@Shasilanabipa Kwa mahakama hizi za simu moja na matakwa ya jamuhuri huwezi kumpima. Ingekuwa mahakama za kimataifa wangalau. Jambo ambalo nadhani hawezi.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 302
Majaji wanaingia.
Ajuaye anasema wako tayari kuendelea wao upande wa Jamhuri.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mh. Lissu nae anasema yuko tayari kuendelea. Na shahidi wake anaitwa JOHN JOHN MNYIKA.
Katibu Mkuu Mhe. John Mnyika anaitwa na anapanda kizimbani amevaa Shati nyekundu ya Chama.
Anafuatwa na Karani wa Mahakama wanateta na Mnyika anacheka.
Jaji: unaitwa nani?
Mnyika: John John Mnyika,
Jaji: umri wako?
Mnyika: Miaka 46
Jaji: Kazi yako
Mnyika: Katibu Mkuu wa Chadema.
Jaji: Dini yako?
Mnyika: Mkristu
Jaji: haya muapishe.
Mimi John John Mnyika naapa ushahidi nitakaotoa utakuwa wa kweli, ukweli mtupu na Mungu anisaidie.
Sasa Mhe. Lissu anaanza.
Mhe. Lissu: Nitakayokuuliza uyajibu kwa utaratibu maana Majaji wanaaandika na mimi nafahamu una sauti nzuri tu.
Sasa waeleze majaji umeshikilia nafasi hii ya Chadema kuanzia lini?
Mnyika JJ: Kuanzia 2019 mimi ni Katibu Mkuu.
Mhe. Lissu: Kabla ya hapo ulikuwa na nafasi yoyote nyingine?
Mnyika JJ: Kabla ya KM nilikuwa Mkurugenzi wa Vijana Chadema Taifa kuanzia 2003 hadi 2011 wakati naishikilia nafasi hiyo mwaka 2007 niliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa habari na uenezi hivyo nilishikilia nafasi mbili kwa wakati mmoja. Nafasi ambayo niliitumikia mwaka 2014.
Na wakati huo huo kati ya mwaka 2009 hadi 2011 nilishikilia nafasi ya Mkurugenzi wa mambo ya nje na uhusiano wa Kimataifa wa CHADEMA.
Na Mwaka 2014 niliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa nafasi ambayo niliishikilia hadi 2019 nilipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu.
Nilipokuwa mbunge pia
Mhe. Lissu: Huko tutakwenda pia bado subiri. Nafasi nyingine je?
Mnyika: Nilikuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Kinondoni kwa vipindi viwili.
Mhe. Lissu: Nafasi nyingine?
Mnyika JJ: Nilikuwa Katibu wa Wabunge wa Chadema Bungeni kati ya mwaka 2010 mpaka 2015 na nikawa tena Katibu kuanzia mwaka 2016.
Jaji ulikuwa mbunge wa?
Mnyika: Nilikuwa Mbunge wa jimbo la Ubungo 2010 hadi 2015 na baadae Jimbo la Kibamba 2015 hadi 2020.
Mhe. Lissu: Nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema ni nafasi ya aina gani katika uongozi wa Chama.
Mnyika: Ni nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Chama ambae ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Chama na ni msimamizi mkuu wa rasilimali, utawala, uendeshaji wa Chama. Na Katibu Mkuu ndie msimamizi mkuu wa utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya vikao vya juu vya Chama ambavyo ni Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Chama.
Mhe. Lissu: Taratibu tararibu.
Mnyika anapeleka moto kwa kasi ๐
Vilevile ni msimamizi mkuu wa wafanyakazi wa Chama na waliopo makao makuu ya Chama ikiwemo pia makatibu wote wa Chama.
Mhe. Lissu: Sasa nisubiri mimi.
Eheee Sasa shahidi naomba waeleze Majaji kama Chama Chako huwa kinafanya vikao au mikutano ya Chama na utaratibu wake ukoje?
Mnyika: Chama huwa kina mikutano ya aina mbili kuu ambazo ni Mikutano ya ndani.
