Kauli za viongozi Zanzibar pamoja na michango ya Wawakilishi yazua gumzo juu ya hadhi na haki ya Tanganyika katika muungano.
Kauli aliyoitoa Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar, Hassan Hafidh Ameir, juu ya kufanya mapinduzi katika ajira—kufuatia malalamiko ya ajira kuchukuliwa na wageni kutoka bara.
Pamoja na kauli iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Saada Mkuya kuwa Zanzibar haina uwezo wa kutibu watu milioni 60–akilalamikia 'wageni' wanaotumia afua zilizowekwa kwa ajili ya Wazanzibari kupata matibabu, zimeibua gumzo mtandaoni hasa juu ya nafasi na hadhi ya Tanganyika katika muungano.
Viongozi hao walikuwa wakijibu maswali ya Wawakilishi wakati wa uwasilishaji wa bajeti katika baraza linaloendelea Zanzibar.