Leo nimeamka na Amani na Furaha na Energy niliyoikosa kwa siku tano.
Jana ndugu yetu @prossoff alihangahika kuhakikisha kuwa anafika Hospital ambayo Sativa yupo. Lakini cha kushangaza Prosper alivofika pale cha kwanza Sativa alihitaji mawasiliano yangu kabla ya yote. Kwa Love aliyokuwa nayo Prosper alimpa simu ndogo na pia akampa laini. Simu ilikuwa haina chaji akamwambia ukifika utai boost utawasiliana na Taivina ntampa namba ambayo ipo humu atakupigia.
Prosper akanicheck akanipa namba ambayo Sativa kaachiwa na kunambia kuwa akifika ndani ya msaa mawili matatu utampigia anataka kuongea na wewe nikasema sawa. Hiyo ilikuwa ni saa 12:02 jioni kilichonishangaza saa 12:10 jioni napata Dm kutoka kwenye account ya X ya Sativa ikiandika "My G" Binafsi niliogopa kwasababu najua mtu yupo kwenye Ambulance anawezaje kunitext mimi Twitter na hana simu. Mimi niliona siko sawa nikaomba msaada kwa Brother @TitoMagoti kwasababu yeye na brother @IAMartin_ ni watu ambao wamekuwa wakini protect kwa namna yoyote kuhakikisha nakuwa salama kwa kipindi hichi. Brother Tito akanambia its okay unaweza ukajibu hiyo message mimi nikajibu "Yes Say Something Bro" After pale ikaingia meseji nyingine kutoka kwenye account ya Sativa usiku saa 4:10 ikisema nipe namba nikapata wasiwasi zaidi kuwa hapa sasa usalama unazidi kuwa mdogo ikabidi nimcheck tena Brother Tito akani connect na Brother Martin. Martin akaniambia cha kufanya nisijibu Meseji na Pia nikilala nizime simu Asubuhi atakuja kunichukua Home.
Usiku tena saa 10:52 ilipigwa simu mara nne na namba moja sikupokea kama nilivopewa maelekezo Lastly ikaingia message kuwa Mgonjwa anataka kuongea na wew mimi ni nurse. Ikabidi nihakikishe kwa Brother Patrick kama ile namba kweli ni ya Nurse akaniambia ni yeye simu bado inaita nikapokea. Direct naambiwa ongea naye. Ile Kuongea naye kuskia Sauti yangu niliskia Kicheko kwa mara ya kwanza cha Mwanangu swali la kwanza kuuliza upo salama? Nikajibu ndio akauliza upo wapi nikwambia nipo Ghetto kwako nimepoa akasema unavoondoka beba na PC yangu kamalizie vimeo. Nikamuuliza yule aliyekuwa ananitext kwenye account yako ya X ni wewe akasema ndio ni mimi nikiwa kwenye ambulance niliomba Nurse a log in account yangu niku dm niliona nachelewa kufika ili niongee na wewe naumwa lakini wasiwasi wangu wote ulikuwa kwako pia nilipata na sekunde kama 50 hivi za ku scroll Timeline.
Nimeona Love ya watu wa X waambie nashukuru sana sana Mungu awabariki Inshaallah akipona atakuja kutoa shukrani zake za dhati.
Bado nashindwa kuelewa ni kwanini Sativa amekuwa akiwa na hofu kubwa kuhusu mimi kiasi cha kupambana kiasi hicho kupata mawasiliano yangu lakini mimi niko sawa ndugu zangu nashukuru sana uwepo wenu unannifariji.
Pokeeni Salamuza SATIVA
Namba za Familia na Lipa Namba kwa ajili ya Mchango wa Sativa
VODACOM
0769916759
Israel Patrick
AIRTEL
0699742232
James Nelson
Lipa Namba ya Voda
5012993
iPhone FIX
Update ya Michango kwa Leo tuishie hapa tutaamka nayo kesho 🙏
Asanteni kwa Moyo wa kujitolea, Mmeonesha kwamba X ni Familia kubwa, Mungu azidi kuwabariki tusishikane kwenye shida tu na kwenye raha ☺️
Tusimshike mmoja tu bali tushike wote wanaohitaji Msaada wetu, Usiku Mwema Fam💜
TAARIFA; @Sativa255 amehojiwa na RCO - Katavi muda siyo mrefu akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi. Sijui Afande RCO atafanya nini na hiyo taarifa. Story ya SATIVA inatisha na kuogopesha sana. Jua likiwaka, tutasimulia. SATIVA kanisimulia pia. Kuna watesaji Serikalini.💔
Bro & everyone: I see your mentions.
