Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) kinampongeza mwanachama wake, Anna Mwasyoke kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF). TAMWA inajivunia kupata sauti za wanawake katika ngazi za maamuzi. #WomenVoices
Access to Internet is essential for education, bussiness and free expression. Let advocate for #InetrnetFreedom and digital rights for all. No to censorship, yes to open & secure Internet! #DigitalRightstz#KeepItOn
Afya ni bora kuliko kinga...
Kama wewe ni mkazi wa Dar Es Salaam sogea kwenye kambi ya Afya Ukonga-Magereza kwa uchunguzi wa Saratani. Huduma hii ni BURE na ni kwa wakazi wote.
#PamojaTunaweza.
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji dhidi ya Mwanamke. Kauli mbiu ya mwaka huu inasema: 'Imarisha ushirikiano kutokomeza ukeketaji'. Hivyo basi TAMWA inaungana na dunia katika kupinga vitendo hivi dhalili kwa mwanamke na mtoto wa kike. #ZuiaUkatili
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania kimezindua jarida la sauti ya Siti.
Jarida hili linawakilisha sauti za wanawake ikiwamo mabadiliko ya sera , kupinga mila kandamizi, ukatili wa kijinsia na kuhamasisha maendeleo ya mwanamke katika jamii.
Namshukuru Mungu kwa kupata tuzo na kuwa mshindi wa kwanza kwa tuzo za uandilifu wa kitaaluma kwa waandishi wa habari wanawake na wanaume zilizotolewa na @UTPCtz. Ambapo kwa wanawake nimekuwa mshindi wa kwanza. @TheChanzo 🙏
Watoto wawili wa familia moja ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wanadaiwa kubakwa na kuambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) na baba yao wa kufikia.🙄🙄😥 #ZuiaUkatili#VunjaUkimya
Zawadi, msichana mwenye umri wa miaka 10 kutoka kijiji cha Mivumoni, alikuwa na ndoto ya kuwa daktari. Hata hivyo, maisha yake yalibadilika kabisa pale mjomba wake alipomlaghai na kumbaka.,
karibu kutazama simulizi hii yenye lengo la kupinga ukatili kwa watoto
#SimuliziZaJackie
Wazazi katika shule zilizotembelewa na @HakiElimu na kufanyiwa tathmini wameitikia vyema wito hata watoto wenye ulemavu wamepelekwa shule. Hii inaonyesha kwamba kuna mwamko wa kutambua umuhimu wa #ElimuJumuishi kwa watoto wote bila ubaguzi
"Jamii isiyo na ukatili huanzia mashuleni. Kama walimu, tunao wajibu wa kulea kizazi kinachoheshimu wanawake na watoto wa kike. Tushirikiane kuondoa ukatili kwa kuelimisha, kuonya, na kuonyesha mfano wa upendo na usawa kwa wote. Mwanamke na mtoto wa kike wana haki sawa za kuheshimiwa na kulindwa!" - Godfrey Abely (Mwalimu) @godfreyabely2
#TokomezaUkatili
#HakiHainaJinsia
Leo Disemba 11 2024 TAMWA imeshiriki kikao kilichoandaliwa na Women Creating Wealth (WCW) kwa kushirikiana na Graca Machel Trust kwa kwa lengo la kujadili jinsi ya upatikanaji wa njia mbadala wa mitaji kwa wanawake ili kijikwamua kiuchumi.#WCW
"Tumieni teknolojia vizuri msikae kwenye mazingira yatakayochochea rushwa ya ngono kama kutuma picha za utupu kwani ni kosa kisheria kufanya hivyo pia ni kinyume na maadili yetu." Dkt. Rose Reuben ~ Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA.
Mratibu wetu wa ofisi ya Tanga, Mh. Mwanaidi Kombo alipata fursa ya kushiriki kama Mgeni Rasmi katika Tamasha la kukuza Stadi za KKK (Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu) lililofanyika katika Shule ya Msingi Changa, Jijini Tanga. Tamasha hili lilihusisha wanafunzi wa Awali, Darasa la Kwanza, na la Pili.
Katika hotuba yake, mratibu wetu aliwakumbusha wazazi na walezi umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wao ili kuwaepusha na viashiria na vitendo vya ukatili wa kijinsia, kwani kuna uhusiano mkubwa kati ya maendeleo ya masomo ya watoto na kuzuia vitendo vya ukatili.
Aliendelea kueleza kwamba, ili watoto waweze kujua kusoma, kuandika, na kuhesabu kwa ufanisi, ni muhimu kwa wazazi kuwa walinzi na wafuatiliaji wa watoto wao, kuwaepusha na mazingira yenye hatari ya ukatili, na kuhakikisha wanapata chakula wanapokuwa shuleni kwa maendeleo bora ya masomo yao.
#HakiHainaJinsia
Nimetembea sehemu nyingi Tanzania kazi kubwa imefanyika katika kuboresha miundombinu mashuleni ikiwemo kwenye ujenzi wa vyoo lakini changamoto hivyo vyoo utakuta vingine havina maji, na miundombinu sio rafiki kwa watoto wa shuleni~ Mr Aman Msumari, @Plan_tanzania#IQEC2024