#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 219
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross Examination Shahidi wa Jamhuri Coplo Amani.
Coplo Amani.: mimi sijalisema tu kama wewe umelisema basi ndio umesema.
Mhe. Lissu: Ni kweli kwamba P3 alikwambia kuwa ni mwanachama wa CHADEMA, kweli au si kweli
Coplo Amani : sio kweli
Mhe. Lissu: Wewe ndio uliandika maelezo yake kielelezo D12
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: Sasa ngoja nikusomee… “mimi pia ni mfuasi na mwanachama wa CHADEMA” kweli si kweli.
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama kwenye maelezo yako uliyasema hayo
Coplo Amani : sikuyasema
Mhe. Lissu: Alikuonyesha kadi yake cha chama
Coplo Amani : sikutaka anionyeshe
Mhe. Lissu: alikwambia wafuasi wa chadema wana alama gani?
Coplo Amani : sikumuuliza mm
Mhe. Lissu: ndo maana nasema huyu ni askari wa kitengo cha intelijensi halafu mnasema ni shahidi.
Mhe. Lissu: Turudi kwa Inspekta Jorum, ni kweli polisi inapopokea watu waliofanya uhalifu , Polisi wanafungua investigation register?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: waelezze majaji kama kwenye maelezo yako polisi walifungua investigation register
Shahidi: sijui
Mhe. Lissu: Waeleze majaji baada ya maafa yote hayo ya October 29 kama mmemchukulia hatua yoyote huyu baada ya kusema atapiga watu mawe?
Coplo Amani: Simfahamu chochote kuhusu swali lako
Mhe. Lissu: inaingia akilini hii
Coplo Amani : Mimi sifahamu chochote kwa kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama unajua mashahidi wote wa kificho walisema waliona hiyo video yangu maarufu tarehe 4 april
Coplo Amani : Mimi sio mpelelezi wa mafile yote
Mhe. Lissu: Na unahabari wote waliokuja hapa ni boda boda na machinga hakuna afisa wa serikali au n.k
Coplo Amani : sina habari
Mhe. Lissu: Ulipomuachilia P3 kwa dhamana ulichukua hatua gani kuhakikisha aendelei na kupiga watu mawe na uasi?
Coplo Amani : sikupewa hilo jukumu
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji mimi sina maswali ya ziada.
Serikali: Kwa leo tulikua na shahidi huyu tu mmoja, tunaomba ahirisho kwasababu hali ya hewa ya Dar es salaam imebadilika na zimebaki dakika 20.
Kwasababu za kiusalama tunaomba ahirisho hadi siku ya Jumatatu ili tuje kuendelea kusikiliza juu ya notice tuliyoileta
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kwa dakika 20 kwangu si haba, mimi ninaomba hizi dakika 20 kwasababu nilishasema nina mapingamizi, naomba niongee juu ya hayo leo ili tusiathiri muda wa mashahidi wengine Jumatatu.
Naomba nipate hizi dakika 20 kwasababu mimi niliyepo Gerezani ndiye ninayepata shida, kwahiyo naomba tutumie hizi dakika jambo lifanyike.
Wakili wa Serikali: Waheshimiwa sisi tunaomba ahirisho lakin vilevile kama mnavyojua dini zote mbili tupo kwenye mfungo kwahiyo tunaomba ahirisho.
Lakini vilevile PO yake haijasajiliwa bado kwahiyo kama ataweza kuisajili na kuisikiliza basi aisajili na sisi tupewe nafasi ya kuiona ili tu-submit
Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji sikutarajia kwamba hili litakua na kubishana namna hii, nililetewa hii notice jana na nikatoa notice ya mdomo kwamba naipinga tena immediately nilipopatiwa tu notice hii.
Naijua sheria, sasa wanaposema tuahirishe ili niendelee kukaa gerezani ni sawa tukutane Jumatatu ili tuzungumzie PO yangu niliyoileta jana.