Usiposikia Jaji amesema Mhhhhhhh ndo uendeleee.
Mnyika: Kuna Mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani.
Jaji Ndunguru : Sio lazima niseme mhhhhhh naweza sema endelea.
๐๐๐๐ kicheko.
Mnyika: Kwa mikutano ya ndani ngazi ya utendaji chombo husika ambacho ni sekretarieti kinakaaa kikao cha ngazi ya Kitaifa chini ya Katibu Mkuu na kufanya maandalizi ya kikao hicho. Na majukumu yanagawanywa ya maandalizi yake.
Mhe.Lissu: Hapohapo. Subiri. Sasa waeleze majaji nani ni wajumbe wa hiyo sekretarieti?
Mnyika: Ni Katibu Mkuu wa Chama Taifa ambae ndie Mwenyekiti wa Sekretarieti. Manaibu Katibu wakuu wawili. Mmoja wa Zanzibar na Mwingine wa Bara, Wakurugenzi wa Kurugenzi za Chama Taifa, Wataalamu na Katibu wa Sekretarieti anayeteuliwa na Katibu Mkuu na Makatibu wa Mabaraza ya Chama kwa maana ya Baraza la Wazee, Baraza la Vijana na Wanawake. Anataja na vifupi vyake BAZECHA, BAWACHA na BAVICHA.
Part 303 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 301
Mhe. Lissu anaendelea na Re-examination
Mhe. Lissu: Kuhusu D1 kile kielelezo cha Kaaya kule chini kabisa kimeendikwa maelezo, ziko hizo sehemu kwahiyo alipaswa kuandika na kuandikwa maelezo.
D2 nacho pia hicho kielelezo Samwel Elibariki nacho niliulizwa maswali kadhaa angalia mwisho utaona. Ipo sehemu ya mtoa maelezo na afisa aliyeandika maelezo, hizo sehemu zote zimesainiwa na mtu mmoja.
D5 ambayo ni maelezo ya PW 6 nayo pia kuna signature moja imepita sehemu zote za aliyeandika maelezo na aliyemuandika maelezo kote ni yule yule.
Exhibit D8 ni maelezo ya PW9 nae pia vilevile. Kuna uthibitisho wa Afisa aliyeandikiwa maelezo. Uthibitisho pia wa chini yake ameandika vile vile yeye pia. Amejionya na kujithibitisha mara mbili.
D11 maelezo ya PW12 inasema Koplo Vicent nae pia alijionya na kujiandika Maelezo yake. Mtu huyo huyo.
D15 ambayo ni maelezo ya Amin Mahamba PW 16 kila page kuna mtoa maelezo na aliyeandika maelezo. Lakini imesainiwa mtoa maelezo pekee lakini aliyeandika maelezo haipo kabisa.
D14 cha PW 15 Koplo Amani kwenye kila page saini ya mtoa maelezo imejazwa na afisa aliyesimamia maelezo ipo Koplo Robert. Ndo nilisema huyu pekee ndio alifuata utaratibu. Detective Corporal Robert ndio niliandika maelezo ya Detective Coporal Amani. Huyu alikuwa sahihi.
Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu wale mashahidi waliokiri kufanya uhalifu. Walikiri Polisi na baadae wakaambiwa wawe mashahidi dhidi yangu na baadae tuhuma zikafutwa. Je unawaita wahalifu walishapelekwa mahakamani hapana lakini ni wahalifu. Ufafanuzi ni kwamba watu ambao ni wamepanga kufanya uhalifu, wakakamatwa kwa kufanya uhalifu, wakakiri wanapanga kufanya uhalifu wakaja mahakamani tumepanga kufanya uhalifu na wakaachiliwa hao ni wahalifu.
Ajuaye: Ameanza kutoa ushahidi hapa tena.
Mhe, Lissu: Nimetoa ufafanuzi Jaji
Jaji Ndunguru: Haya tuendelee hebu
๐๐ Ni kama Jaji amesema bila kusema kuwa AJUAYE WEWE NI KILAZA. Kwa Maneno Mengine Jaji anasema AJUAYE NI KATUGA ambae hana maelezo mengi lakini ujinga ni ule ule.
