Leo, CHADEMA imetunga sheria (PRECEDENT) mpya. Imefuta DHANA POTOFU kwamba maandamano ni FUJO! Hili tukio ni la KIHISTORIA na itakuwa VIGUMU kwa Polisi KUZUIA maandamano yanayofuata kutokana na kauli za wanasiasa wa vyama vingine. CHADEMA imetengeneza USHAHIDI (evidence). ☄️
Leo ni mwanzo mpya wa mwaka 2026. Tunafungua ukurasa wa kwanza wa kitabu kipya chenye kurasa 365 tupu, kinachotualika kutafakari yaliyopita jana, kuishi kikamilifu leo, na kuwa na matumaini thabiti kwa ajili ya kesho.
Hata hivyo, Siku hii ya Mwaka Mpya inawasili katika ukimya unaotia wasiwasi. Tundu Lissu yupo jela kwa zaidi ya siku 268 na amezuiwa kuzungumza na Taifa leo.
Tundu anaendelea kusimama imara bila kuyumba wala kufanya maridhiano hadaa, na imani yake katika haki ya lengo alilolitumikia maisha yake yote bado haijatetereka hata kidogo.
Kwa hiyo, karibuni tena kusikiliza kwa makini na kwa tafakari maneno aliyoyasema mwaka moja uliopita, katika hotuba yake ya “Salamu za Mwaka Mpya 2025.”
Maneno haya, aliyo yasema wakati ule, sasa yana uzito mpya na uhalisia mkubwa zaidi.
#HakunaMaridhianoBilaUkweliNaUwajibikaji #HakunaAmaniBilaHaki
#NoReformsNoElections
#FreeTunduLissu
— Admin
Leo ni mwanzo mpya wa mwaka 2026. Tunafungua ukurasa wa kwanza wa kitabu kipya chenye kurasa 365 tupu, kinachotualika kutafakari yaliyopita jana, kuishi kikamilifu leo, na kuwa na matumaini thabiti kwa ajili ya kesho.
Hata hivyo, Siku hii ya Mwaka Mpya inawasili katika ukimya unaotia wasiwasi. Tundu Lissu yupo jela kwa zaidi ya siku 268 na amezuiwa kuzungumza na Taifa leo.
Tundu anaendelea kusimama imara bila kuyumba wala kufanya maridhiano hadaa, na imani yake katika haki ya lengo alilolitumikia maisha yake yote bado haijatetereka hata kidogo.
Kwa hiyo, karibuni tena kusikiliza kwa makini na kwa tafakari maneno aliyoyasema mwaka moja uliopita, katika hotuba yake ya “Salamu za Mwaka Mpya 2025.”
Maneno haya, aliyo yasema wakati ule, sasa yana uzito mpya na uhalisia mkubwa zaidi.
#HakunaMaridhianoBilaUkweliNaUwajibikaji #HakunaAmaniBilaHaki
#NoReformsNoElections
#FreeTunduLissu
— Admin
Tofauti kati ya haki na dhuluma iliyojaa uonevu ndiyo msingi wa mapambano ya kweli ya kujenga Taifa bora. Wizi wa kura na kuumiza wananchi ili CCM ipate mamlaka ni jinai, na historia inaonyesha kuwa jinai hulipwa, leo au kesho. Mmeumiza sana nchi hii. Sasa nuru inataka kupambazuka, lakini mnajaribu kuizuia kwa propaganda, ikiwemo kuingiza udini kwenye siasa. Mmeua kabisa dhana ya utawala bora, na mnaacha taifa bila mwelekeo wa matumaini. Kila sekta mmeiharibu. Taifa haliwezi kuongozwa kwa propaganda. Mwisho wa udanganyifu umefika, na ubaya wowote una mwisho.
TUNAJIPANGA VIBAYA NA KUISHIA KUHARIBU KILA KITU.
1.Hatujakubali kanuni ya Ukweli,Haki na Uwajibikaji kama Msingi na dira ya kuliongoza Taifa letu katika jitihada Jumuishi za kutafuta ufumbuzi wa kilichotokea kabla ,wakati na baada ya Oktoba 29,2025
2.Kupitia Jeshi la Polisi linaendelea kukamata watu wa ndani na Nje ya nchi kwa namna ya ubaguzi na isiyokuwa na ueledi kisheria kwa mambo yaleyale wanayo lalamikiwa kama chanzo cha Mauaji ya Halaiki ya Vijana na Watanganyika wasio na hatia ambayo tunataka yawe sehemu ya tinachokiita Maridhiano.Hili ni kosa kubwa.
