VIDEO:
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, ameeleza kuwa kesi za jinai hazianzi mahakamani wala polisi pekee, bali huanzia katika jamii ambako matukio ya kihalifu hutokea.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa wadau kuhusu ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki mahakamani katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Jaji Mkuu alibainisha kuwa mhalifu anapotenda kosa, vyombo vya sheria kama polisi wakati mwingine huwa hawapo eneo la tukio, hivyo ni muhimu jamii kutoa taarifa.
"Kosa limetendeka kabisa mtu kauawa pale, watu wanajua hawataki kujitolea kutoa taarifa, nani amemuua huyu mtu, sasa polisi unamlaumuje? Kwa hiyo kesi ya jinai inaanza kwenye jamii tu huko tukio lilipotokea," alisema Jaji Mkuu Masaju.
Jaji Mkuu alieleza kuwa mnyororo wa haki jinai ni mpana na mrefu, ukianzia kwenye jamii, ukienda vyombo vya uchunguzi kama Polisi, Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kisha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Mahakamani, na hatimaye gerezani kwa ajili ya marekebisho ya tabia.
Alisisitiza kuwa licha ya kuwa mnyororo huo ni imara, mahakama haiwezi kuwa na ufanisi peke yake ikiwa hatua za awali kabla ya kuingia mahakamani hazijafanya kazi mapema na kwa ufanisi.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Mtaa wa Kinyerezi, Mchungaji Maotola Lumbe, amemshukuru Waziri Mkuu na Serikali kwa msaada walioutoa baada ya wanakwaya wa kanisa hilo kupata ajali eneo la Bahi, ikiwemo kuwezesha waliokuwa wakihitaji matibabu zaidi kusafirishwa hadi Dar es Salaam.
โYapo mambo ambayo fedha inaweza kuyapima, lakini yapo ambayo thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha. Kwetu sisi, ule haukuwa msaada wa kifedha pekee; ulikuwa ujumbe wa faraja, upendo na mshikamano katika kipindi kigumu tulichokipitia,โ amesema Mchungaji Lumbe.
-----------------------
Aliyasema hayo jana, Jumamosi Septemba 19, 2026
Wakati wa Ibada ya Kufunga Makambi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato yaliyofanyika kwa siku saba katika kanisa hilo, Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.
Huyu bwana Mushi na familia yake yote wanakamatwa na kuwekwa sero kwa kosa gani wazee?๐ค
Ni takwa la kisheria kwamba nikiitwa au kualikwa na Mkuu wa Mkoa ninapaswa kuwepo au ndio ubabe?๐ค
#BREAKING: KINGAI AKATAA KUMTETEA LISSU MAHAKAMANI KESI YA UHAINI
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Tanzania, DCI Ramadhan Kingai amekataa kumtetea Lissu katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Taifa.
Aidha, Kutokana na hayo hata Wakuu wengine wa Majeshi nchini hapo nao hawataenda kumtetea hivyo Tundu Lissu amefunga mashahidi wake na ameomba Jumatano ijayo kwenda kufanya majumuisho ya mwisho kabla ya hukumu kutolewa na Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar Es Salaam
Zaidi: https://t.co/9pJqvoLlu2
Msanii wa Bongo Fleva Godfrey Tumaini 'DUDU BAYA' akizungumzia amri iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi kwa Jeshi la Polisi kumkamata na kumpima baada ya Dudu Baya kukaidi wito wa kufika ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Dudu baya amesema kupigania kwake haki na kusema ukweli ndio sababu ya kusingiziwa mambo yasiyofaa juu yake.