Mhe. Lissu: Naomba niishie hapo. Kwenye hii re examination.
Kesi imeahirishwa hadi saa nane kamili tutarudi Mahakamani.
Kuendelea na Shahidi John Mnyika. DW2.
Naomba Repost yako.
@TanzaniaAnalyst Vilaza mnapongezana๐คฃ Kwenye kesi ya Lisu ndio imedhihirika kile alichosema Prof. Asad kuwa huko serekalini 60% hawana uwezo kabisa, na 20 wana afadhali, na 20% ndio wanafaa. Hawa mawakili wa Gov wako hilo kundi la 60%. Ndio maana serekali huwa haishindi kesi yoyote nje.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 297
Ajuaye: Ulitoa taarifa sasa wewe polisi?
Mhe. Lissu: Ilikuwa ni miezi sita kabla ya uchaguzi. Natoaje taarifa polisi wakati siku kwenye mkutano wa kampeni na nilishakwambia sikuwa nafanya public meeting.
Ajuaye: Soma kifungu cha 23 cha Political parties act
Mhe. Lissu: Soma wewe uliza swali.
Ajuaye: anakisoma je ulitoa taarifa
Mhe. Lissu: Siwezi kutoa taarifa mikutano ya ndani. NEXT?
Ajuaye: Kifungu kinasema public place or any other area
Mhe. Lissu: Hujui wewe hata kusoma kingereza kifungu kinasema public meeting conducted at any area. Sasa wewe umesoma shule gani Dada angu?
Ajuaye: Tulia kwanza. Una kifungu chochote kinachosema unaweza kufanya mkutano wa ndani bila kibali?
Mhe. Lissu: Hicho hicho kifungu cha 23 cha Sheria ya Vyama vya siasa.
Ajuaye: Maneno ya kukinukisha uliyakubali hata kama video hatujaleta?
Mhe. Lissu: Sikuongea maneno ya Uhaini mimi.
Ajuaye: Ni ukweli kwamba hata kama video haikuletwa lakini uliongea maneno ambayo yapo kwenye hati ya mashitaka?
Mhe. Lissu: Maneno niliyoshitakiwa kwamba yalikuwepo kwenye video yalikuwa ya masaa matatu hayakuwa ya uhaini.
Ajuaye: Video ni kifaa kilichobeba maandishi?
Mhe. Lissu: Kumbe iko hivyo? Mimi sijui.
Ajuaye: subiri nikiwa mshitakiwa au shahidi utaniuliza. Nitakuomba uwe Wakili wangu?
Mhe. Lissu: Siwezi kuwa na mteja kama wewe ambae anasingizia singizia watu makosa.
Ajuaye: ni kweli mahakama ndio inaweza kusema mtu fulani amefanya kosa fulani?
Mhe. Lissu: Itasema kama mtu huyu atakuwa amepelekwa mahakamani.
Ajuaye: Nani anasema walikamatwa kwasababu walikuwa na makosa?
Mhe, Lissu: Walikamatwa bila kuwa na makosa.
Ajuaye: Ulisema kama ukamataji wako ulikosewa?
Mhe. Lissu: Nilisema na Kiswaga aligoma kuandika na hapa nilisema kwenye mahakama hii.
Ajuaye: Ni very serious allegation hizo
Mhe. Lissu: Ndio ndio maana nilileta mahakamani na wewe ulikuwepo siku ile. Uliona.
Ajuaye: Wanaosimamia sheria ya uchaguzi ni serikali?
Mhe. Lissu: Sheria ya Uchaguzi inasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Na tume ya Uchaguzi sio Serikali.
NB. Leo nimeshuhudia ni kwa kiwango gani TAIFA lina Mawakili wa Serikali ni VILAZA.
Ajuaye: Kupinga uchaguzi ni takwa la kisheria?
Mhe. Lissu: Sisi tulikuwa tunataka uchaguzi usifanyike kabisa. Mambo ya kupinga hata kwenye uchaguzi halali kuna kupinga matokeo ya uchaguzi.
