MNANIKUMBUSHA ILE MEME AMBAYO MTU ANAENDESHA BAISKELI, ANACHUKUA MTI NA KUINGIZA KWENYE SPOKE MWENYEWE, KISHA ANAANZA KULALAMIKA BAADA YA KUANGUKA.
Tuulizane maswali machache⬇️
Kulikuwa kuna ulazima gani wa Rais kusimama public na kusema UTEKAJI NI DRAMA?
Rais anatoaje kauli za aina hii katika mazingira ambayo kweli watu wametekwa na kupotezwa, tena watu wenyewe ni wakosoaji wake?🤔
Kulikuwa kuna ulazima gani kwa kiongozi mkuu wa nchi kusema kifo cha mtu mmoja tu Mzee Kibao tunapiga makelele?
Kulikuwa kuna ulazima gani kwa polisi kupiga na kuumiza watu hadharani kabisa kwa sababu tu wameenda kusikiliza kesi ya Lissu?
Kulikuwa kuna ulazima gani kwa polisi kukamata watu kinyemela na kukaa nao kimya kwa muda mrefu kisha baadae kutoka na kusema “tunawashikilia” baada ya watu kupiga kelele kwamba wametekwa??
Kulikuwa kuna ulazima gani kwa serikali kumkamata, kumpa kesi, na kumfunga jela kijana mdogo kama Shedrack Chaula kwa kosa la kuchora taswira ya Rais na kuichoma? Kulikuwa kuna ulazima gani wa kumteka na kumpoteza yule kijana?
Kulikuwa na kuna ulazima gani kwa polisi kumharras Deus Soka repeatedly kabla ya kumteka na kumpoteza kabisa? Soka na Chaula walikuwa na threat gani kwa taifa kiasi cha kustahili treatment ya aina ile?
Vipi familia ya Mchungaji Mbarikiwa, kulikuwa na ulazima gani wa kuinyanyasa kiasi kile kwa kukosoa utendaji wa serikali??
Vipi Tundu Lissu, kulikuwa kuna ulazima gani wa kumpa kesi ya uhaini na kuparade ubabe wa hali ya juu dhidi ya wakosoaji?
Askofu Gwajima je, kulikuwa kuna ulazima gani wa kufungia kanisa lake?? Ukosowaji wake ulikuwa unahusiana vipi na waumini wake?
Twende kwenye matumizi ya serikali; display ya ukwasi wa CCM katika taifa ambalo sehemu kubwa ya vijana wake wanaumizwa na umaskini uliokithiri ilikuwa na ulazima gani?
Mabasi ya CCM kwa mamia kama sio maelfu, mapikipiki ya CCM kwa maelfu mama sio malaki, magari ya kifahari, tambo za matumizi ya anasa za viongozi, yote haya yalikuwa na ulazima gani? Yani mlikuwa mnajaribu kutuma ujumbe gani kwa umma?🤔🤔
Halafu mnafanya hayo wakati kila kukicha mnawaona wananchi wanavyoteseka na usafiri hapo Daresalaam. Watu wanalazima kusafiri kwa tabu kuliko hata ng’ombe halafu nyie mpo busy kuwamock kwa kuwaonesha namna mnavyochezea kodi zao. Mlikuwa mnawaza nini??
Watu wanalia njaa, vijana wanalia hawana ajira wala means ya kipato lakini nyie ndio kwanza mpo busy kupita kwenye makanisa na kuhonga viongozi wa dini mamilioni ya pesa waziwazi kabisa. Mlikuwa mnawaza nini??
Halafu kama haitoshi Mkuu wa Mkoa kama Chalamila anamjibu mama mjamzito kuwa aende akapasuliwe na mumewe nyumbani kama hana uwezo wa kununua vifaa vya kujifungulia kwenye hospitali za umma. Really? Hili ndio jibu la kiongozi anayetumia million 600+ za kodi ya umma kununua gari ya kutembelea huku wananchi wake wakikosa vifaa vya kujifungulia mahospitalini?🤔🤔
Tuje kwenye lile igizo la uchaguzi. Kulikuwa na ulazima gani kudanganya wazi kabisa kwamba watu wote wenye sifa ya kupiga kura Tanzania wamejiandikisha kupiga kura tena ndani ya siku kumi tu?
Hivi kweli Tanzania hii tunayoifahamu kwa elimu ya watu wake, uchumi wao, na hata interests zao kwenye masuala ya siasa inaweza kweli kuwa voter registration ya rate hiyo hata miaka 100 ijayo??
Kulikuwa kuna ulazima gani wa kuwa arrogant kiasi hiki katika hali ambayo hata mpumbavu anaona kabisa hampo serious?
Lengo lilikuwa ni ili mseme Samia alichaguliwa kwa kura milioni 33 na kupata ushindi wa asilimia 98%?🤔 Ili iweje?🤔🤔
Yani mlitaka kusema SAMIA kimiujiza ameongeza kura za incumbent kutoka milioni 12 za Magufuli 2020 mpaka milioni 32 mwaka 2025?🤔🤔 Kwamba ndani ya miaka minne tu watu wameelimika, wamehamasika, wametambua umuhimu wa kura, na kumpenda SAMIA kiasi cha kujitokeza kwa asilimia 200% zaidi?🤔🤔
Then what?🤔🤔🤔
Mnawezaje kuparade kiburi kwa kiasi kikubwa hivi halafu halafu wananchi wakitoka kudemand mabadilko mnawau kwa maelfu?🤔🤔
Wakati mnafanya haya mlikuwa mnahisi mnaongoza magogo au?🤔🤔🤔🤔