Leo umetimia mwaka mmoja tangu mauaji yaliyofanywa kwa makusudi na vyombo vya dola vya Tanzania dhidi ya Watanzania wasio na hatia.
Mauaji ya October 2025 yalikua yanaweza kuepukika na uchaguzi ukafanyika kwa amani na usalama.
Kwasababu ya kiburi na uchu wa madaraka watawala waliamua kupuuza wito wa mda mrefu wa viongozi wa dini, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na hata watu maarufu ya kutaka mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki.
Mpaka sasa mwaka mmoja baadae Nchi iko kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa, watu wanaendelea kutekwa, kuuawawa na kupotezwa.
Kila anaetoa sauti ya kukemea uovu na kutaka maridhiano na uwajibikaji wa kweli anakabiliwa na kifo au mashitaka ya uongo.
Inaonekana hawa watawala wameshindwa kujifunza kwa yale mabaya yaliyotokea, Inaonekana wanafurahia kuendeleza utawala wa mkono wa chuma, udikteta na ubabe, mauaji, utekaji na kunyamazisha badala ya kushawishi na kutatua matatizo.
Kwa kutumia njia hizi mbele ni giza tupu, hakuna sehemu ambayo utawala wa kibabe Umefanikiwa kunyamazisha watu wote, Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 70, hakuna siku watu wote hawa watanyamazishwa kwa uongo na kikundi kidogo cha watu kwa kutumia ubabe.
Njia pekee ya kutatua mkwamo huu ni.
1. Kumuachia Mwenyekiti Lissu na kufuta kesi za uongo dhidi ya wanachama wetu wote.
2. Kuachia mateka wote na kusitisha utekaji na mauaji ya kiholela.
3. Kuruhusu msuluhishi huru (mediator) kuleta watu pamoja na kuzungumza kwa ukweli na uwazi.
4.Uwajibikaji bila upendeleo kwa wahusika wa mauaji, kulipa fidia familia za wahanga, kutibu majeruhi wote na kuwapa fidia.
5. Kuruhusu Uchunguzi huru na kuomba radhi mbele ya Watanzania kwa makosa makubwa yaliyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wake.
6. Kuandika katiba mpya ya Nchi na sheria za uchaguzi ambazo zitarudisha umoja na haki kwa kila mtu.
7. Kutamka kwa uwazi kwamba makosa kama yale hayatajirudia tena kwenye Nchi yetu.
8. Kuhakikisha familia zinapata miili ya wapendwa wao na kufanya maziko ya heshima, kiafrika na kidini.
Kuendelea kutumia ubabe ni kuchochea chuki, uhasama na visasi kwa siku zinajazoโฆ
Watawala badala ya kutumia chawa na ubabe kujaribu kuhujumu Chadema na uongozi wa Chadema, Tumia busara kufanya jambo sahihi la kuponya Nchi hii.
Tunajua mipango yenu dhidi yetu, lakini haki haijawahi kushindwa.
Endeleeni kupumzika kwa amani wote mliouwawa kikatili na kibabe, poleni majeruhi na wahanga wote.
Haki inaweza kuchelewa Lakini haki itapatikana tu.
โUtakula nini?โ
Hivi hamna(ga) maswali mengine?
Niulize mambo ya maana mfano:-
1. โNikikupa donati utakula?โ
2. โLeo nikupe kwa mtindo gani?โ
Na mengineyo!!
Kenge kabisa ๐ฎ๐ฎ๐
Mnaanza kupata akili kumbe?Malengo yao sio malengo ya kuanzishwa kwa chadema kama chama cha siasa..mkatuona hatuwapendi..hivi tofauti na vurugu tangu waruhusiwe kuingia cdm imepata kitu gani mkuu?
@Excess300 Ukimsikiza utaamini kuwa kuwaachia uwaharakati Wanawake ambao by nature wako too emotional tulikosea Sana Maria na mange hawana busara ata ndogo
Hivi brother, hujiulizi kwanini wanachadema wenyewe rasmi hawapati khadhia hizo?
Huoni kama hao kina Sativa, Twaha na Hilda ni class tofauti kidogo na kina Mahinyila, Brenda na kina Mnyika n.k.
Hao waasi, wahaini na magaidi mnaowaita wanaharakati ni maadui wa taifa na mawakala wakazi wa mabeberu so chochote kinachowakuta ni FAIR PLAY sababu wanafanya shughuli za KIJASUSI.
Kutaka kuweka tozo nyingine ya barabara ni wizi wa wazi wazi. Tayari Watanzania wanalipa kodi ya barabara kila wanaponunua mafuta. Huyo aitwaye Waziri wa Ujenzi au jina lolote lile la Wizara hiyo ajue hilo. Kwa wastani Mtu Mwenye gari ya uwezo wa CC 2500 kwa mwaka analipa si chini ya shilingi milioni mbili hadi tatu za Kodi ya kutumia Barbara. Shida hapa si malipo ya fedha bali matumizi yake kwani falsafa ya waliotwaa madaraka kwa kumwaga damu ya maelfu ya Watanzania ni "kula Kwa urefu wa kba zao". Sasa hapo kutakuwepo fedha za kujenga barabara?
Tangu zamani, tozo ipo. Inaitwa Road and Fuel Toll - Tsh 523 kwa kila lita ya mafuta tunayonunua.
Kila ukijaza mafuta, tayari umeshalipia barabara
Sasa mnatuambia "tunaaanzisha" tozo za barabara na madaraja. Mnaanzisha kitu ambacho kipo? Au mnaongeza mzigo juu ya uliopo?
Sema Nabii Lema ana Mchukia sana Mh John Heche sana inaonekan tatzo Heche hayupo tayari katika biashara ya udalali na ndo maan kanamchukia, unga doti vzr hata kwenye msiba wa dereva wake hakwenda au hata kumpa pole
Chadema inapaswa kuendesha shughuli zake za kisiasa bila kutegemea au kuingiliwa na watu wanaojiita wanaharakati vivyo hivyo, wanaharakati wanapaswa kufanya harakati zao bila kujificha nyuma ya jina la Chadema au kugeuza chama kuwa sehemu ya kutekeleza ajenda zao binafsi la sivyo mtaendelea na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama na migogoro ya Chadema na hao wanaharakati uchwara.
Ndo maana wanawake wanaishi mda mrefu, Fellaini hata kumzika tu baba yake aligoma katakata ila yeye na mama ubaya wakawa wa kwanza kumshauri cottonlu aje bongo aratibu phase 2 eti jumuiya ya kimataifa itaingilia kati yani chair yupo ndani ww uogopwe kweli wajinga ndo waliwao