Mpaka sasa, tumefanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 170 katika Marathon ya kufikia Tsh. Milioni 334
TUNAWEZA KUFIKISHA 180M LEO, TUENDELEE KUCHANGIA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Kwa kawaida Mwalimu akiwa darasani ni sawa na mbunge bungeni au hakimu akiwa mahakamani…
Anakua na kinga ya Asili huwezi kukamata mwalimu kwasababu ametoa mfano usioupenda au unaokuudhi..
Serikali ya kidkteta ya kidhalimu ya Samia inakamata walimu wanaofundisha wanafunzi kujua uovu wa serikali.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, ametoa wito kwa wanachama, wafuasi na wadau wa mageuzi kuongeza ushiriki wao katika kampeni ya uchangiaji wa fedha kupitia mfumo wa Tone Tone, akisema mchango wa kila mmoja ni muhimu katika kuimarisha shughuli za chama.
Amesema hayo kupitia waraka aliouchapisha katika akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Lema ameeleza kuwa kampeni hiyo imeendelea kupata mwitikio mkubwa tangu ilipozinduliwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, pamoja na kutangazwa kwa maazimio ya chama na maandalizi ya kikao kijacho cha Baraza Kuu. Ameongeza kuwa viongozi, wanachama na wananchi wameendelea kuhamasishana kuchangia ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.
Amesema anawashukuru wote waliojitokeza kuhamasisha na kuchangia, akieleza kuwa kila mchango una thamani katika safari ya chama. Hata hivyo, amesisitiza kuwa bado kuna nafasi ya kuongeza ushiriki kutokana na idadi kubwa ya wafuasi wanaodaiwa kuunga mkono chama hicho.
"CHADEMA ni Chama chenye wafuasi wengi kuliko Chama chochote cha siasa nchini."
Lema amesema wakati wa operesheni ya CHADEMA ni Msingi, chama kilikuwa na kanzidata ya wanachama zaidi ya milioni saba, huku akidai kuwa tathmini za sasa zinaonyesha wapenzi wa demokrasia, haki na mabadiliko wanafikia au hata kuzidi asilimia 65 ya Watanzania wazima.
#EastAfricaRadio #TogetherTunawakilisha
Baraza la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Tarime wakiambatana na viongozi wake wa mkoa, Wilaya na Jimbo leo July 15 wamefika nyumbani kwa makamu mwenyekiti wa chadema Bara John Heche kumpatia pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Dereva wake marehemu Suez Daniel.
Akipokea salamu za pole na John Heche ametumia wasaa huo kuwakumbusha wanachama wote nchini ajenda mbili kuu za chama chao ambazo ni "Free Tundulisu na Katiba mpya".
Kila mchango, mkubwa au mdogo, ni sehemu ya kufanikisha Baraza Kuu la CHADEMA litakalofanyika tarehe 15 Septemba 2026.
Jinsi ya Kuchangia:
M-Pesa
📱 0744 446 969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
🏦 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Changia leo. Tufanikishe Baraza Kuu la Umma.
ASANTENI WATANZANIA! MPAKA ASUBUHI HII TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 53.5 ✌️
Safari inaendelea.
CHANGIA SASA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Kwa wafuasi wote wa CHADEMA na mageuzi, wapenda haki, ukweli na demokrasia nchini.
Baada ya Katibu Mkuu wetu, John Mnyika, kutangaza maazimio ya Chama chetu, ikiwa ni pamoja na kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika siku sio nyingi , vilevile alizindua mpango maalumu wa uchangiaji wa fedha kupitia Tone Tone.
Kwa siku kadhaa sasa, kampeni hii imeendelea kwa nguvu kubwa mitandaoni, ikibebwa na viongozi wetu, wanachama, wananchi pamoja na wana harakati mbalimbali. Nawashukuru kwa dhati kabisa wote mlioamua kubeba jukumu hili; kuanzia anayehamasisha michango hadi anayetoa mchango wake. Kila mmoja wenu ni sehemu ya historia inayoandikwa.