Na jana nilisema kabisa PO ni ya kisheria na itaenda na kifungu icho icho cha 308(1) cha CPA, mimi nakaa gerezani kwasababu ya michezo hii mnayoleta mawakili wa serikali kila siku.
Jaji Ndunguru anasema shauri litaendelea siku ya Jumatatu, tunatarajia serikali mlete mashahidi, tutaanza na hoja ya notice, tukimaliza tutaendelea na mashahidi wengine.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 218
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross examination Shahidi wa Jamhuri Coplo Amani.
Mhe. Lissu: Angalia D14 tuambie wapi alisema alimuona Tundu Lissu akihamasisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi wa 2025?
Coplo Amani : Hayo maneno kufanya vurugu hayapo kwenye kielelezo
Mhe. Lissu: April 17, 2025 kwenye ushahidi wako wa hii siku unasema ulikuwa kituo cha Polisi Ilomba na ukapewa maelekezo na inspekta Jorum kuandika maelezo ya mtuhumiwa kama shahidi kuhusiana na alichoeleza juu ya Mwenyekiti wake Tundu Lissu kuhusu kauli yake na akahamasika na akashawishi wenzake wafanye vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu 2025, eleza kama maelezo hayo yapo
Coplo Amani : hayo maelezo hayapo
Mhe. Lissu: Coplo Amani shahidi haya yote ambayo nimekuuliza kama yapo au hayapo ma umesema hayapo katika maelezo yako, swali langu ni uliyasema hapa mahakamani kwasababu ni mambo muhimu kwa mahakama kuyasikia, kweli au si kweli.
Coplo Amani : Waheshimiwa majaji naomba nitoe ufafanuzi.
Mhe. Lissu: Hapana naomba ujibu swali langu
Coplo Amani: nawaomba majaji
Mhe. Lissu: hapana
Coplo Amani : ni kweli
Mhe. Lissu: Umewaeleza waheshimiwa majaji kwanini hayo mambo muhumu hayapo katika maelezo yako??
Coplo Amani : bado nina muda
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi ajibu swali langu
Coplo Amani : sijayasema na sijayaeleza kwasababu ninazozijua Mimi.
Mhe. Lissu: Nataka uangalie icho kielelezo D14 ni nataka uangalie halafu uniambie kama nakosea umeandika baada ya kupata maelezo ya kazi ya Jorum nilianza ufuatiliaji Isyesye mtaa wa Mwantengule, kwa maneno hayo nitakuwa sahihi nikisema kwamba ulikwenda Mwantengule ukiwa tayari unamjua P3
Coplo Amani: nilikua simfahamu
Mhe. Lissu: Kama ulikua humfahamu uliendaje moja kwa moja ukamkamata
Coplo Amani : Nilishasema nilionyeshwa na askari wa intelijensi
Mhe. Lissu: hayapo kwenye maelezo yako and it is too bad.
Mhe, Lissu: P3 ni dereva wa boda boda sio
Coplo Amani : ndio
Mhe. Lissu: Na umesema askari wa intelijensi huwa wanajichanganya hata kwa boda boda
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: sasa waambie waheshimiwa majaji kama huyu P3 sio askari wa kweli wa intelijensia
Coplo Amani : si kweli
Mhe. Lissu: umesema P3 alipanga kupiga watu mawe, kuasi nchi halafu umesema Jorum alikwambia umuachie kwa dhamana, inaingia akilini??
Coplo Amani : inaingia akilini
Mhe. Lissu: mtu anayepanga uasi na kupiga watu mawe mnampa dhamana?! Kwanin tushangae yaliyotokea October 2025!
Coplo Amani : mimi sijui bwana muulize Jorum
Mhe. Lissu: Jorum hayupo kwenye kizimba
Mhe. Lissu: kwahiyo nyinyi Polisi ndo mlipanga mambo ya October 29
Coplo Amani : Mimi sina majibu ya hilo.
