"Hivyo katika miezi 3 ya Aprili, Mei na Juni 2026 inakadiriwa taifa letu limepata hasara ya Tsh. Trilioni 2.16 ambapo Tsh trilioni 1.5 upandishaji holela wa bei za mafuta, Tsh Bilioni 501.67 malipo ya ziada ya Kampuni ya Vitol na Bilioni 161.98 malipo hewa ya ruzuku katika kashfa ya uagizaji wa mafuta nchini. Kiasi ambacho ni kikubwa zaidi ya kiwango cha Tsh. Bilioni 700 tulichokadiria awali."
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa @ACTwazalendo
Luhaga Mpina
#KashfaYaMafuta
UZI
KASHFA YA MAFUTA YA TPDC NA VITOL
Serikali ya Tanzania ilibadili mfumo wa uagizaji wa mafuta wa pamoja kwa utaratibu wa ushindani na kuanza kutumia zaidi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (Tanzania Petroleum Development Corporation_TPDC) katika uagizaji wa mafuta kwa madai ya kupunguza gharama na kuleta utulivu wa bei ya nishati nchini kwa miezi mitatu kwa maana Mei, Juni na Julai, 2026. Licha ya kutumia Shirika la Serikali lakini bei za mafuta ya Petroli na Dizeli haikushuka.
Naibu Waziri Mkuu Kivuli
Luhaga Mpina
#KashfaYaMafuta
"Bajeti ya 2026 imeongeza mzigo wa kodi, ushuru na tozo kwa wananchi, hususan wanyonge, huku ikiendelea kutenga sehemu kubwa ya fedha za umma kugharamia matumizi yasiyo ya kipaumbele, yakiwemo anasa za viongozi, safari, posho nk."
Naibu Waziri Mkuu Kivuli
Luhaga Mpina
#KashfaYaMafuta
"Mkataba wa Bwawa la Nyerere ulilenga kutumia Tsh. Trilioni 6.5 badala yake umetumia Tsh. Trilioni 7.44 sawa na ongezeko la Shilingi Bilioni 940."
Naibu Waziri Mkuu Kivuli
Luhaga Mpina
#NaSasa2026Tena#UchambuziWaBajeti
Leo Juni 23, 2026 KC @SemuDorothy akiwa na Naibu Waziri Mkuu Kivuli, Luhaga Mpina na Waziri Kivuli wa Elimu, Ndugu @rizikishahari; wamechambua Bajeti Kuu ya Serikali na kuonyesha jinsi Serikali inavyoendelea kuwakandamiza wanyonge kwa mzigo wa tozo na kodi.
#NaSasa2026Tena #UchambuziWaBajeti @ACTwazalendo
"Huwezi kuahidi afya kwa wote ndani ya siku 100 halafu miezi kadhaa baadaye wananchi waendelee kukosa bima, dawa, madaktari na huduma bora za afya. Huu ni ushahidi wa ahadi hewa na sarakasi za kisiasa."
Kiongozi wa @ACTwazalendo@SemuDorothy#NaSasa2026Tena#UchambuziWaBajeti
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameonesha wazi kuwa Serikali ilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 207 kupitia tozo ya shilingi 10 kwa kila lita ya mafuta kwa malengo ya kuimarisha Miundombinu ya miradi ya maji . Hata hivyo, ripoti hiyo hiyo inaonesha kuwa shilingi bilioni 94 ziliondolewa na kutumika nje ya utaratibu uliowekwa na sheria na bila kufuata matakwa ya Katiba.
Leo mnapojitokeza mbele ya wananchi mkijifanya kusikitishwa na hali inayowakabili, ni lazima mjibu kwanza maswali kuhusu matumizi ya fedha hizi za umma. Wananchi wanateseka kutokana na uhaba wa huduma na miradi iliyopaswa kugharimiwa na fedha hizo, huku hakuna uwajibikaji wa kutosha kwa waliohusika.
Badala ya kutoa matamko ya kisiasa yasiyoleta suluhisho, ni wakati wa kuwajibika kwa matendo yenu. Fedha za umma si mali ya viongozi wala familia zao; ni jasho la wananchi. Nchi haiwezi kujengwa kwa maneno matamu huku rasilimali zake zikihujumiwa. Watanzania wanahitaji uwazi, uwajibikaji na hatua madhubuti dhidi ya wote waliohusika na ubadhirifu wa fedha za umma. @mwigulunchemba1 ,@TheChanzo ,@MwananchiNews ,
Uzi
Leo Juni 12, 2026 Kiongozi wa @ACTwazalendo, Ndugu @SemuDorothy ameongoza kikao cha @ACTBarazaKivuli Jijini Dar es salaam.
Pamoja na mambo mengine, mawaziri vuvuli wamekabidhiwa rasmi majukumu yao "Instruments" na kupitia Bajeti Kuu za Serikali ili kutoka na uchambuzi wake.
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Leo KC @SemuDorothy amewakabidhi rasmi majukumu yao Waziri Kivuli wa Uchukuzi, Ujenzi na Miundombinu, @MtuturaAbdallah; Waziri Kivuli Kilimo, Bazililo Mbwilo; Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Ndugu Rashidi Ali na Naibu Waziri Kivuli TAMISEMI, Ndugu Bakari Shingo.
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Leo KC @SemuDorothy amewakabidhi rasmi majukumu yao Naibu Waziri Kivuli wa Utumishi na Utawala Bora, Samson Chacha; Naibu Waziri Kivuli Elimu, Said Ibrahim; Waziri Kivuli wa Kilimo, Ndugu @ruhasha2 na Naibu Waziri Kivuli Mambo ya Ndani, Ndugu Hussein Kalyango.
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Naibu Waziri Kivuli wa Kilimo, Umwagiliaji na Maendeleo ya Ushirika wa @ACTwazalendo, Frank Ruhasha anashiriki kikao cha Baraza Kivuli kinachoendelea Jijini Dar es salaam.
#TaifaLaWote#MaslahiYaWote