Hata hivyo, pamoja na shukrani hizi, kuna ukweli ambao hatupaswi kuogopa kuusema. Wakati mwingine ukweli huwa ni sehemu muhimu ya kujitathmini kama taasisi na kama watu wenye maono ya pamoja.
CHADEMA ni Chama chenye wafuasi wengi kuliko Chama chochote cha siasa nchini. Wakati wa operesheni ya CHADEMA ni Msingi tulikuwa na kanzidata ya wanachama zaidi ya milioni saba. Kwa tafiti na tathmini zetu za sasa, si jambo la kupindukia kusema kuwa wapenzi wa demokrasia, haki na mabadiliko nchini wanafikia au hata kuzidi asilimia 65 ya Watanzania wazima. Kama tunakubaliana na ukweli huo, basi ni lazima tukubaliane pia na wajibu unaoambatana nao.
CHADEMA haipaswi kuwa na upungufu wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kama watu milioni moja tu wataamua kuchanga shilingi 1,000 kila mwezi, Chama chetu kitakuwa kinapata zaidi ya shilingi bilioni moja kila mwezi. Katika kampeni hii ya kuhakikisha kikao cha Baraza Kuu kinafanyika, watu laki tano pekee wakichanga shilingi 2,000 kila mmoja, tayari watakuwa wamechangia takribani shilingi bilioni moja kwa Chama chao.
Hii ina maana kuwa changamoto yetu siyo idadi ya watu, bali ni kiwango cha dhamira yetu (commitment) katika kuwekeza kwenye kile tunachokiamini. Ni lazima tujifunze kwamba mapambano ya demokrasia yana gharama zake. Haki ina gharama yake. Mageuzi yana gharama yake. Hakuna taasisi inayoweza kuwa huru kama utegemezi wake unatoka mahali pengine isipokuwa kwa watu wake wenyewe. Vyama vikubwa vya siasa duniani vimejengwa kwa michango midogo lakini ya kudumu kutoka kwa wananchi wanaoviamini. Nasi tunapaswa kujenga utamaduni huo.
Tusifanye uchangiaji kuwa jambo la misimu au la kusubiri vikao maalumu. Uchaguzi wa mwaka 2025 ulipita na Chama chetu hakikushiriki. Hivyo, hatuna ruzuku tunayoitegemea. Tunachokitegemea ni imani, mshikamano na mchango wa wananchi wenyewe. Huo ndio mtaji mkubwa wa CHADEMA.
Ni jambo lisilo na mantiki kusema tuna mamilioni ya wafuasi huku tukishindwa kukusanya fedha za kuendesha shughuli zetu za msingi. Tukitaka kuwa Chama kikubwa, imara na huru, ni lazima tukubali kubeba gharama za ukubwa huo. Tusitarajie wachache wabebe jukumu ambalo mamilioni yetu yanaweza kulifanya kwa wepesi kabisa.
Ni rai yangu kwa kila mwanachama, mfuasi na mpenda mageuzi popote alipo, afanye jukumu hili kuwa sehemu ya maisha yake ya kisiasa. Elfu moja yako inaweza kuonekana ni ndogo, lakini inapoungana na elfu moja za wengine, hujenga taasisi kubwa. Michango yetu midogo ndiyo itakayolinda uhuru wa maamuzi yetu na uimara wa Chama chetu.
Tusichangie kwa sababu tunaombwa kuchangia. Tuchangie kwa sababu tunaamini katika Tanzania yenye haki, demokrasia na utawala wa sheria. Tuchangie kwa sababu tunaamini kuwa mageuzi tunayoyatamani hayawezi kujengwa kwa maneno pekee, bali kwa kujitoa kwetu kwa vitendo.
Your small donation can make a very big change.