Mhe. Lissu: Eleza kama umeleta pikipiki uliyomkamata nayo
Coplo Amani : sijaonyesha
Mhe. Lissu: usajili wa Bodaboda
Coplo Amani : Hakuna
Mhe. Lissu:Kadi ya bodaboda
Coplo Amani : hakuna
Mhe. Lissu: Na huyu jamaa tunamtambua kama P3, hatujui jina lake, amejificha kwenye kibox hatujamuona tutajuaje kama ni boda boda?
Coplo Amani : hayo mambo yanahusika vipi kwenye kesi hii
Mhe. Lissu: yanahusika
Mhe. Lissu: Huyu P3 ulivyomfikisha Ilomba ulimuweka mahabusu, kweli au si kweli
Coplo Amani : Si kweli
Mhe. Lissu: Naomba nimsomee shahidi kielelezo D12 jinsi P3 alivyofikishwa kituoni……”tulivyofika kituoni aliniweka mahabusu”
Sasa swali langu kati ya ushahidi wako ww na ushahidi wa P3 Mahakama ichukue upi kuwa ni ushahidi wa kweli?
Coplo Amani : hilo ni jukumu la mahakama.
Mhe. Lissu: naomba ujibu swali langu
Coplo Amani : hilo ni jibu la mahakama
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji naomba shahidi ajibu swali langu
Katuga: Waheshimiwa shahidi ameshajibu sasa kama halimpendezi basi hilo ndio jibu
Mahakama: endelea na Cross
Mhe, Lissu: Kwenye ushahidi wako kizimbani umewaambia majaji kwamba P3 alikua anahamasisha watu kupiga mawe?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: Kwanini hujalisema wakati upo kizimbani
Part 219 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 216
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa Maswali ya Dodoso.
Anasimama Mheshimiwa Lissu kwa ajili ya kumfanyia Cross Examination Shahidi ambae anaitwa Coplo Amani.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa kwa kuanzia naomba nipatiwe kielelezo D12, waheshimiwa majaji haya ni maelezo ya P3.
Mhe. Lissu : Sasa shahidi naomba uwaeleze majaji kama uliandika maelezo polisi
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama unaweza kuyatambua ukionyeshwa
Coplo Amani : nikionyeshwa nitaweza kuyatambua
Mhe. Lissu: naomba shahidi aonyeshwe maelezo yake aliyoandika polisi.
Coplo Amani : haya ndio maelezo yangu
Mhe. Lissu: asante sana, sasa shahidi hayo maelezo yako naomba uwaeleze majaji kama uliyaandika mwenyewe au uliandikiwa na askari mwingine?
Coplo Amani : haya maelezo niliandikiwa na askari mwingine
Mhe. Lissu: mtaje jina tafadhali
Coplo Amani : Anaitwa H9207 detective coplo Robert
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako hayo waeleze majaji kama ni utaratibu mtu anayeandika maelezo ya shahidi hawezi akawa ndio mtu huyohuyo kama shahidi?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji pamoja na majibu mazuri ya shahidi huyu nataka ku-impeach credibility yake, nitamsomea maelezo yake, nitamuonyesha maeneo nitakayotaka kumuuliza maswali halafu nitamtaka ayawasilishe kama kilelezo.
Mhe. Lissu anamsomea maelezo yake
Mhe. Lissu : Haya ndio maelezo yako kama nilivyoyasoma?
Coplo Amani : Waheshimiwa majaji mshtakiwa kuna maeneo amekosea naomba nimrekebishe, sio kata ya Isuesue ni Isyesye 😁
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji kwakua na nyie mnarekodi hii mimi nimeona imeandikwa isuesue waheshimiwa…
Kwenye maneno “ni dereva wa bodaboda isuesue Mwintengule”… kwenye original Isyesye… kwahiyo tutaenda na ya kwako.
Kuna eneo lingine ambalo lina shida?
Coplo Amani : hapana.
