KWAKUWA NI HALALI KWA WAZANZIBARI KULINDA HAKI ZA WAZANZIBARI HAIWEZI KUWA HARAMU KWA WATANGANYIKA KULINDA HAKI ZA WATANGANYIKA.
Kwa yanayoendelea kujitokeza katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu kujitanabaisha kwa misingi ya Uzanzibari na kulinda maslahi ya Zanzibar, je, si wakati sasa kwa Watanganyika nao kuzungumza kwa uwazi, kuhoji kwa uhalali na kujadili kwa kina masuala yanayohusu haki, hadhi na maslahi ya Tanganyika?
Je, Watanganyika hawana haki ya kuhoji na kulinda:
1. Bandari zilizopo ndani ya Tanganyika.
2. Misitu na rasilimali za mazingira za Tanganyika.
3. Rasilimali za asili zilizopo katika eneo la Tanganyika.
4. Hadhi, haki na umiliki wa ardhi ya Tanganyika.
5. Nafasi, haki na uwepo wa watu wasio Watanganyika katika idara na taasisi ambazo si za Muungano.
6. Uhalali wa viongozi wasio Watanganyika kuingia au kusaini mikataba inayohusu rasilimali za Tanganyika, hususan pale ambapo baadhi ya masuala hayo tayari yameondolewa katika eneo la Muungano kwa upande wa Zanzibar.
7.Kuhoji mchango wa Zanzibar katika kugharimia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano na Ulipwaji wa Deni la Taifa.
Ikiwa ni halali kwa Wazanzibari kujadili, kuhoji na kulinda maslahi ya Zanzibar kwa misingi ya utambulisho wao wa kisiasa na kikatiba, kwa mantiki hiyo hiyo haipaswi kuwa kosa kwa Watanganyika kuhoji, kujadili na kutetea maslahi ya Tanganyika.
Katika mfumo wowote wa haki, usawa na kuheshimiana ndani ya Muungano, haki ya kulinda maslahi ya Zanzibar haiwezi kutenganishwa na haki ya Watanganyika kulinda maslahi ya Tanganyika.
Haki hizo zinapaswa kutambuliwa kwa usawa, bila upendeleo na bila kuonekana kuwa ni tishio kwa Muungano, bali kama sehemu ya kujenga Muungano wenye misingi ya haki, uwazi na kuheshimiana.
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI ndiyo Msingi bora wa kuliongoza Taifa kutoka katika vitendo vya Ukatili dhidi ya ubinadamu,ukiukwaji wa Haki za Raia na,Mauwaji na Utekaji vilivyofanyika kanla,wakati na Baada ya Tarehe 29 Oktoba 2026.
BAK MWABUKUSI.
Kesi ya uongo ya mgogoro fake wa mali, ni kesi ya Msajili wa vyama..
Marehemu mama Komu alituelezea namna ambavyo Sisty Nyahoza, Msajili msaidizi akiwa na mtu anaitwa Salehe Bohora, walivyomfuata nyumbani kwake na kuomba aweke jina kwenye kesi..
Marehemu Mama Komu alituambia hata malipo ya mawakili yalilipwa na Salehe Bohora na bwana Sisty, kwa mujibu wa mama Komu huyu bwana Salehe alitumwa na Rais.
Mtakumbuka pia kuna mtu alijiita Mwenyekiti wa Chadema Mwanga.. huyu nae alikua analipiwa mpaka mahali pakukaa na ofisi ya msajili, kupitia ofisi hiyo hiyo ya msajili walidai kutotambua uongozi halali wa Chama, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na wajumbe wa kamati kuu ya Chama.
Hii kesi ilifunguliwa siku hiyo hiyo ambayo Mwenyekiti wetu alikamatwa na kupewa kesi ya uhaini.
Kesi hii ilipangwa kwa Jaji mwingine awali lakini katika mazingira tata ikapelekwa kwa jaji Mwanga.
Jaji Mwanga tangu awali alionekna wazi kutofuata sheria, kuendesha Kesi kibabe na kudharau kila hoja iliyotaka upande wetu… alikua na maelekezo ya wazi na alionesha upendeleo uliovuka mipaka..
Kupitia kesi hii shughuli za Chama zilizuiliwa kinyume cha sheria kwa siku 309, Mpaka mahakama ya rufani ilipofuta zuio fake..
Kupitia Hilo zuio watu wetu walipigwa mara nyingi na polisi kila walipojaribu kufanya shughuli za chama.