Nawashukuru sana kwa upendo wenu, mshikamano wenu na imani yenu katika mapambano haya. Historia ya mageuzi huandikwa na watu wanaoamua kufanya zaidi ya kushangilia. Naamini tutafanya zaidi ya tuliyoyafanya jana.
Mungu akubariki , asanteni kwa wale wote mliochanga na mnaoendelea kuchanga na ni wito wangu kwa kila mtu kujali kwa vitendo jukumu hili muhimu , tena sio mara moja bali kila wakati.
Leo amezaliwa Mh. John Heche tuungane kumtakia maisha marefu.
Happy birthday John Heche.
CHANGIA SASA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Happy birthday Makam Mwenyekiti Mhe. @HecheJohn Mungu akujalie maisha marefu yenye baraka na amani tele, Mungu akulinde dhidi ya waovu ili uendelee kuwapelekea moto madhumati.
Tuendelee kuchangia CHAMA ili kufanikisha BARAZA KUU
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
#SamiaMustGo #FreeTunduLissu #TanzaniaMassacre
Watch BBC Africa Eye: Tundu Lissu -A Story of Resilience, Survival, and the Fight for Democracy A story the world needs to hear. A story of what it means to fight for democracy, justice, political reforms, the rule of law, and the common good in East Africa-through the story of Tanzania.
For years, we have heard from Tundu Lissu himself. We have listened to his son speak in the corridors of Washington, D.C., about what it means to be the son of a man who chose freedom over silence. We have listened to the deeply moving testimony of his wife, Alicia Magabe Lissu, before the European Parliament. And now, through the BBC Africa Eye documentary, the world can hear this story through the voices of those who have lived it every single day.
But this story is bigger than one family.
It represents countless Tanzanian families whose lives have been changed by loss, fear, imprisonment, uncertainty, and the search for justice.
This is why we continue speaking.
This is why we continue advocating.
This is why justice for the many families affected by the events surrounding October 29, 2025, and those who continue to suffer, cannot be forgotten.
This is why the bipartisan bill before the United States Senate is so important. This is why continued engagement by the international community matters. Because when speaking out inside your own country can come at such a high personal cost, the world must not look away.
Even surviving an assassination attempt and enduring multiple gunshot wounds did not silence Tundu Lissu. His resilience-and the strength of Alicia and their family-should inspire all who believe in democracy, justice, and human dignity.
Please watch. Please listen. Please remember.
Unawezaje binadamu kuangalia majeraha ya Lissu, miili ya waliouwawa October 29, damu walioacha nyumbani kwa waliotekwa kama Mh.Polepole, Mdude na wengineo halafu ukakaa kimya au kujifanya nchi ina Amani? How?
Some stories are not just about one person-they become the voice of an entire nation still waiting for truth, accountability, justice, and healing.
#FREETUNDULISSU
https://t.co/avwsdd3JIa
@BBCWorld@BBCAfrica@BBCNews @BBCNewsSwahili @Reuters@AP@AFP@CNN@nytimes@washingtonpost@guardian@TheEconomist@ForeignPolicy@VOANews@StateDept@SenateForeign@HouseForeign@SenatorShaheen@SenTedCruz@RepJoeWilson@ChrisCoons@SenatorRisch@MarcoRubio@SecVetAffairs@RepMcCormick@USAmbUN@EUparliament@EP_HumanRights@USCIRF@amnesty@hrw@freedomhouse@CFR_org@AtlanticCouncil@NDI@IRIglobal@NEDemocracy
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema kuwa makala za uchunguzi zilizotolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) zimegusa sehemu ndogo sana ya ukweli wa ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala wa sheria unaoendelea nchini kwa sasa.
Kupitia tamko lake rasmi alilolitoa leo Julai 14, 2026, Wakili Mwabukusi ameishauri serikali kuacha kutumia nguvu nyingi kupingana na vyombo vya habari vya kigeni na badala yake ielekeze nguvu hizo kutatua changamoto za ndani zinazowaumiza wananchi.