Mhe. Lissu : Sasa kuna maeneo nataka kukuhoji kwa ajili ya kukukanusha kama ifuatavyo;
1. Kwamba unafanya kazi chini ya OCCID Mbeya mjini
2. Kwamba wewe ni msaidizi wa upelelezi ndani ya Mbeya mjini
3. Umeelezea Kituo cha Polisi cha Ilomba kwamba ni kituo kidogo kilichopo chini ya kituo cha Kati Mbeya umesema ni kama out post.
4. Umeeleza kwamba kaimu OCCID Inspekta Jorum alipokupa maelekezo ya kwenda kumkamata P3 alikupa namba ya simu ya askari wa kitengo cha intelijensia kwa ajili ya kwenda kumkamata P3
5. Kwamba hawa askari huwa wanajichanganya na raia kama dereva boda boda n.k
6. Baada ya kupewa namba ya simu ukawasiliama nae na mkakutana Isyesye.
7. Kwamba kulikua na watu wengi na mlipita na akakuonyesha mtuhumiwa kwenye kituo cha boda boda.
8. Taarifa mlizopewa na Jorum ni mtuhumiwa ndiye anayehamasisha wenzake kufanya vurugu uchaguzi wa 2025
9. Baada ya kuonyeshwa huyo mtuhumiwa ulimfata na kumtoa pembeni ya kijiwe na kisha ulijitambulisha kwake kwa jina na kumueleza tuhuma zake.
10. Ulimwambia baada ya kumtoa pembeni kwamba anahitajika Kituo cha Polisi Ilomba na yeye alikubali kwenda.
11. Ni ushahidi wako maelezo aliyoandika mtuhumiwa ni uchochezi, kusababisha vurugu na kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025.
12. Shitaka uliloandika lilikua ni kukiuka masharti ya kifungu cha 390 cha Penal code
13. Wakati ukimhoji alikwambia kwamba aliona taarifa kwenye YouTube akamuona Lissu akiwa anahamisisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi 2025.
14. Baada ya kuandika maelezo yake ulimjulisha inspeka Jorum akakuelekea kumuachia kwa dhamana na we anaripoti kila baada ya siku tatu
15. Ni ushahidi unaohusu tareh 17 april 2025 kwamba siku hiyo wakati ukiwa Ilomba Kituo cha Polisi ulielekezwa na inspekta Horum kuandika maelezo ya mtuhumiwa kama shahidi kuhusiana maelezo ya Mwenyekiti wake Tundu Lissu na yeye kuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana wenzake kufanya vurugu.
16. Baada ya kurekodi malezo hayo na ulimjulisha Inspekta Jorum na ukamkabidhi malezo hayo.
Part 217 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 214
Leo Mhe. Lissu ameingia Mahakamani akiwa amepiga Jeans na T-Shirt fulani hivi nyeusi yenye neno moja lililoandikwa kwa herufi kubwa "DUDA"
Kaka David Jumbe anasema DUDA ni neno la Kinyaturu ambalo maana yake ni mtoto ambae anapendwa sana.
Majaji wameingia,
Naona wanaandika kidogo pale juu.
Wakili wa Serikali anasimama, anasema upande wa Serikali wapo Kama walivokuwa asubuhi.
Wakili wa serikali: Shahidi anayefata sio shahidi wa kulindwa, anaitwa Coplo Amani.
Shahidi anaingia Mahakamani.
Jaji anamuuliza unaitwa nani?
Naitwa G9304 detective Coplo Amani
Una miaka mingapi: Nina miaka 35
Dini yako: Shahidi: mkristo
Kazi yako: Shahidi: mimi ni askari polisi.
Wakili wa Serikali : Toka lini?
Coplo Amani : Nimekua askari polisi tangu 2012
Wakili: unaifanyia wapi hiyo kazi?
Coplo Amani : Kazi yangu naifanyia mkoa wa Mbeya wilaya wa Mbeya mjini, kituo cha polisi cha kati Mbeya.
Wakili: Kituo gani?
Coplo Amani : Kituo cha Kati Mbeya nipo tangu 2012
Wakili: Una elimu gani ya Polisi?
