Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, ametoa rai kwa wenyeviti wa mitaa na askari polisi wa ngazi ya kata kushirikiana kwa karibu katika kulinda amani na usalama wa wananchi ndani ya wilaya hiyo.
Wito huo umetolewa leo katika kikao kazi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam, kikihusisha viongozi wa Polisi wa Mkoa na Wilaya, watendaji wa kata na wenyeviti wa serikali za mitaa.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Mpogolo amesema ulinzi na usalama wa wananchi unaanzia katika ngazi ya mtaa, hivyo ni wajibu wa viongozi hao kufanya kazi kwa umoja na mshikamano ili kuhakikisha Ilala inaendelea kuwa mahali salama kwa shughuli za kijamii na kiuchumi. “Ulinzi na usalama unaanzia kwenye mtaa, hivyo ushirikiano wenu ndiyo nguzo ya amani ya wilaya yetu,” amesema.
Aidha, amewataka viongozi hao kuwa walezi wa vijana, wakiwamo waendesha bodaboda na wamachinga, akibainisha kuwa makundi hayo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa kila siku na yanahitaji mwongozo ili yasigeuke kuwa chanzo cha vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa miundombinu yote ya serikali iliyoharibiwa baada ya Uchaguzi Mkuu inaendelea kukarabatiwa ili huduma kwa wananchi zirudi katika hali ya kawaida. Amesema baadhi ya ofisi za serikali na vituo vya polisi vilipata uharibifu, jambo lililosababisha wananchi kukosa huduma muhimu kwa muda.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kipolisi Ilala (RPC), Mgonja, aliwahimiza wananchi kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu au matukio yanayoweza kuhatarisha amani katika maeneo yao, akisisitiza kuwa taarifa zao ni sehemu muhimu ya kuimarisha ulinzi wa mtaa.
Kikao kazi hicho kililenga kuweka mikakati imara ya kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote ya Wilaya ya Ilala, huku viongozi wakiahidi kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha jamii inaendelea kuishi kwa amani na utulivu.
BREAKING! Tanzania NGOs admit receiving $2m from Ford Foundation to fund thousands of protestors who participated in the October 29th demos. The demos that the government declared unlawful led to looting and burning down of government and private property. Tanzania police had to use lethal force to thwart the criminal acts.
#CNNFakeNews #BBCFakeNews