Baadhi ya picha katika fainali ya #BashungwaKaragweCup iliyofanyika Jana katika uwanja wa Kayanga @JimboniKaragwe Hongera kwa Timu ya Nyakahanga kwa kutwaa Kombe na hongera kwa @innobash kwa kuleta hamasa ya michezo kwa vijana wa Karagwe.
Mbunge wa Karagwe @innobash amewasisitiza wananchi wote waliofikia umri wa kupiga kura (miaka 18 na kuendelea) kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa #UchaguziSerikaliZaMitaa2019
@kigogo2014 @innobash Bahati mbaya Mhe Waziri hajibu bunduki za kukodi ila kwa sababu umeshazoea kutumika kupost kila nyepesi unayopenyezewa bila kuhakiki nakushauri tafuta mahojiano aliyofanyiwa na @efmtanzania mwezi uliopita aliulizwa hili swali la kahawa na hizo kampuni akatolea ufafanuzi
Waziri wa Viwanda na Biashara @innobash ameungana na Waziri Mkuu Mhe @majaliwa_kassim katika ufunguzi wa kongamano la uwekezaji Kagera lililohusisha wadau wa uwekezaji na biashara takribani 300 toka Tanzania na nchi za jirani
#Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa Jana Amewasili Jimboni kwake Karagwe kwa ziara ya siku mbili hapa amefika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Karagwe na Kupokelewa na Viongozi na Wanachama wa CCM @hpolepole
Mashindano ya mpira wa miguu ya Bashungwa Karagwe Cup yanazinduliwa rasmi kesho na mbunge wa Karagwe Mhe @innobash kwa mechi kati ya Kamagambo vs Kiruruma. Mabingwa watetezi ni Ihembe
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akizunguza na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Ndugu Fred Kafeero na msaidizi wa mwakilishi huyo Ndugu Charles Tulahi katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam
#KFUPDATES: Wakulima wa chai mjini njombe wamemuomba Naibu Waziri wa kilimo Innocent Bashungwa(@innobash) kukirejesha kiwanda cha kuchakata chai cha Lupembe mkoani Njombe kwenye chama cha ushirika baada ya muwekezaji kushindwa kuwalipa wakulima hao kwa utaratibu wa ushirika.