3.Tunaendelea kuwatuhumu watanganyika wenzetu waliokimbia nchi kujinusuru roho zao badala ya kuelewa hoja zao tunatafuta jina baya ili tuwadhuru, kuwakamata, kuwabambika makesi na kuwaita wachochezi,sijui vibaraka au wanaolipwa na Mataifa ya nje wakati kiuhalisia tunajuwa kabisa siyo kweli na hawa wenzetu wana haki ya kutoa Maoni yao iwe kwa lugha nzuri au mbaya Maoni ni Maoni .
4.Wanao pigia chapuo Maridhiano huku wakikwepa msingi wa kufikia maridhiano wengi wanakuwa walewale walio husika kuwabeza wananchi walipotaka marekebisho ya kikanuni, kisheria na kiuwajibikaji na kuweka mkazo kwenye Amani huku wakiibagaza Haki katika demokrasia ya Uchaguzi.
Ndiyo maana tunazungumza maridhiano huku Tume ya Uchaguzi ambao ndiyo watuhumiwa wakuu wa vurugu za uchaguzi wa Oktoba 29 bila hofu na kwa ujasiri bila kuwajibika wakiendelea kutimua mbio na chaguzi zao ndogo zisizokuwa na vichwa wala miguu.
5.Tuna zungumzia Maridhiano huku Serikali kupitia jeshi la Polisi ikionekana kuwashambulia kwa mkakati maalum wakosoaji ,ikitweza haki za kiraia na kuwachukia watanganyika waishio nchi za nje badala ya kuelewa concern yao na msingi wa hoja zao serikali inajaribu kuwa kamata na kuwabambika kesi .katika mazingira haya kuitana mezani kwenye suluhu ukiwa na panga mkononi ni kuanza mazungumzo kwa namna ya kushindwa.
6.Tunazungilumzia Maridhiano huku Waziri mkuu akizunguka nchi nzima na kutoa kauli kali za shutuma ,akibeza,akitifuatifua na kudogodesha msingi wa vurugu na Mauwaji ya raia yakiyofanyika Oktoba 29,akionekana kuumizwa na kusononeshwa na uharibifu wa magari,pikipiki,mikokoteni na vituo vya mafuta lakini akishindwa kabisa kuimizwa na vifo vya wajawazito, watoto, waandamanaji na hata ambao hawakauandamana ambao wengi waliuwawa majumbani mwao na wengi hadi sasa Maiti za ndugu zao hazijulikani ziliko ,Mamia wametekwa na kupotezwa lakini hatujasikia Kauli ya kukwazwa na https://t.co/IaSvRa7omZ hapa Maridhiano yatakuwa kati ya serikali na barabara? Magari? vituo vya Mafuta na majumba yaliyochomwa?
7.Tunazungumzia Maridhiano ambayo ni matokeo badala ya kuzungumzia njia yakutufikisha kwenye matokeo kwa pamoja ambayo ni Ukweli, Haki na Uwajibikaji.
8.Tunazungumzia Maridhiano bila kuzungumzia wanao ridhiana ni nani na wanaridhiana nini kwa utaratibu upi? Je umewahi kujiuliza ni karidhiano ya nani na nani? .Ukweli ni Upi? Vipi kuhisu Haki za wahanga? waliopotezwa wako wapi? nani alifabya nini na kwanini?
huwezi kufikiri Maridhiano wakati hujapata majawabu ya maswali haya. Hili jambo siyo monogamy ni jambo lenye sura nyingi na haliwezi kuzibgunziwa Maridhiano kana kwamba ni mgogoro wa watu wawili au vyama viwili vya siasa. Huu ni mgogoro dhidi ya Raia.
9.Kuzungumzia Maridhiano na kukwepa kuzungumzia msingi wa kufanikisha muafaka wa kitaifa ni kutamani kwenda mbinguni lakini wakati huo huo unaogopa kufa.
10.Kuzungumzia Maridhiano huku tukishambulia taasisi zilizosimama kidete na raia wakati wa majonzi na hata kabla ya majonzi kutaka kuepusha sintofahamu hii.
Mfano TEC ambapo hata baadhi ya viongozi wake walishambuliwa kutaka kuuwawa wakati wakiwa kwenye jitihada za kutaka kulinusuru Taifa na yale yaliyotokea Oktoba 29 itakuwa sawa na Muislamu anayepinga Utume wa Mohamed SW au Mkristo anayepinga wokovu kupitia Yesu Kristo.
BAK Mwabukusi.
GIRISHONI
Tuliposema mradi wa SGR kuna pesa za walipa kodi zinatumika vibaya, mlisema “TUNATUMIKA NA MABEBERU” Mvua imenyesha kidogo, daraja limebaki linaning’ia angani kama kende za mbuzi..
TRC wanasema safari kati ya Morogoro-Dodoma zimesitishwa kutokana na athari ya mvua zilizopelekea uharibifu wa miundombinu. GIRISHONI unasema reli haijaharibika ni tahadhari tu. UMEROGWA?
