@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
🇺🇸 The Secret Service told Trump to leave his new Qatari jet behind when flying out of Turkey...
Agents advised the president to depart on the legacy aircraft because it carries fully integrated secure communications and the military grade defense systems the job demands.
The Qatari donated plane was rushed into service and still lacks capabilities considered desirable for presidential travel, even as the White House insists it comes equipped with advanced security features.
The timing gave the recommendation teeth.
Trump flew out of Ankara days after Israel warned of a fresh Iranian plot against him, and with funeral crowds in Tehran waving banners promising his death.
When the threat picture looks like that, hardened comms and missile defenses beat new furniture every time.
Source: CBS News / Writer: Daniel
US President Donald Trump has already left his mark on the new Air Force One jet, signing his name on the Boeing 747 donated by Qatar. Trump has described the jet as a luxurious 'flying White House'.
Umewahi kuchunguza tabia za watu wenye nguvu na mamlaka wanapokuwa kwenye majukwaa sogozi? Nazungumzia majukwaa kama makundi ya WhatsApp yanayokutanisha watu wanaofanya kazi pamoja, watu wanaokutanishwa na kusudi fulani, wanaofahamiana kwa historia ya kusoma pamoja (alumni). Umewahi kuwachunguza wale wanaozungumza muda wote na kulinganisha na tabia zao katika majukumu nje ya majukwaa?
Sina rejea ya utafiti wowote na sijafanya utafiti rasmi ninachotaka kukisema ni maoni ya ‘pattern’ ambayo huenda isiwe sahihi sana. Nafikiri nguvu (mamlaka) yana tabia ya kunyamazisha watu. Kwenye makundi machache ya WhatsApp niliyopo, naona kama watu wenye nguvu katika uhalisia wa maisha ni wakimya na hawajitokezi sana kusema sema tofauti na wepesi wenzangu wasioishiwi cha kusema. Huenda na wewe umewahi kujiuliza inakuwaje kuna watu unaamka unakuta wanaongea kwenye Group na unaenda kulala unawaacha wanaongea. Karibu kila kinachotokea wana taarifa nacho, wana-forward na hawakosi maoni. Unajiuliza hawa watu wanafanya kazi saa ngapi huko waliko?
Halafu kuna hawa ambao unaweza usijue kama wapo kundini maana hawana-ga maoni. Huwezi kusikia wakiongea wala wakibishania jambo. Utawaona pale panapohitajika kuchukua hatua (michango, uamuzi kwa mfano) na ni kama hawana chochote cha kusema. Hawa ikitokea wanaongea, sauti yao inakuwa-ga na mshindo maana hawashambulii mtu, hawajitetei wala kulalamika. Huja na taarifa zenye majibu na ufumbuzi na kupotea. Hawa kama unawafahamu wanakuwa-ga ni watu wenye nguvu katika maisha halisi, wana utulivu fulani unaotisha, wana taarifa sahihi, na hawahitaji kuonekana.
Nafahamu kuna watu ni waongeaji tu kwa hulka na wengine ni wakimya hata kwenye vikao unaweza kuhesabu maneno yao. Hata hivyo, waongeaji wengi hunyamaza kitu fulani kinachowapa nguvu kikitokea. Sidhani kama hili hutokea kwa bahati mbaya lakini kuna namna vitu fulani katika maisha vikitokea mtu anakuwa na utulivu unaomnyamazisha asione haja ya kujieleza muda wote anapokutana na watu. Kwa lugha nyingine kwa kutazama tabia za mtu kwenye makundi sogozi unaweza kujua kinachoendelea katika maisha yake huko alipo. Unagundua mwepesi, mnyonge, huwa hakosi maoni pengine kwa kuamini kelele zinampa nguvu, wakati mwenye nguvu husema mengi kwa kutokusema. Naweza nisiwe sahihi na haya ni maoni tu yasitafsirike kama majumuisho.