It is a NO bargain when one of us is held btn life & death: a judgment you wouldn't wish to endure.
So, this is a THANK YOU to all of us. Our voices, our strength.
Mdogo wangu @MiriamMkanaka - I'm so proud of you🫶
Nimemsikiliza Sativa, nimepata maumivu makubwa sana. Nimetafakari mno video yake na maneno yake.
Namfahamu Sativa nje ya mitandao. Nimefanya nae kazi. Ni kijana mcheshi na mwenye uwezo mkubwa sana wa kupembua mambo.
Nilikutana nae 2018. Nilifanya nae kazi kwenye page yangu ya habari Sportpanel Instagram.
Baadae akaniambia brother nimefiwa. I think alikuwa baba yake mzazi (stand to be corrected). Hivyo majukumu ya kulea familia yalihamia kwake. Alinieleza nyakati ngumu alizopita.
At that time nilikuwa na dili moja tu la ubalozi ambapo ilikuwa kampuni moja ya betting, nilikuwa nalipwa 80,000.
Kiasi hicho nilimpa Sativa agawane na kijana mmoja ambaye alikuwa anapost nae. Nilimwambia achukue kiasi kile nikiamini kingemsaidia.
Ghafla Sativa akanimbia bro nimekwama nahitaji kuacha chuo kwani mama hawezi kuendelea kunilipia ada.
Nahitaji nipambane nje ya elimu. Nilimsihi sana asiache lakini nikagundua hakuwa na namna
Kweli akaendelea na biashara nyingine.
Mojawapo nahisi ilikuwa kuuza simu Makumbusho. From there tuliendelea kuwasiliana mpaka niliposikia amepotea.
Sijui sativa amemkosea nani na amemkosea nini. Sijui aliyepima hii adhabu aliyotoa kwa Sativa ametumia kigezo gani.
Sativa ni kijana mdogo sana ambaye nyuma yake amebeba hatma ya wengi mno.
Tanzania ni nchi ya amani, natamani tuendelee kuenzi Amri iliyokuu kuliko yote nayo ni AMRI YA UPENDO. Upendo ukikosekana UOVU HUTAMALAKI. Na Mungu sikuzote hachangamani ni upendo.
Tusiruhusu UOVU wa namna hii uwe agenda na kilio cha wengi. Vilio na machozi ya namna hii vinaacha makovu ambayo yataondoa uzuri wa TAIFA letu. 🙏🏾
A small request to carpet journalists. Muacheni Edga atibiwe na awe sawa. Btw you did not show up when he needed you most. Stop intruding his privacy, you bloody hypocrites.
Msiwe watu wa kupuuzia hisia zenu sometimes zina maana kubwa.
Baada ya kuona video ya Sativa akihojiwa na kudai alikuwa Oysterbay nikakumbuka Jumatatu nilipelekwa na gari ya @millardayo Oysterbay nikakutana na Brother Patrick baada ya kupata majibu yasiyo na matumaini nilimuuliza Patrick @PatrickMnyama96 kuwa saizi kituo wapi akaniambia twende makumbusho. Nikamwambia hapana tusubiri hapa hapa Oysterbay mimi ntakuwa naangalia magari yanayoingia kituoni nione kama kuna mtu anafanania na Sativa atashuka mpaka tutakapopata taarifa za wakina Aunt huko walipo wamepata nini kwenye kituo walichoenda wao.
Huwezi amini mpaka Patrick ana request Bolt kuondoka mimi aliniacha pale pale ingawa sielewi nilikuwa nasubiri nini. Waandishi waliokuwa kwenye gari ya @millardayo akiwemo @BecaTZA waliniuliza whats next nikawaambia kama mnaenda nendeni mimi nabaki ila nawaomba mkamuhoji Kamanda Murilo kama ataweza kutusaidia kwa chochote . Niliendelea kubaki pale Mpaka akatokea Jamaa mmoja wa kuitwa @Aboucontrolla akachukua Bolt toka Oysterbay akanipeleka mpaka Home.