Coplo Amani : Elimu yangu niliipata 2011-2012 ndani ya chuo cha polisi Moshi
Wakili: Ulivyohitimu ikawaje?
Coplo Amani: Baada ya kuhitimu mafunzo nilipangiwa Kituo cha Polisi Kati Mbeya Mkoa wa Mbeya.
Wakili: Kitengo gani upo?
Coplo Amani : Kituo cha Polisi Kati Mbeya nipo kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai
Wakili: Unafanya kazi chini ya nani hapo?
Coplo Amani : Nikiwa chini ya ofisi ya mpelelezi wa wilaya ya Mbeya kwa kifupi ni OCCID
Wakili: Kingine?
Coplo Amani: Katika ofisi hiyo nipo kama msaidizi wa shughuli zote za upelelezi ndani ya wilaya ya Mbeya mjini.
Wakili: Majukumu yako ni yapi?
Coplo Amani: Majukumu yangu ni kufanya doria, kupeleleza kesi zote za jinai, kukamata watuhumiwa wote wa makosa ya jinai na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa jinai
Wakili: Unakumbuka nini tarehe 04 April?
Coplo Amani : April 4, 2025 nakumbuka nilikua Kituo cha Polisi Ilomba ambacho kipo Wilaya ya Mbeya Mjini, Mkoa wa Mbaya, hiki ni kituo kidogo cha polisi kinajulikana kama outpost
Wakili: Unajua nini kuhusu hicho kituo cha Polisi?
Coplo Amani : Kituo cha Polisi Ilomba kipo chini ya kituo cha polisi kati Mbeya.
Wakili: Nini kikaendelea?
Coplo Amani: Nilipewa maelekezo na Inspekta Joram, ambaye ni kaimu wa upelele Wilaya ya Mbeya mjini.
Wakili: Akakwambia nini?
Coplo Amani : Alinipa maelekezo ya kwenda Isyesye mtaa wa Mwamtengule ambapo alinieleza kwamba kuna watu wanapanga njama za kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Wakili: kingine?
Coplo Amani: Lakini pia alinipa namba ya simu kwamba niwasiliane na askari mwenzangu, ambaye yupo kitengo cha intelijensia ili aende akanionyeshe watu hao wanaojipanga kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili: Kazi yako inahusiana na nini?
Coplo Amani: Askari ambaye yupo intelijensi ni askari wanaofanya kazi ya kujichanganya na wananchi ili wapate taarifa mbalimbali za uhalifu.
Wakili: mnafanyaje kazi?
Coplo Amani: Askari wa intelijensia huwa wanajichanganya katika shughuli mbalimbali za wananchi, wengine ni bodaboda n.k ili kupata taarifa za makosa ya jinai.
Wakili: nini kilifuata?
Coplo Amani : Baada ya maelekezo hayo niliwasiliana na huyo askari tukakutana Isyesye mtaa wa Mwantengule
Wakili: Mkafanya nini?
Coplo Amani : Tulivyokutana akaniongoza na kunionyesha mtuhumiwa ambaye nilipaswa kumkamata.
Wakili: Kulikuwaje?
Coplo Amani : Pale kulikua na watu wengi tukapita kwa siri na akanionyesha mtuhumiwa katika kijiwe cha bodaboda akiwa na wenzake.
Wakili: Ukafanya nini?
Coplo Amani : Huyo mtu niliyetakiwa kumkamata ndiye aliyekuwa anahamasisha wenzake kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.
Part 215 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 213
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P9
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji hilo pingamizi la Wakili la Serikali halina maana yoyote, kwasababu shahidi mwenyewe amesema kwamba summons alipelekewa summons na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti ni ofisa wa serikali, lakini vilevile Mahakama haitaweza kujua kama huyu shahidi ni mkweli au ni muongo kwahiyo swali langu ni halali na ninaomba pingamizi lao litupitiliwe mbali, lakini huyo Mwenyekiti sio mtu ambaye amelindwa na sheria.
