DODOMA: Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wa mapingamizi yaliyowekwa na Chama Cha Mapinduzi (#CCM) dhidi ya Mchungaji Dkt. Godfrey Malisa, ambaye anapinga uhalali wa mchakato uliompitisha Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwania urais kupitia Chama hicho.
Mawakili wa CCM, Fabian Donates na Alex Mgongolwa, leo Agosti 19,2025 wamewasilisha mapingamizi wakidai hatua za kufungua shauri hilo hazikufuatwa, huku wakisisitiza mlalamikaji alipaswa kuandika barua kwa Katibu Mkuu badala ya mwenyekiti wa Chama.
Aidha, wakili wa mlalamikaji, Denis Maringo, amesema taratibu zilizingatiwa kwani Februari, 2025, Dkt. Malisa alimwandikia barua Rais Samia akilalamikia uteuzi wake, ambapo baada ya hoja za pande zote kusikilizwa, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 22, 2025.
Soma https://t.co/2q7d7u9pzJ
#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
Wizara ya Elimu nchini Ethiopia imetoa Mwongozo mpya unaopiga marufuku Viongozi wa Serikali na viongozi wa Kisiasa nchini humo kutunukiwa Shahada za Heshima (Honorary Doctorate).
Agizo hilo ambalo limetiwa saini na Waziri wa Elimu Nchini Ethiopia Profesa Berhanu Nega kuwasilishwa kwa Vyuo vikuu na taasisi za Elimu nchini humo limezitaka taasisi hizo hususa ni Vyuo ambavyo Wanafunzi wake hawajahitimu angalau awamu nne na havitoi Shahada ya Uzamilivu havitoruhusia kutokoa shahada ya Heshima.
Mwongozo pia unaeleza kuwa Shahada za Heshima zinaweza kutolewa kwa raia wa Ethiopia au Wageni waliotoa mchango wa kipekee katika taaluma au nyanja zao za kazi. Tuzo hiyo inaweza kutolewa kwa mtu mmoja au kikundi kilicho hai au kilichofariki, mradi kimekidhi vigezo vilivyowekwa.
Aidha kuna masharti ya vizuizi Kifungu cha 2 Ibara ya 10 kimeeleza kuwa wafanyakazi wa kudumu wa vyuo vikuu, wajumbe wa Seneti au miundo ya uongozi hawawezi kupokea shahada ya heshima wakati bado wako kazini, isipokuwa pale ambapo uhusiano wao rasmi na chuo hicho umeisha na pia viongozi wa serikali walioko madarakani hawataruhusiwa kuteuliwa kabisa.
Sambamba na hilo kwa mujibu wa masharti ya mwongozo huo chuo kikuu kitakachotoa shahada ya heshima kinapaswa kuwa kimehitimisha angalau wanafunzi wa awamu nane, kinatoa kozi ya PhD, kinakubalika kwa viwango vya kitaifa na kimataifa na kutokana na masharti haya, vyuo vipya kama vile Selale, Dembi Dolo, Mekdela Amba, Raya, na Debarak havitaruhusiwa kwa sasa kutoa shahada za heshima.
#MillardAyoUPDATES
Kuchangia chama au kiongozi ni vizuri kwa sababu inaonesha chama au kiongozi anapendwa na wanachama. Ila taasisi za dini na timu za mpira haziruhusiwi kujihusisha na Siasa. Sio sahihi Mwamposa na Yanga kuchangia CCM kwa sababu ya waumini na mashabiki wa vyama mbalimbali.
Siasa za kiinimacho na fikra za walalahoi.
Watu wanafanya udalali wa kisiasa.
CHADEMA ya kwenye kanda mbalimbali ilikuwa ya Mbowe, ilivyoshindwa uchaguzi mkuu ikaanzisha G-55, sasa wapo CHAUMMA na ACT-Wazalendo.
CHADEMA ya kamati kuu ni ya Lissu, imenyooka.
Askofu Dkt. Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amesema Watawala wabaya huanza kwa kuchafua hekalu ili kuzima sauti ya kukemewa.
Amesisitiza kuwa ni wajibu wa Viongozi wa Dini kuonya na kukemea maovu yanayotokea kwenye Jamii, na kama watashindwa, basi waoneshe kutokubaliana kwa kununa. Alitoa kauli hiyo Julai 12, 2025 wakati wa ibada ya kuweka wakfu vifaa na alama za Askofu Mteule wa Dayosisi ya Mwanga.