Tutakumbuka siku ya wanawake duniani namna wanawake wa Bawacha walivyopigwa mpaka kanisani kwasababu ya zuio hili haramu..
Mali za Chama zimeharibika, Mimi pamoja na Katibu mkuu tulifunguliwa kesi ya contempt of the court. Kutokana na Amri hizi hizi.
Jaji Mwanga alipuuza hukumu ya mahakama ya rufani ambayo ilikua inamlazimisha kutokifungia Chama chetu..
Nani atalipia maumivu, usumbufu, matatizo ya makusudi, nani atalipia hasara zisizolipika za kuzuia chama mda wote huu kufanya kazi zake..
Tunafurahia leo, lakini Fikiria damage zote hizi hazikutakiwa kuwepo, zilifanywa kwa makusudi kwa manufaa ya Samia na Ccm.
Bado msajili anatufuata fuata na kutuandikia barua baaada ha maumivu yote haya aliyotusababishia..
Kama ilivyo kesi ya uongo ya kumtesa Mwenyekiti wetu ndivyo zilivyo zote hizi ni kwa manufaa ya Samia wala sio Nchi..
Tuacheni tufanye wajibu wetu wa kisiasa. Hatutapiga magoti wala kununuliwa.
Tukubali "ghasia" zilipangwa, kuratibiwa, kufadhiliwa na kutekelezwa.
Tukubali watu 518 tu ndio waliouwawa, 758 wamepotea na 448 hawajulikani walipo ( 518+758+448=1,724! Namba 8 imependwa sana na Tume).
Jumla watu 1,724 HAWAPO kama matokeo ya hicho kilichopngwa, kuratibiwa, kufadhiliwa na kutekelezwa;
- Mkuu Usalama wa Taifa (DGIS) bado yupo ofisini
- Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) bado yupo ofisini
- Wakuu wa Mikoa na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa yote husika wapo ofisini
- Wakuu wa Wilaya na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zote husika wapo ofisini
Hakuna kuwajibika wala kuwajibishwa, halafu Umma ukubali kuwa hii haikuwa kazi ya dola yenyewe kujiandaa kuua watu wake?
Mwenyekiti wetu amesema mwenyewe kwa maandishi yake na sisi tunajua…
Alishambuliwa kwa risasi nyingi mwaka 2017.
Tangu wakati huo alikua anakwenda kufanya checkups na matibabu mara kwa mara.
Leo ni mwaka mzima yuko gerezani Ukonga kwa kesi ya uongo, hqjakutana na wataalamu wake wala hajafanya checkup inayotakiwa.
Sisi viongozi wenzake haturuhusiwi kwenda kumuona, marafiki zake pia hawaruhusiwi kumuona, kinyume kabisa cha utaratibu wa sheria.
Hapa sijui hawa Magereza wanasema nini!!!!
Umoja wa Mataifa (UN) umefanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa kesi ya Uhaini ya Mwenyekiti Lissu ni ya 'Mchongo' na wametaka ifutwe.
Mwenyekiti wa Ccm na chama chake wanatakiwa kuifuta kesi hii la sivyo wataiingiza Tanzania kwenye mgogoro na Umoja wa Mataifa.
Bado hamuoni aibu kuendelea kumshikilia kwa kesi ya uongo.
You cannot sue or imprison the truth.
Mnahangaika bure, mwachieni bila masharti yoyote kwa sababu hana hatia.
Mnaua na kutesa watu, halafu mnatafuta kichaka cha kujificha.
These schemes will eventually fail you big time.
@smkami Walikwepo kuboost Ccm Sasa mission ilikamilika wanarudi kudai Haki tena, njaa na pesa ni vitu viwili tofauti lolote lile Kwa mwenye njaa pasipo akili atafanya tu ilimradi apate ulaji wa pesa hata kama ni kujidhalilisha kama hao G55 fake
@ajirapsrs Nasikia vijana wengi walishinda mitihani ya kuandika mkawapeleka Kambi ya jeshi Makotopora na kuwafanyia Medical checkup Hadi Naked checkup dhen oral interview ila Cha kushangaza mmetoa majina ya watu ambao hata hawafiki robo ya waliofanyiwa vipimo hivyo, Tafadhali zingatien hilo
Sio kuundwa kwa Tume Huru ya Uchunguzi kama walivyoandika kwenye press yao.
Huku wanaita kabisa Tume ya Rais! Mtu na Tume yake, alafu mnategemea kuna uhuru wa Tume hapa?