"Samia, kesi ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu imekushinda na hamna ushahidi wowote wa kuuthibitishia umma. Tafuta njia nyingine ya ushindani wa kisiasa badala ya kutumia mahakama. Muachieni Tundu Lissu sasa hivi! #FreeTunduLissu"
Tunapoadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Kenya ninatoa pongezi kwa majirani zetu na ninaleta kumbukizi ya wasifu wangu rasmi kwa Hayati RAILA AMOLO ODINGA NA UJASIRI WAKE KUCHAGUA AMANI BADALA YA MADARAKA 2007. Tumuenzi na kujifunza kutoka kwake katika changamoto zinazotukabili leo. Apumzike kwa amani.
Baada ya miaka mingi ya kifungo na mateso, kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga alikabiliwa na wakati ambao vurugu zingempa ushindi. Badala yake, alichagua maridhianoโna kwa kufanya hivyo, akaokoa demokrasia ya taifa lake.
Nilibahatika kufanya kazi kwa karibu na Raila akiwa waziri wa Ardhi na mimi nikiwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat, na pia Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi (UNON). Kwa hiyo ninaandika kwa undani.
"Mazishi ya Raila Amolo Odinga yanafunga sura ndefu ya historia ya kisiasa ya Kenyaโna Afrika kwa ujumla. Anaacha nyuma si tu rekodi ya upinzani na mageuzi, bali pia mfano wa jambo adimu zaidi: kiongozi ambaye, baada ya kuonja ukatili wa madaraka, alikataa kuwarudishia wengine ukatili huo.
Maisha ya kisiasa ya Odinga hayawezi kutenganishwa na miaka yake ya kifungo katika miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990. Aliwekwa kuzuizini bila kupelekwa mahakamani kwa takribani miaka minane, akiteswa kwa upweke na udhalilishaji katika seli maarufu za Nyayo House. Miaka hiyo ingeweza kumgeuza mtu yeyote kuwa mwenye kisasi. Badala yake, ilimjenga kuwa na nidhamu. Alitoka gerezani akiwa na imani isiyotetereka kwamba demokrasia, hata ikiwa na mapungufu, ni salama kuliko vurugu.
Imani hiyo ilijaribiwa mwaka 2007 -2008 wakati wa machafuko ya uchaguzi uliohatarisha na kulisukuma taifa la Kenya hadi ukingoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kuhesabu kura kulivurugika; jamii pinzani zilihamasishwa kila moja kutetea upande wake; mamia ya watu walipoteza maisha. Ndani ya makao ya Umoja wa Mataifa Nairobi, tulihisi uzito wa historia ukibisha mlangoni. Tukahofu bila kuchukua hatua maalum nchi itasambaratika.
Kama mkuu wa mfumo wa UN nchini Kenya, niliripoti moja kwa moja kwa Katibu Mkuu Ban ki Moon huko New York kuhusu hali halisi na athari zake kwa Kenya na nchi jirani zote ikiwa machafuko hayatadhibiwa. Nilipendekeza kuangalia uwezekano wa mfumo wa kugawana madaraka. Pia nilimshauri aliyekuwa mkuu wangu mstaafu, Kofi Annan, akiwa Ghana wakati huo, naye alikubaliana kuwa upatanishi ulikuwa muhimu na kugawana madaraka kungetuliza mtafaruku. Tulihitaji kwanza kuungwa mkono na mataifa makubwa na Umoja wa Afrika.
Kupitia rafiki yangu Mary Chinery-Hesse, Makamu mtendaji mkuu wa ILO mstaafu, akiwa mshauri wa Rais Kufuor wa Ghana ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, nilifikisha ujumbe huo Accra. Tuliamini Waafrika walipaswa kuhamasisha dunia kuisaidia Kenya kabla ya mgogoro haujateketeza ukanda nzima.
Ndipo wazo la serikali ya mseto likaanza kukubaliwa na kusambaa kati ya UN, Umoja wa Afrika, na washirika wa kimataifa. Nilipotoa taarifa kwa washirika Nairobi, niliwasihi maafisa wa Marekani na viongozi wakuu waliotembelea nchi hiyo kufikiria upya kauli zao za mapema za pongezi kwa Rais Kibaki zilizokuwa zikifunga mlango wa mazungumzo. Nilizungumza si tu kama afisa mwandamizi wa UN, bali pia kama mzaliwa wa eneo la Maziwa Makuu niliyeshuhudia tangu nikiwa mtoto mdogo tatizo la wakimbizi wa kwanza wa Rwanda wakivuka mpaka wa Kagera mwaka 1959, kabla ya Uhuru wa nchi yangu Tanganyika. Baba yangu aliwapokea wakimbizi wengi kama 20 nyumbani na mama akalazimika kuwapikia na mimi nilimenya ndizi mikungu mitatu peke yangu mara niliporudi kutoka shule kwa ajili ya chakula chao. Kumbukumbu hiyo haikuniacha kamwe hadi leo. Amani ikivurugika mateso ni kwa wengi hata wa mbali.
Mantiki tuliyotumia kwa Kenya ilikuwa rahisi lakini ya mapinduzi: pale uchaguzi unapopingwa hadi kumwagika damu, uhalali wake uko mashakani na unaweza kurejeshwa tu kupitia muafaka kwa ushirikishwaji kukiri makosa na kutenda haki. Inahitaji ujasiri kutoka pande zote.
It's been a week since we released our Tanzanian investigation.
The government has attacked CNN's reporting in two separate press conferences but did not point out a single lie. They have still not responded to our questions
Kayunga from different angles looks as if weโve gone to war with them. They have the guns, yet they are fighting President Kyagulanyi, @HEBobiwine, who stands only with the flag, the microphone, and the camera. #ANewUgandaNow