Kwa hiyo tuache kuwasikiliza Tanzania Railways Corporation (TRC) wanaosema uharibifu wa miundombinu ndiyo chanzo cha kusitisha safari tukusikilize wewe unayesema ni tahadhari?
Tuwapuuze wataalam kutoka TRC wanaosema safari zimesitishwa hadi marekebisho yatakapokamilika, tukusikilize wewe ‘government propagandist’ unayesema hakuna uharibifu ni tahadhari tu?
Mnawaona watanzania wote ni wapumbavu na wajinga kwa wakati mmoja? Tahadhari gani muhimu ambayo mmechukua? Hiyo SIYO tahadhari. Mvua kidogo imewaonyesha jinsi mnavyotumia pesa zetu vibaya.
This was a design and build project. Ni wazi, takwimu walizokusanya hazikutafsiriwa vizuri kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia ya nchi. Halafu, over designing sio dhambi katika uhandisi. Inafanyika vizuri.
Wali’ over design KILOSA kupita mto MKONDOA ndio maana kuna pale kuna 4 tunnels. KIDETE kuna uzembe. Maana palijengwa bwawa la Kidete wakati wa mkoloni kudhibiti maji yanayotokea Kiteto (Manyara)
Kama hayakuwa factored out kwenye design hii kuna ujanja umetumika ili zipigwe pesa za umma hapo. Hapo kabla, tumewashauri sana kuhusu the conventional way of tendering vis-a-vis the feasibility study..
Ndiyo madhara ya single source procurement. Zabuni sahihi katika nanunuzi ya umma ni zabuni za wazi (open tender) na washindani wajulikane. BIDS shindani zionekane pale TANePS. Hamzitaki zabuni hizo…
KILOSA, reli ilitakiwa kupita juu. Wahuni waliopitisha chini some sections walilenga kuokoa gharama zao at our blood expenses. Mjerumani alipojenga reli, anajua KILOSA ni flood prone area. HAMJUI?
SGR ya majirani, KENYA ina miaka zaidi ya 10. No single technical hitch; NO single accident. Wamejenga CHINA. Majirani wakiweza kuunganisha Malaba - Kampala. Tumekwisha; tutabaki na monuments tu.
Wengine tulilia machozi Mturuki kupewa huu mradi mkubwa sana kwao. Hatukusikilizwa kamwe. Waturuki SGR ndio mradi wao wa kwanza kufanya MKUBWA. Lazima wazushi mkubali, it was a learning trail
Ipo hivi, hatutakiwi kukubali kuingia gharama hata jero au buku kwani mradi bado upo kwenye liquidated liability period. Uharibifu wowote na uzembe ni jukumu la mkandarasi ikiwemo fidia ya loss of business
Itakua kosa kubwa kama pesa za walipa kodi zikitumika kurekebisha huo uharibifu na uzembe. Aajiriwe independent consultants kupitia mradi mzima, kama kuna technical shortfalls zote zirekebishwe
Machi 2013, Rais wa China, Xi Jinping katika ziara yake Tanzania, mikataba zaidi ya 17 ilisainiwa ukiwepo mkataba wa ujenzi wa reli ya SGR, full delivered ndani ya miaka mitano. Uzinduzi ulifanyika PUGU.
Sisi walipa kodi, hatuelewi kilichotokea. Hivi kweli mnaweza kutueleza kwanini mliachana na WACHINA na mkawachukua hawa WATURUKI? Technical issues? Ndiyo mkaamua kuwachukua WATURUKI?
Tunaishia kulipa gharama kubwa mwaka wa nane hatujafika mbali na gharama imekua exorbitantly high. Tutafute wataalam, wa’ overhaul mradi wote. SGR ni mradi wa kimkakati na kikanda. Tumieni akili.
UPDATE 6: Kesi ya Thadei Kweka
January 1, 2026
1. Mawakili wa Thadei wame—file Habeas corpus ili afikishwe mahakamani haraka. Matarajio Jumatatu kesi itasikilizwa
2. Pia, Mawakili wame—file revision (marejeo) ya maamuzi kumtaka Thadei atoe password ya simu yake kwani kuna suala la kukiuka haki ya kimsingi ya privacy.
3. Bado Thadei ameshindwa kutoa password kwa sababu haikumbuki baada ya kupitia unyanyasaji wa kisaikolojia tokea akamatwe. Zoezi la kutoa password limeshindikana hadi hapo Thadei akikumbuka password yake.
5. Polis bado wamemkatalia Thadei dhamana.
6. Leo Thadei amesaini form kutoka Ubalozi wa Marekani baada ya pressure kubwa kutoka Ubalozi wa Marekani.
7. Thadei anashtakiwa kuchapisha taarifa za uongo kwenye groups za *”what sup”*. What sup hatujui ni Application gani haya Thadei mwenyewe haelewi!
