha kutoka marekani, huyu ni mtu ambaye amewahi kuwa Katibu wa Rais." Mhe. @HecheJohn