Anakuja askari wa Magereza huwa ni mnaa mnaa sana. Mnoko sana. Amewafuata mawakili wa serikali kwasababu imefika saa 11 na nusu kwa sasa.
Wanajadili mawakili wa Serikali muda huu.
Mhe. Lissu: Ule utaratibu wa kuishia saa 11 kamili vipi tumeubadilisha.
Jaji Ndunguru: Tulidhani wanamaliza maswali yao ndio maana tukawa tunawaangalia tu. Sasa ngoja tuwaulize. Upande wa serikali mnasemaje?
Ajuaye: Basi tuahirishe hadi kesho.
Jaji Ndunguru anateta na wenzake.
Sasa tukutane kesho asubuhi kuendelea.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 296
Wakili wa Serikali Job Mrema: Kama kuna mgogoro si unatakiwa kwenda Mahakamani?
Mhe. Lissu: Ukiwa ni mgogoro wa kiimani unaenda kanisani na msikitini kutatua. Yakisheria ndio unaenda Mahakamani.
Job Mrema: Unakubaliana na mimi kuwa ulisema majaji hawatendi haki?
Mhe. Lissu: Hilo sio geni amelisema jaji Nyalali, Tume ya Warioba imesema. Hata na kikosi kazi pia kimesema. Hakuna jipya hapo.
Job Mrema: Ulisema Majaji ni Ma CCM na Huko Mahakamani hakuendeki?
Mhe. Lissu: Ndio.
Job Mrema: Kupandikiza wananchi chuki katika mfumo wa utoaji haki ni kosa? This is general question.
Mhe. Lissu: hiyo chuki maana yake nini sasa? Niambie kwanza.
Job Mrema: Kifungu cha 52 cha Media service Act. Kinasemaje na unakionaje?
Mhe. Lissu: Kama ukisababisha chuki, dharau au kutokuridhika na mfumo wa utoaji haki ni nia ya kichochezi.
Job Mrema: ukiwa na nia unakiuka kifungu hicho
Mhe. Lissu: Kwa maana ya kifungu cha 52(2) hukiuki lakini 51(1) C ni sawa.
Job Mrema: Kuhusu Majaji ni ma ccm na mahakamani hakuendeki hiyo statement inakiuka kifungu cha 52(1)
Mhe. Lissu: Sikubaliani na wewe kabisa.
Job Mrema: Kulikuwa na amri ya kuficha mashahidi?
Mhe. Lissu: Ndio
Job Mrema: Hukuchukua hatua.
Mhe. Lissu: Niko gerezani unataka nichukue hatua gani?
Job Mrema: Unawakumbuka mashahidi wa siri?
Mhe. Lissu: Nawakumbukaje wakati nimekwambia siwafahamu? Unawafahamu wewe. Majaji na mimi.
Job Mrema: Ni sahihi kwamba uamuzi wa mashahidi wa vificho hauwezi kuzungumziwa kwenye kesi hii?
Mhe. Lissu: ingekuwa haiwezekani hivyo vizimba hapo visingefumuliwa kipindi kile. Kwani nilipinga kwenye kesi gani ya Bibi yako?
Jaji: Haya tuendelee swali lingine.
Job Mrema: Mheshimiwa tunaendelea.
Jaji Ndunguru: Sasa nyie si mpo wengi hapo Mawakili wa Serikali mwingine aingie haraka aanze kuuliza wakati huyu anatafuta maswali yake.
Watu wanacheka๐๐
Job Mrema: Uliwasilisha chochote kuhusu kupigwa Tar. 11/08/2024 kule Mbeya?
Mhe. Lissu: Nimesema kwa mdomo na ndio maana niliapa kabla ya kutoa ushahidi.
Job mrema: Tar. 23/09/2024 ulivamiwa nyumbani kwako na polisi na hakuna ushahidi wowote ulioleta?
Mhe. Lissu: Nilisema nivamiwa na kukamatwa wakanipeleka mbweni na usiku walinirudisha nyumbani. Ulitaka nilete nini kwenye hayo maneno?