8. Thadei yupo kwenye spirit nzuri na anawashukuru diaspora kwa kusimama naye na anatambua hii sijui vita dhidi yake, bali ni vita dhidi ya diaspora wote.
Tutaendelea kuwapa taarifa.
#FreeThadeiKweka
Asante
Huu Kama sio uhujumu uchumi ni nini?
Yaani Makame Mbarawa bado eti ni waziri.
Masanja Kadogosa eti ni mbunge… wahujumu wa Nchi eti ni viongozi wa umma..
Watu wema wako gerezani…
Alafu eti kuna mtu anaitwa waziri mkuu, utetezi wake kwenye uhujumu huu ni kwamba hata Nchi Kubwa SGR huwa inasimama!!!! Fikiria akili kama hizo..
Nchi ambayo watu wanalala njaa, watu wanakufa kwa kukosa panadol… pesa zao zaidi ya trilioni zanateketea kabla hata ya miaka miwili kwasababu ya uzembe, wizi na ujambazi..
Hatutakubali.
Hakumpotea bure, mateso yenu na damu za wengine wengi kama nyie zitanena kwa sauti kubwa sana kuanzia sasa. Malipo ya damu ni ahadi ya Mungu. Zamu ya malipo ya wasio haki kupokea mishahara yao ni sasa. Nchi itamtukuza Mungu maana harufu ya uovu iko kwa Mwenyezi Mungu. Ushuhuda mkubwa kwa familia zenu unaanza Mwaka huu wa 2026. Tutamsifu Mungu maana tulikosa nguvu tukamtazama yeye na kumtumaini yeye. Halikuwa jambo baya wala uoga bali tumaini lenye kutambua kuwa yeye yupo.
@TweveDevota Mimi nataka kujua Huko Ccm vipi? Ile ahadi ya kutangaza TIBISI wamekupa?
Iman ni njia ya ukombozi , kujiunga na ccm kuwa chawa ni kujunga na mkono wa shetan kwa matendo yake.
Unamdanganya Mungu
Anaandika @MalisaGJ_
Nasikitika kuwajulisha kuwa jana majira ya saa 8 usiku (kwa saa za huko nyumbani) watu wenye silaha walivamia nyumbani kwa wazazi wangu, kijijini Old Moshi Kidia. Kabla ya uvamizi huo watu hao walionekana wakiwa na gari mbili (Landcruizer) zisizo na plate number wakipanda na kushuka barabara ya Old Moshi kwa siku kadhaa. Jana saa 8 usiku wameingia nyumbani na kukata umeme.
Wakiwa wamefunika nyuso kwa mask, wamezunguka maeneo mbalimbali ya nyumba wakimulika kwa tochi bila kuvunja mlango wala kubomoa kuta. Asubuhi palipopambazuka ilibainika kuwa walipanda juu ya tank la maji na kufungua (mfuniko wa tank umekutwa chini). Haieleweki wameweka nini. Kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji maji hayo yamemwagwa na tumezuia tank hilo lisitumike tena kutunzia maji.
Baada ya kutoka nyumbani walienda pia kwa baba yetu mkubwa usiku huohuo na kusababisha taharuki, ambapo wanafamilia walipiga kelele na watu hao kuondoka. Hali hii imeleta hofu na usumbufu mkubwa kwa wazee wetu ambao wana zaidi ya miaka 70. Tumetoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kwa polisi Kata kwa sababu hatujui malengo ya watu hao. Keep us in your prayers 🙏🏽
"Ni juzi tu watu wamekufa kama panya alafu tunaambiwa usiseme hicho, na sisi tumekuwa wapumbavu tunadhani hizi ni zama kama zile za mababu "-; Padre Parokia ya kiwanja cha Ndege Dodoma.
In response to the election protests between 29 October and 3 November 2025 in #Tanzania, security forces used unnecessary or disproportionate force, amidst a nationwide internet shutdown, showing a shocking disregard for the right to life and to the freedom of peaceful assembly.
Keep the spotlight on Tanzania and call for independent, thorough, prompt and impartial investigations into the human rights violations by security forces during election protests. Our latest findings, out now: https://t.co/us2wGmzpLX
#ProtectTheProtest #KeepEyesOnTanzania
“Bavicha inatambua kuwa mauaji haya hayakufanyika kwa bahati mbaya yalikusudiwa, yaliandaliwa kwa kuzingatia kauli na maagizo yaliyokuwa yakitoka kwa viongozi wa Serikali na vyombo vya Dola, kwa kuwa mauaji haya ni matokeo ya amri rasmi”;- Mhe. @duahamud, Katibu Mkuu BAVICHA.
“Uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba,BAVICHA tunaendelea kusema kuwa ni batili,haukuwa uchaguzi bali mchakato haramu wa kudhalilisha demokrasia na kuhalalisha uporaji wa madaraka”.-; @duahamud, Katibu Mkuu BAVICHA Taifa.