Yaani kubadili jukwaa la siasa kunakuwaje usaliti hadi kuamua kumdhalisha mama mtu mzima hivi?? CHADEMA na Kiwanga vilibebana. Mama alishinda Ubunge kwa kuchaguliwa. Lema na Lissu walitoka NCCR na TLP wakaja Chadema kipindi CUF inasema CDM ni mpango wa CCM.Hii sio Democracy.
Kila siku nazidi kujifunza, TZ Udikteta ni asili yetu.Ukatili wa CCM unaakisi tabia ya watanzania wakipata madaraka. Kabla hamjatetea Ujinga leteni Clip ya Heche akisema usaliti wa Msigwa kwa maneno ya Chuki kama aliyoyatumia kwa Mama Kiwanga. Kiwanga anakuwaje msalit kwanza??
@onesmo_gerson@CatherineRuge Kwahyo ili kuwa halali kutete wanawake wanaodhalilishwa hadharani na viongozi wanaojiita ni watetezi wa haki ni lazima record yako ya kukemea iwe imekidhi kukemea wote?? Nyie nani kawaroga??
Umaarufu wa kweli haujengwi kwa kudhalilisha wanawake.
Mimi binafsi nawathamini na kuwaheshimu sana wanawake waliopigana kutoka chini hadi kufikia hatua za juu za mafanikio, ikiwemo kuchaguliwa kuwa wawakilishi wa wananchi. Wengi wetu, mimi nikiwa miongoni mwao, tumelelewa na mama zetu walioteseka kwa hali na mali, wakifanya kazi za kuuza mkaa, kuuza vitumbua, au hata kupika pombe za kienyeji ili kutuwezesha kupata elimu na kufika hapa tulipo leo kama viongozi wa jamii.
Kumdhihaki au kumdharau mwanamke anayefanya kazi za ndani ni kitendo cha kudhihirisha ujinga, ushamba na ukosefu wa staha. Hivi unamkejeli mwanamke huyo huku ukisahau kuwa hata mama yako alijitahidi kadiri ya uwezo wake kukufikisha hapo ulipo?
Kumsimanga Mama Kiwanga eti amejenga nyumba baada ya kuwa mbunge, ni dharau isiyo na sababu, na ni uwongo wa mchana kwa sababu MAMA Kiwanga alijenga nyumba hata kabla hujazaliwa.
Hata kama amejenga nyingine au ameiboresha baada ya kuwa mbunge, si jambo la kudhihaki, maana hata wewe ulijenga kwa fedha za ubunge. Kabla ya hapo hukuweza kumiliki hata kibanda, ulikuwa mpangaji tu huko uswahilini.
Tujifunze kuthamini juhudi na mafanikio ya wanawake wetu. Si kwao tu, bali kwa heshima ya mama zetu, hao mama wa ndani, waliotufikisha hapa tulipo. Tafadhali mwombe radhi Mama Kiwanga na wanawake wote!
Pamoja na viongozi wa kitaifa waliokamatwa leo walikuwepo viongozi kutoka Mkoa wa Dodoma, Katibu wa Mkoa, Mkiti Kongwa na Katibu wa Bahi.Viongozi hawa hawakufikishwa kituoni bali maporini. Ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi. HAIKUBALIKI
Kushikiliwa kwa Mwenyekiti wetu hakutorudisha nyuma mapambano haya ya kudai HAKI bali ni kutupa hasira ya kuendelea kwa nguvu. Hofu na uongo wa watawala ndio unazaa uonevu. Tutasimama imara na kuendelea na vuguvugu hili la kudai Reforms. #NoReformsNoElection#FreeTunduLissu