Well Rounded Broadcast Professional, Radio Host and Producer, TV Presenter (EA Radio & TV) | Part Time Script Writer | Marketing and Communications Expert.
Mama wa Konektion mjini @ireeneyes anatukutanisha na wadau wa sheria ambapo unaambiwa, endapo kama Mwanandoa utakaa kimya kwa muda wa miaka mitano mfululizo na upo kwenye ndoa basi mwenza wako anayo haki ya kufunga ndoa nyingine kwa dhana ya kifo.
#DriveShow#EastAfricaRadio
I am Honoured and humbled 🙏🏾 for some of my Artworks from the Exhibition i did in 2021 called SHADES OF MAGUFULI, to be a part of this🇹🇿🇹🇿.
Much appreciation goes to the family of The late John Pombe Magufuli for the great support.
Jana katika kusherehekea siku ya walimu duniani kwenye #DriveShow tulikuwa na Mwalimu Michael Mahundi ambaye ni mtaalam wa somo la hisabati mpaka wazazi wakampachika jina la ''Mwalimu wa vichwa vigumu''.
#EastAfricaRadio#DriveShow
Mama wa Konektion mjini @IreenEyes leo anatukutanisha na mtindo wa maisha ambao unapelekea kupata maradhi ya shinikizo la damu.
Kutazama kwa urefu zaidi ingia kwenye youtube channel ya #EastAfricaRadio
Tusikilize #DriveShow kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 10:00 jioni mpaka 1:00 usiku.
Mtangazaji wa kipindi cha #MamaMia cha East Africa Radio, Ritha Chuwalo @RithaChuwalo2 akiwa nchini Kenya amepokea cheti kutoka taasisi ya AVAC ya Nchini Marekani baada ya kumaliza mafunzo ya kuripoti magonjwa ya mlipuko pamoja na chanjo yaliyotolewa kwa siku tatu na taasisi hiyo jijini Nairobi, Kenya.
Baada ya kupokea cheti hicho Ritha kupokea ukurasa wake wa instagram ameandika
''Naishukuru Taasisi ya AVAC ya Nchini Marekani kwa kufadhili mafunzo haya kwa jamii mbalimbali za watu wa Afrika kupitia sisi waandishi wa habari ambako magonjwa ya mlipuko ni janga kubwa kutokana na mazingira wanayotoka.
Pili nawashukuru tena na tena Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA kwa kunipendekeza kushiriki mafunzo haya na tatu na mwisho lakini sio kwa umuhimu ni Uongozi mzima wa EATV Company Limited kwa kunipa kibali kuhudhuria mafunzo haya .
"Hata hizi field ambazo wanaenda vijana zinawasaidia nini, wakati mwingine haziwasaidii, kuna watu wengine wanafika kwenye ofisi yeye ni kuprint tu karatasi, wanatumwa chai, mwisho wa siku miezi mitatu inakatika alichojifunza hakuna"
#NUKUU "Jinsi ya kujikinga na Marburg ni kuepuka kugusana na maji maji ya mgonjwa, nguo, godoro na kitu chochote kilichotumiwa na mgonjwa, hata maiti iliyofariki kwa ugonjwa huu ina utaratibu wake wa kuzikwa"- Dr. Rashid Mfaume, RMO Dar es salaam.
#SupaBreakfast#EastAfricaRadio
Ikiwa zimebaki siku 2 tu kuelekea kwenye kilele cha #EATVKinara huyu hapa Mfanyabiashara wa nguo #FabtrendsTz ameshajipatia tiketi yake ya kushiriki katika kilele hicho kitakachofanyika pale Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel Jumamosi hii Machi 18, 2023.
#HABARI Afisa Ustawi wa Jamii katika halmashauri ya jiji la Dar es salaam Rosemary Wilfred amesema sheria ya sasa kwa mwanaume anayetelekeza mtoto baada ya kuzaa na mwanamke inamtaka mwanaume husika kulipa faini ya Sh. Mil. 5 ama kufungwa jela miezi 6 au adhabu zote kwa pamoja.
Mkutano wa kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 25 ya Siku ya Bima Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (Insurance Institute of Tanzania) unaendelea muda huu katika ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam.
@TIRA_TZ#TanzaniaInsuranceConvention2022
#Kipenga Mchambuzi wa soka Martin Mwakiposa akiuchambua mchezo wa @yangasc1935 dhidi ya Club Africain baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika nchini Tunisia.
Throw Back Thursday (TBT) Kundi gani la zamani la bongo flava lilikuwa lina kuvutia zaidi?
CHANGIA MADA
1. Tuma comment yako ukianza na neno #EatvTBT
2. Comment yako tutaruka nayo hewani leo saa 12:30 Jioni
#PICHA Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ndirigishi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wakiwa wamepanda juu ya mti ili kupata mawasiliano ya mtandao wa simu ambapo wamedai wakati mwingine huwa wanapata madhara ya kuanguka huku wakiomba Serikali kuingilia kati kuondoa adha hiyo.