"Haya mambo yote yanakiuka hata Katiba hii tuliyonayo, wala hatuhitaji kukimbizana na makala za BBC kwani zimeandika kidogo sana kuliko uhalisia," amesema Mwabukusi, akisisitiza kuwa hata kauli za Jumuia ya Madola (Commonwealth) ni ukumbusho tu wa misingi ya haki iliyoainishwa tayari kwenye Ibara ya 13 hadi 29 za Katiba ya Tanzania.
Mkuu huyo wa TLS amebainisha kuwa nchi haiwezi kukwepa ukweli wakati kuna matukio ya wazi ya utekaji na upotezwaji wa watu kama akina Soka, Mdude na Chaula, pamoja na ubaguzi wa kisheria ambapo viongozi wa upinzani kama Tundu Lissu wakikabiliwa na ukamataji wa mara kwa mara huku watu wanaounda vikundi vya kihalifu hadharani wakiachwa huru. Mwabukusi ametoa wito wa kuundwa kwa Tume ya Ukweli (Truth Commission) ili kuleta uponyaji na uwajibikaji wa dhati kitaifa.
GIRISHONI amefanya niipakue hii makala, tusikilize wote.
Wote sasa tukatazame makala ya BBC AFRICA EYE ya mwaka 2026 inaangazia mapambano ya kisiasa ya Tundu Lissu na jaribio la mauaji dhidi yake la mwaka 2017, ikionyesha juhudi zake zinazoendelea za kudai mageuzi ya mfumo wa uchaguzi nchini Tanzania licha ya kukabiliwa na mashtaka ya uhaini aliyopewa mwaka 2025.
Halafu baadae tutapata muda wa kujadili kipeperushi cha Serikali katili ya CCM kilichotolewa na GIRISHONI.
HERI YA SIKU YA KUZALIWA, MHE. @HecheJohn ✌️
Leo tunaungana na maelfu ya Watanzania kumtakia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, heri na baraka tele katika kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Katika siku hii ya kipekee, zawadi yenye thamani zaidi tunayoweza kumpatia si maneno pekee, bali ni kuendelea kuunga mkono wito wake wa kujenga chama imara kwa kuchangia kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Mhe. John Heche amekuwa mstari wa mbele akihamasisha Watanzania kushiriki katika ujenzi wa chama. Hivyo, tunawaalika wanachama, wapenzi na marafiki wa CHADEMA kuadhimisha siku hii kwa kutuma mchango wao kwa ajili ya Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334.
Zawadi bora kwa Mhe. John Heche ni kuona Watanzania wakijitokeza kwa wingi kuchangia Baraza Kuu la Umma. Kila mchango, mkubwa au mdogo, ni sehemu ya mafanikio ya chama chetu.
Heri ya kuzaliwa Mhe. John Heche! Mwenyezi Mungu akupe afya njema, hekima, nguvu na ulinzi unapoendelea kulitumikia Taifa na CHADEMA.
Hoja ya Kupinga Tamko la Serikali kuhusu Makala ya BBC Africa Eye
Na Rev Peter Simon Msigwa
Tamko la Serikali linaibua maswali muhimu kuhusu namna nchi ya kidemokrasia inavyopaswa kushughulikia tuhuma nzito zinazotolewa dhidi yake.
Kwanza, ikiwa Serikali inaamini makala hiyo ina makosa ya ukweli, njia bora si kutishia kuchukua hatua dhidi ya chombo cha habari, bali ni kujibu hoja kwa hoja na ushahidi kwa ushahidi. Ukweli hauhitaji kulindwa kwa vitisho; unahitaji kuthibitishwa kwa vielelezo vinavyoweza kuchunguzwa na umma.
Pili, Serikali inasema BBC haikutoa nafasi ya kutosha kwa upande wake kujibu. Ikiwa hilo ni kweli, basi Serikali ina haki ya kueleza ni lini iliombwa maoni, ni maelezo gani iliyatoa, na ni sehemu zipi ambazo haikuridhika nazo. Hata hivyo, hoja hiyo pekee haiondoi wajibu wa kujibu tuhuma zilizomo kwenye makala yenyewe.
