"Katika kuendeleza mpango wangu wa kukutana na makundi mbalimbali, kundi la machifu bado sijakutana nalo, hivyo basi najipanga nikutane nanyi ili tuweze kujadili changamoto zote, jinsi tutakavyoweza kuzifanyia kazi na Mipango yenu ya baadae."
@SuluhuSamia
"Niagize wizara katika mchakato wa maandalizi ya sera hii lazima tuchukie maoni kwa machifu wetu, maoni yao yaingizwe kwenye sera hii ili tuendeleze utamaduni wetu. Hatua hizi zitasaidia kulinda, kuenzi, kukuza na kuendeleza utamaduni wetu." @SuluhuSamia
"Mwakani nchi yetu itafanya zoezi la Sensa viongozi wa kimila nawasihi muwahimize wananchi kushiriki zoezi hilo kwasababu ni muhimu katika maendeleo ya nchi" Rais Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Utamaduni, Mila na Desturi zetu lililoandaliwa na na Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) katika Viwanja vya Redcross - Magu, Mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amekuwa Chifu mkuu, chifu wa machifu wote Tanzania, ambapo amepewa jina la kitamaduni la Chifu 'Hangaya', likiwa na maana ya nyota Inayong'aa.
"Utamaduni unasaidia kutunza na kurihisha maadili kutoka kizazi kimoja kwenda kingine,ninawapongeza Umoja wa Watemi wa Wasukuma kwa kuandaa Tamasha hili la Utamaduni.Naamini Watanzania mnajifunza mambo ikiwemo mila na desturi za Wasukuma" @SuluhuSamia
"Kwenye masuala ya kujenga masoko, masuala ya maji najua bado ni changamoto katika maeneo mengi, lakini tunaweka nguvu kwenye mradi wa Butimba ili maji yasogee kwa wananchi." - Rais @SuluhuSamia Hassan, mkoani Mwanza
"Katika kuendeleza mpango wangu wa kukutana na makundi mbalimbali, kundi la machifu bado sijakutana nalo, hivyo basi najipanga nikutane nanyi ili tuweze kujadili changamoto zote, jinsi tutakavyoweza kuzifanyia kazi na Mipango yenu ya baadae."
@SuluhuSamia
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Fedha la Kimataifa #IMF@IMFNews, limeidhinishia #Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 567.25 sawa na shilingi za Tanzania tril 1.3 kwa ajili ya kukabiliana na athari za ugonjwa wa UVIKO 19.
"Tupo kwenye mchakato wa kuanzisha sera mpya ya utamaduni itakayo endana na mazingira ya Sasa ya dunia lakini itakayo linda maadili yetu." - Rais @SuluhuSamia
Waziri wa @ortamisemitz @ummymwalimu amekabidhi pikipiki 74 kwa Makatibu Wasaidizi Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu zenye thamani ya mil.218.Waziri amesema lengo ni kuboresha utendaji kazi wa tume hasa katika kutembelea walimu ili kusikiliza na kutatua changamoto
"Ningependa kusikia mkoa mwingine mwakani wanafanya Tamasha kama hili na kutuonyesha mila na desturi. Matamasha haya yazunguke kila mkoa ili Watanzania wajue mila na desturi zetu kila mkoa na kila pembe ya Tanzania." - Rais Samia Suluhu akiwa Kisesa, Mwanza.
#RAISSAMIAMWANZA Nimekuja kwa tukio la kufunga Tamasha letu la Utamaduni hapa Mwanza. Wiki nzima sasa tunazunguka Tanzania tukichukua vivutio na maeneo yetu ya muhimu kuyaonesha ulimwenguni, na hayo ni pamoja na Tamasha hili - @SuluhuSamia
Rais @SuluhuSamia ameahidi kuanzisha mashindano maalumu yatakayoshindanisha michezo ya kitamaduni kote nchini yatakayoitwa "Hangaya", likiwa ni jina lake jipya alilopewa na machifu wa Kisukuma,leo Septemba 8 akiwa Kisesa Mwanza.