HISTORIA HAIKUMBUKI MACHAWA
Nimeona clip ya MWIJAKU akikejeli jitihada za Wanataaluma kumsaidia mwenzao ambae anashikiliwa na Polisi. Amebeza kiasi cha fedha kilichochangwa, na kuweka msisitizo wa kutahadharisha watu kwenda kinyume na matakwa ya WATAWALA, maana watakamatwa na hela za kujichanga zisitoshe.
Sijataka kuiweka Clip hapa maana nitakuwa naisaidia kufika mbali. Ila hii level ya UCHAWA ni lazima tuikemee!
Kama wewe hauna kitu ambacho unakisimamia, hauna principles wala muelekeo kama MTU HURU au mwanaume aliyekamilika, basi usitie neno/kauli kwenye Harakati za Watu ambao wanajitambua.
Kama wewe umeamua kujivunjia HESHIMA, KUUZA UTU wako, na KUINGILIWA MAKALIONI ili uishi SOFT LIFE, jua kuwa wengine wanakula na kuishi kwa jasho kama isemavyo BIBLIA (na naamini QURAN pia).
Wewe ambae unawachekaga Chawa Wenzako kuwa hawajasoma na wewe ni Msomi, alafu unakuja kuwadhihaki Wasomi ili uwafurahishe Watesi wao? You are an enabler of a repressive regime, which makes you as guilty as they are!
HELA sio kila kitu maishani! Na historia ya dunia haikumbuki hela bali UJASIRI, MSIMAMO, FALSAFA, MABADILIKO, KUJITOA KAFARA, etc MANSA KANKAN MUSSA alikuwa tajiri ila hamna anayemuwaza kwenye ulimwengi wa ELON MUSK
Hakuna CHAWA aliyejengewa Sanamu wala kuandikwa kwenye Kumbukumbu. Ila MASANAMU, VITABU, MITAA NA MAJENGO yanaimba story za Thomas Sankara, Che Guevara, Patrice Lumumba, Martin Luther King, Malcolm X, Steve Biko, nk. Na wameuwawa hata shilingi 10 hawana!!
Na amini nakwambia, Miaka 100 mbele, MWIJAKU hutokumbukwa, ila HUMPHREY POLEPOLE, DEUS SOKA, MDUDE NYAGALI, BEN SAANANE, CHRISTOPHER MTIKILA watakumbukwa kama tunavyowakumbuka KINJEKITILE NGWALE, CHIEF MKWAWA, NYERERE…
And by the way, Maisha niliyoishi mimi, Maria Sarungi, Mange Kimambi, nk wewe hata robo hujaishi, but still chose to stand on what’s right.
Dar Es Salaam umeanza julikana 2018 sijui, ndio uje kutaka kufundisha watu Maisha na kuongelea Hela? smh
KAMA HAUNA LA MAANA LA KUSEMA, KAA KIMYA
The Leader
Wazee wa Back stage.....!
kukaa kwetu hapa ndiyo kumetufanya tuone Vibaka wanaingia na mapanga na pilipili kuelekea Jukwaa la Viongozi.
Leo ndiyo nimejua bado nipo fit bado.
Kama siyo kuishi China kidogo ungekuta wamekata kitambi kama mkate.
Wakati tunapambana Raia na wao wakaona.