Tatu, kauli kwamba Serikali “itachukua hatua za kulinda heshima ya nchi dhidi ya mashambulizi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii” inaweza kutafsiriwa kama ishara ya kutishia uhuru wa vyombo vya habari. Heshima ya taifa hailindwi kwa kuzuia uchunguzi wa waandishi wa habari; inalindwa kwa kuhakikisha taasisi za dola zinawajibika, sheria zinaheshimiwa, na madai yoyote yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu yanachunguzwa kwa uwazi.
Nne, Serikali imeelekeza nguvu nyingi katika kuhoji BBC kuliko kujibu tuhuma zilizowasilishwa. Wananchi wanahitaji majibu kuhusu madai yaliyotolewa, si mjadala kuhusu nani aliyaripoti. Kinachopaswa kujadiliwa ni ukweli wa yaliyomo kwenye makala, si utambulisho wa mtoa taarifa.
Tano, katika demokrasia zilizo imara, uchunguzi wa vyombo vya habari hauchukuliwi kama shambulio dhidi ya taifa bali kama fursa ya kuboresha uwajibikaji. Serikali yenye kujiamini hujibu kwa uwazi, huruhusu uchunguzi huru, na ikiwa madai si ya kweli, ushahidi huonyesha hivyo.
Watanzania wana haki ya kupata taarifa kutoka pande zote. Vivyo hivyo, Serikali ina haki ya kujibu. Lakini haki ya Serikali kujibu haiwezi kuwa sababu ya kuzuia au kutisha vyombo vya habari vinavyoibua maswali kuhusu maslahi ya umma.
Mwisho, heshima ya Tanzania duniani haitajengwa kwa kupinga kila taarifa ya uchunguzi. Itajengwa kwa kuonyesha kwamba nchi ina taasisi zinazoweza kuchunguza madai kwa uhuru, kuwawajibisha wanaokosea bila kujali nyadhifa zao, na kulinda haki za wananchi pamoja na uhuru wa vyombo vya habari. Huo ndio msingi wa taifa lenye nguvu na linaloaminika kimataifa.
ASANTENI WATANZANIA!
MPAKA ASUBUHI HII TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 30.2 ✌️
Asanteni kwa mwitikio wenu mkubwa na moyo wa kujitolea. Mpaka asubuhi hii, Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334 imefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 30.2 kwa ajili ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Kasi hii inaonyesha jambo moja kubwa tukisimama pamoja, tunaweza. Tunawashukuru wanachama, wapenzi na Watanzania wote ambao mmeendelea kuweka nadhiri zenu na kuchangia kwa kadri ya uwezo wenu.
Bado safari inaendelea. Tunawaomba Watanzania wote kuendelea kushiriki katika kampeni hii kwa kuchangia na kuwahamasisha wengine kufanya hivyo. Kwa umoja wetu, lengo la TSh. Milioni 334 linawezekana.
@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
Samia baada ya kuua watu October 2025 aliambiwa na wananchi #SamiaMustGo
Watu wake wakaanza matusi na utekaji ukashamili kwa kasi
Ufisadi ukakomaa
Polisi wakaendelea na ushenzi
Leo Zungu ametumwa kuzunguka anasema Ukweli na Maridhiano
Ukweli = wajibikeni, Polisi acheni kuteka, Ufisadi ukome, mauaji hapana, onyesheni miili mmezika wapi, Samia Must Go, Jeshi la Polisi lifutwe tujenge jipya , uchaguzi ni batili , Free Tundu Lissu na wote waliotekwa
Tukimaliza kwenye ukweli, Maridhiano ni simple tu , tupate katiba mpya yenye Tanganyika kama yenye serikali kamili , kesi mahakamani za ufisadi na waharifu wote , uchaguzi mpya