WANASAYANSI WA HONG KONG WANAUPIGA MWINGI.
Wanasayansi nchini Hong Kong wamegundua aina mpya ya chuma kinachoitwa ULTRA STAINLESS STEEL, ugunduzi ambao unaweza kubadilisha kabisa mustakabali wa nishati safi kwa binadamu Duniani.
UNAJUA KWANINI WANAHARAKATI WA MAZINGIRA WANAOMBEA HII IFANIKIWE?
NI HIVI,
Ultra stainless steel ina uwezo wa kuhimili kutu karibu sawa kabisa na madini ya Titanium, lakini chuma hii ni gharama nafuu mara 40 zaidi ya Titanium endapo itaingia sokoni.
Kwa maana hiyo ultra stainless steel inaweza kutumika kutengeneza vifaa vinavyoitwa HYDROGEN ELECTROLYZERS.
HYDROGEN ELECTROLYZERS ni nini?
Hivi ni vifaa au mitambo inayotumika kutenganisha maji (H₂O) kuwa gesi mbili tofauti:
Hidrojeni na Oksijeni.
Kwa kifupi, electrolyzer hufanya kazi kama “mashine ya kuvunja maji kuwa gesi” kwa kutumia nguvu ya umeme (electrolysis)
Hidrojeni inayopatikana katika mtambo huu inaweza kutumika kama mafuta ya magari ya hydrogen (kama uliwahi sikia), Pia kuzalisha umeme ili kuendesha viwanda, pia inaweza kutumika kuhifadhi nishati safi.
Pia kumbuka ndani ya Process hii unapata gesi ya Oksijeni kama zao la pembeni, Japo sijataka hasa kuongelea hiyo, nataka kubase na Hydrogen zaidi.
SASA, Kwa nini hydrogen ni muhimu?
Hydrogen inachukuliwa kama nishati safi kwa sababu inapochomwa au kutumika kuzalisha umeme, haitoi moshi wa carbon dioxide (CO₂), huchafua mazingira kidogo sana, hivyo inaweza kusaidia kupunguza mabadiliko ya tabianchi.
SASA, Ugunduzi wa hii ultra stainless steel utasaidia nini katika uzalishaji wa Hydrogen?
Wanasayansi Kwa Muda Mrefu walihitaji kuzalisha Hydrogen kutoka katika Maji mengi, Yaani Maji ya Bahari, Lakini ilishindikana kwakuwa Vyuma vililiwa na kutu kwa haraka, Maji ya Bahari yalikua na Chumvi nyingi, Chumvi husababisha Metali kupata kutu kwa haraka.
Ndiyo maana ugunduzi wa ultra stainless steel ni muhimu sana,
Kama ugunduzi huu utafanikiwa basi Mfumo wa kuzalisha Hydrogen unaweza kufanya kazi hata kwa kutumia maji ya bahari, jambo linalomaanisha kuwa bahari kubwa duniani zinaweza kutumika kuzalisha nishati.
Tatizo kubwa lilikuwa kwamba metali nyingi huharibika kwa kutu kwa haraka sana katika mazingira hayo yenye chumvi nyingi. Hapo ndipo ultra stainless steel inapokuwa suluhisho muhimu.
Chanzo hiki cha nishati safi ambacho hapo awali kilikuwa ghali mno kutokana na matumizi ya vipuri vya titanium, sasa kunaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kujengwa kwa gharama ndogo kwa kutumia aina hii mpya ya chuma.
Ni Wakati huo huo viongozi wa Nchi ya Malawi wanahangaikia kubadilisha Uraia wa Mchezaji wa nchi nyingine.