Nyumbani tumezoea fujo —fimbo, makofi, matusi kama njia ya wazazi kulinda mamlaka yao. Hakuna mazungumzo yenye upendo na mtoto. Tunaamini amani kwenye familia ni pale unapokuwa na watoto wasiofikiri, wasiouliza, wasiothubutu kutofautiana na wazazi ambao ndio mamlaka katika familia.
Shuleni anakuja mwalimu anayeamini njia pekee na ya uhakika kulinda heshima na mamlaka yake darasani ni vitisho, fimbo na ubabe kwa mwanafunzi. Hata ufundishaji wake hauamini katika ushirikishwaji wa mwanafunzi—tangu asubuhi mpaka jioni ni zoezi la wanafunzi kupokea maelekezo na kuyakariri. Mwalimu anaamini nidhamu ni amani inapotawala darasani na ndio maana shule zinahangaika na wapiga kelele kuliko kuchochea udadisi.
Ukienda kazini hali haiko tofauti. Unakutana na msimamizi asiyeamini mazungumzo ya wazi. Kazi ya mfanyakazi ni kusikiliza, kufuata na kutekeleza. Huwezi kuwa mbunifu ukaeleweka kirahisi. Huwezi kuuliza maswali ukaeleweka. Hata vikao, kimsingi, ni matangazo yanayohitaji utekelezaji. Nidhamu ya kazi inatafsirika kama uwezo wa kutambua uwezo usio wa kawaida alionao kiongozi.
Unaingia kwenye ndoa unakutana na mazingira yanayolinda mamlaka ya mume kwa vitisho, ubabe na unyanyasaji. Mume hasemi wazi lakini kimsingi haamini kabisa uwezekano wa kupanga jambo la maana na mke wake kwa usawa na likaenda. Usiri na giza hugubika mfumo wa maisha yake na muda wote anaamini ni muhimu kukoroma, kutisha na kunyamazisha sauti kinzani.
Ukiangalia unaona tunavyoamini katika matumizi ya nguvu, vitisho na kuogopesha. Tunaamini madaraka hulindwa kwa ubabe na kuwafanyia fujo watu ambao wakati mwingine kwa unyonge wao hawana wanachoweza kufanya zaidi ya kuhitaji kusikika. Sisi hawa hawa tunaoamini katika kuumizana na kutunishiana misuli tunatarajia siasa za kiungwana, kistaarabu, zinazoendeshwa na watu wapole, waelewa wenye utu wanaoamini katika mazungumzo yenye usawa.
“KAMA UNASOMA UJUMBE HUU, INA MAANA UKO HAI,HIYO NI ISHARA TOSHA KUWA MUNGU ANA MAKUSUDI NA WEWE.
ANAYEKUPINGA SIYE ALIYEKUUMBA, BALI MUNGU PEKE YAKE NDIYE ANAYEJUA HATIMA YAKO.
MUAMINI MUNGU NA WEKA TUMAINI LAKO KWAKE TU
ATAKUPA HEKIMA YA JINSI YA KUVUKA MTO ULIO MBELE YAKO.”
@Sirjeff_D ROHO siyo kiungo katika mwili wa mwanadamu.
Roho ina maana tatu tofauti na kila moja hutumika kutokana na mandhari husika.
1. Roho, ikiwa na maana mtu.
2. Roho, ikiwa na maana ya pumzi ya uhai.
3. Roho, ikiwa na maana ya tabia/wazo nzuri au mbaya.
@Haloteltz usiku mmenigomea kujiunga dakika. Sikufanya mawasiliano kabisa Saivi najiunga naambiwa sina Salio la kutosha, zaidi ya shilingi 500 imekatwa naomba ufafanuzi maana sina kumbukumbu za kudaiwa.
@Haloteltz ni muda sasa nimekwama kufanya mawasiliano ya muhimu sana kutokana na maboresho yenu kwenye mfumo nashindwa kujiunga kifurushig cha maongezi. Hamkutoa taarifa na sina namba mbadala mitandao mingine 😡
@Enemy_19 Enemy umefanya uamuzi madhubuti, usitikiswe na mawazo kinzani.
Hii kauli ya "hana shida na ombaomba wa mtandaoni" haiakisi moyo wa kutoa kwa wahitaji. Akajifunze kwa mtumishi wa Mungu Thabita. Hii alikusudia iwe fimbo ya kukuchapia.
@HowIWish5@JamiiForums Usipotoshe watu. Hiyo siyo cash, ni ahadi tu. Itatolewa pale mshitakiwa atakaporuka dhamana (kushindwa kudhuria mahakamani bila taarifa au ruhusa ya Mahakama/kukimbia/kutoroka na kutokomea kusikojulikana).
@tanescoyetutz Bila shaka ilipaswa kuwa 4000 na sio 6000 naomba kujua hilo ongezeko la 2000 iliyokatwa ni la nini?
Pia naomba ufafanuzi wa hiyo sms ya tokeni 3 inayosema mita ina maboresho. Ni maboresho yapi?