Soma https://t.co/jlWtmA5cC7
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFUtawala #Uwajibikaji #Governance
Ukisoma sura ya 5 ya Animal Farm utagundua Tanzania ni Orwellian State kwa asilimia 100%.
Hakuna chochote kilichoongelewa kwenye hiki kitabu ambacho leo hatukiishi.
Sio kamari tu, Dira 2050 inahitaji kuwa na kipengele maalum kinacholenga kulinda sanctity ya rasilimali watu yetu.
Pombe za hovyo, kamari za kubet, na na aina nyingine nyingi za urahibu ni hatari sana katika maendeleo ya watu wetu.
Kwenye taifa ambalo zaidi ya asilimia 70% ya watu wake wana elimu ya darasa la saba, ni hatari kuruhusu vitu hivi kufanyika kiholela holela kama invyofanyika sasa.
Yes, tunakusanya kodi kubwa sana kutoka kwenye haya mambo lakini gharama ya rasilimali watu inayopotea ni kubwa na impactful kuliko hii kodi.
Wachina, WaSingapore, na kwengineko waliiona hii hatari ndio maana fasta wakaanza kutumia falsafa za Confucius kutengeneza misingi ya morality kwenye jamii zao.
We need this, tunahitaji kufanya hivi kuliko tunavyodhani. Lazima tutafakari aina ya jamii tuliyonayo and how fragile it is when exposed to these toxics.
@kitilam
Kwenye #Dira2050 nimeona mengi sana kuhusu UCHUMI na mengi kuhusu SIASA.
Hata hivyo sina hakika kama nimeona ya kutosha kuhusu JAMII.
Kwa mfano, najaribu kuwaza kama tutakuwa na taifa hiyo 2050 endapo tutaendelea kuwaexpose vijana wetu kwenye uraibu wa kamari, pombe kali, na utapeli wa madhabahu kwa kasi tuliyonayo sasa.
Nadhani mipango ya kuilinda jamii dhidi ya hivi virusi ni muhimu sawa na mipango ya kiuchumi pamoja na ile ya kisiasa.
Lazima tuwe na wivu na vijana wetu; lazima tuilinde rasilimali watu yetu sasa while we can.
@kitilam
Mbunge wa Jimbo la Kisesa anayemaliza muda wake Luhaga Mpina huenda safari yake ya kuwawakilisha wananchi wa Kisesa ikafikia tamati ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka huu baada ya vikao vya mchujo kwa ngazi ya wilaya ya Meatu na mkoa wake wa Simiyu kumtupa nje ya mbio za kuwania kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera kwenye nafasi ya ubunge katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu; vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya kikao cha kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu vimeitonya Jambo TV.
Mpina Mbunge machachari ndani na nje ya Bunge aliyejipatia umaarufu kwenye takribani miaka mitano sasa kwa kuibana serikali ndani ya Bunge na hata nje ya Bunge kwa hoja mbalimbali amekumbana na rungu la chama chake ngazi ya wilaya na mkoa baada ya vikao vya Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Meatu kumtupa nje kwa kutopendekeza jina lake- maamuzi ambayo yamebarikiwa na chama ngazi ya mkoa hivyo sasa nafasi ya mwisho ya yeye kupenya jina lake kwa ajili ya kwenda kwenye mchakato wa kura za maoni ikibakia vikao vya ngazi ya taifa kwa maana ya Kamati Kuu ambayo imepewa mamlaka ya kufanya uteuzi wa mwisho.
Katika jimbo hilo, wagombea waliokuwa wakichuana katika hatua ya awali walifikia 14, lakini kupitia kikao cha wilaya na mkoa, majina yaliyopendekezwa ni Sitta Risinge, Mussa Mbuga, na Silinde Gumada.
Kiujumla, majina yote yaliyopendekezwa ngazi ya wilaya na mkoa hupelekwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa, na Kamati kuu hiyo ina uwezo wa kuja na mapendekezo yake ya majina kwa kurejea majina ya awali ya wote waliochukua fomu, waliopendekezwa nkwa upande wa wilaya na hata yale ya mkoa.
Baada ya hapo Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kitapokea na kuchambua majina ya wagombea Ubunge kwa ajili ya maandalizi ya vikao vya uteuzi, kisha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kitafikiria na kuteua majina ya WanaCCM wasiozidi watatu walioomba nafasi ya Ubunge na ili wakapigiwe kura za maoni na hatua zaidi ndani ya chama zitafuata kabla ya kumpata mgombea atakayekiwakilisha chama katika jimbo husika.