Vituo vyote nilivopita nilikuwa nikipata majibu mabovu tu naondoka ila hapa Oysterbay niliamua kupiga mpaka hizi picha.
Then leo naona Sativa anasema ametolewa Oysterbay saa mbili asubuhi pale.
Anyway nashindwa kuiweka hii Vizuri lakini nawaomba msiwe watu wa kupuuzia Hisia zenu hasa kipindi cha matatizo.🙏🙏🙏
#Video Edger Mwakalebela maarufu kama Sativa ambae anadaiwa kutekwa Dar es Salaam siku chache zilizopita amesema baada ya kutekwa alipelekwa kituo cha OysterBay.
Sativa ameyasema hayo wakati akiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe alipokuwa akipatiwa matibabu kabla ya kupelekwa hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi huku Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Martin Lohay akithibitisha kumpokea akiwa na majeraha.
#Video Edger Mwakalebela maarufu kama Sativa ambae anadaiwa kutekwa Dar es Salaam siku chache zilizopita amesema baada ya kutekwa alipelekwa kituo cha OysterBay.
Sativa ameyasema hayo wakati akiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe alipokuwa akipatiwa matibabu kabla ya kupelekwa hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi huku Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Martin Lohay akithibitisha kumpokea akiwa na majeraha.
Hawa wanaotukanwa kila siku kwasababu wanaPush Hashtag zisizo rafiki kwa Watanzania wengi wanaona ni sawa kwasababu ndio tunaocheka nao, tunaoMeet, tunakula na kunywa nao, tuko kwenye biashara zao.
Na wanajua kabisa watatukanwa na watavumilia kutukanwa na siku wakiona inatosha wataacha na watarudi kwetu wakisema “Nisameheni, yale mambo siendelei nayo tena, najua niliwakera ila nimeacha”. Na sisi kama kawaida tutawapokea vizuri tukisema“Angalau umejitambua, hayo ndio maneno, safi umefanya jambo zuri” na maneno mengine mengi. Pasipo kutambua waliyoyafanya tayari yalishasababisha damage/madhara mengi.
Ninachojaribu kusema chochote kibaya kwa sasa kinapaswa kukataliwa sio kwa maneno tuu bali hadi vitendo vihusike, kama utakataa hashtag kwa maneno ila mtu huyohuyo ni mshirika wako kwenye mambo mengine ina maana ataona ni sahihi yeye kuendelea kufanya yale yasiyo sahihi. (Mfano, ukikemea uuaji alafu marafiki zako ni wauaji ina maana na wewe unachangia wauaji wale wawe comfortable kufanya yale mauaji kwasababu hakuna repercussions, (wanaona hutowafanya chochote mwisho wa siku).
Tunapokataa hashtag zao alafu haohao ndio tunawaita marafiki, wapenzi, washkaji, dada/kaka, shangazi, Mwana, shoga yangu, Shemeji, ni kama tunawapa urahisi wa wao kufanya yale wanayoyafanya.
Tukikataa Hashtag tukatae na wanaozisambaza, na hata siku wakiona wameshajikusanyia mitonyo ya kutosha hivyo wanataka kuacha na kujirudi kundini pia muendelee kuwakataa, itakuwa ni funzo kwao na funzo kwa wale wanaofikiria kufanya yale yanayoumiza Wananchi.
Kama tutapuuzia na kuona ni ujinga au hatuwezi basi pia tusilalamikie habari za Hashtag Kandamizi. Maana malalamiko ya bure bila vitendo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Mabadiliko huanza na wewe, Kesho Bora umeibeba wewe.
Asanteni kwa Muitikio natoa Update ya Michango
Vodacom (M-Pesa) 3,690,000
Lipa Namba (Voda) 1,300,000
Airtel Money 993,000
Jumla = 5,743,000
Malipo Bill ya Hospitali: 250000
Asanteni kwa Moyo wenu wa utoaji 🙏