Katuga: Sisi tunaomba swali hilo shahidi asiulizwa kwasababu swali hilo litapelekea utambuzi wa shahidi huyu na kama tunavyojua humu ndani kuna wafuasi wake, researchers wake wanaweza wakaenda kumtafuta ili kumtambua shahidi huyu.
Mhe. Lissu: naomba ondoa hiyo kauli yako mimi sijazungumzia kuhusu wafuasi wangu humu.
Katuga: Naondoa hiyo ilikua ni by the way lakini msimamo wetu ni kwamba swali hilo shahidi asiulizwe
Mahakama: tunadhani uendelee na x-examination bila hilo jina.
Mhe.Lissu: Lakin waheshimiwa majaji mnaweza kuona namna cross examination yangu inavyokua limited lakini naomba niendelee.
Mhe. Lissu: shahidi umekujaje hapa
Shahidi wa kificho P9: nimependa bus
Mhe. Lissu: nani amekulipia nauli
Shahidi wa kificho P9 : nimejilipia mwenyewe
Mhe. Lissu: Umefikia wapi
Shahidi wa kificho P9 : Kwa ndugu yangu.
Mhe. Lissu: Waambie waheshimiwa majaji kama kuna kiongozi au mfuasi anajua kama unakuja kutoa ushahidi
Shahidi wa kificho P9: Ndio wapo baadhi
Mhe. Lissu: waliwahi kukutishia
Shahidi wa kificho P9 : ndio
Mhe. Lissu: unajua hilo ni kosa
Shahidi wa kificho P9 : hilo ni kosa la jinai
Mhe. Lissu: umewataja,
Shahidi wa kificho P9 : siwezi kuwataja kwa usalama
Mhe.Lissu: waeleze majaji kama ulitoa taarifa kituo cha polis
Shahidi wa kificho P9 : ndio
Mhe. Lissu: Kituo cha polisi kipi?
Shahidi wa kificho P9: Sasa nikitoa taarifa hiyo hapa si itakua navunja usalama?
Mhe. Lissu: Hebu jibu swali bwana tusisumbuane
Mahakama: Shahidi hebu jibu hilo swali
Shahidi wa kificho P9: Nilitoa kituo cha polisi Ilomba
Mhe. Lissu: Ulipewa RB
Shahidi wa kificho P9: ndio
Mhe. Lissu: umeitoa hapa mahakamani?
Shahidi wa kificho P9 : hapana
Mhe. Lissu: Polisi walichukua hatua gani?
Shahidi wa kificho P9: Walisema watafatilia
Mhe. Lissu: waambie waheshimiwa majaji kama kuna mtu yoyote amekamatwa
Shahidi wa kificho P9 : hapana
Mhe. Lissu: Waambie kama kuna mtu yoyote amepelekwa mahakamani:
Shahidi wa kificho P9 : hakuna
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Wakili wa Serikali: Leo tunashahidi mmoja, tunaomba break kidogo halafu tuje na shahidi mmoja aliyebaki, kwasababu jana hatukupumzika.
Mahakama: Mshitakiwa unasemaje
Mhe. Lissu: Tukienda kwa utaratibu huu tutachukua mida mrefu sana, Mahakama ilisema upande wa serikali ulete mashahidi wasiopungua watatu, kwanin hawajaleta hao mashahidi wengine.
Upande wa mashtaka wanatakiwa wawe na mshahidi wengine kama walivyotakiwa na Mahakama.
Katuga: Jana tulisema tutakuja na shahidi mmoja then twende kuargue application yetu, hatujaweza kuja na mashahidi wengi ili tupate muda wa kutosha kwasababu yeye alisema ana-objection.
Mahakama: Nadhani twende break fupi kwanza ili tukirudi tuendelee na huyo shahidi halafu tukimalizana nae mambo mengine yatafata.
Part 2014 itaendelea tukirudi.
Naomba repost yako.