Job Mrema: Ulisema watu 466 ulisema case no zao wale wa Tarime.
Mhe. Lissu: Sikueleza.
Job Mrema: PW1 ulisema alifungua jalada tarehe 04 April
Mhe. Lissu: Nilivyosema mimi au PW 1 mwenyewe ndio alisema.
Job Mrema: PW 1 Kwahiyo umesema ilikuwa ni lazima amwambie DPP kuhusu mashitaka haya?
Mhe. Lissu: Soma kifungu cha 16 na 24 cha National Prosecution Act kinasema makosa ya jinai ni DPP ndio anapaswa ku coordinate ushahidi. Sasa yeye hakufanya hivyo. Hakuwahi kumpa taarifa na alisema hivyo.
Job Mrema: Ni chombo kipi kimepewa mamlaka ya huyu ana hatia na huyu hana hatia?
Mhe. Lissu: Ilikuwaje nyie polisi mseme huyu ni mkosaji wa uhaini hata kabla ya ushauri wa DPP?
Job Mrema: Sasa kama mashitaka yalikosewa unafanya nini?
Mhe. Lissu: Najitetea kwa makosa ya kubambikizwa.
Job Mrema: Mahakama hii imetoa uamuzi kuhusiana na makosa yako?
Mhe. Lissu: Haijatoa.
Job Mrema. Amerudi kwa wenzake wanaongea kama dakika tano hivi. Jaji Ndunguru anawaangalia kwa hasira sana.
Anasimama anasema naomba kuishia hapa nimkaribishe Ajuaye Zengeli.
Ajuaye: Ni sahihi kwamba wakati mnafanya mkutano huo hamkuwa na kibali chochote?
Mhe, Lissu: Hakuna mkutano wa ndani unahitaji kibali. Pia hakuna mkutano wowote wa vyama vya siasa unahitaji kibali unatakiwa kutoa taarifa tu.
Ameingia kilaza mwingine huyu Ajuaye.๐ฎ
Ajuaye: PGO 403
Mhe. Lissu: Soma wewe inasemaje nikujibu swali.
Ajuaye: Basi soma PGO 402
Mhe. Lissu: Inahusu mikutano ya kampeni
Watu wanacheka๐
Ajuaye: Umekielewaje?
Mhe. Lissu: Mambo ya uchaguzi na taratibu za kampeni za uchaguzi
Part 297 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 294
Mwenyekiti ameingia tayari baada ya kumaliza kuongea na mawakili wake na break pia kwa ajili ya Chakula cha Mchana.
Alipata nusu saa pia ya kukaa na Mawakili wake na mashahidi wake wengine. Mh. Heche, Mnyika, Amani na Brenda walikuwepo nae.
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa uko tayari tuendelee.
Mhe. Lissu: Niko tayari.
Katuga: Mh. Jaji naomba Exhibit D15. Makarani wanaitafuta. Ni maelezo ya PW 16. Ulisema wapelelezi hawakukuuliza maana ya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka?
Mhe. Lissu: Ndio
Katuga: PW 1 alisema alikuhoji kuhusu maana ya maneno yako?
Mhe. Lissu: Hakunihoji hilo.
Katuga: PW 1 alisema alikupa nafasi kuhusiana na haya maneno kwanini yasiwe ya uhaini?
Mhe. Lissu: Nilimjibu mmeshanikamata na mmeshanishitaki tutakutana mahakamani ndio nilimjibu.
Katuga: PW 1 alikupa nafasi au hakukupa nafasi?
Mhe. Lissu: Alishanishtaki kwa uhaini.
Katuga: Ulizuiwa nini ulipoambiwa utoe maelezo yako?
Mhe. Lissu: Tutakutana mahakamani
Katuga: Ndio maana hukutaka kutoa maana ya maneno?
Mhe. Lissu: Sikuulizwa kuhusu maneno alisema kuhusu uhaini, nikamwambia twende mahakamani.
Katuga: Ungeweza kutoa maana ya maneno au usingeweza pale angekuuliza?
Mhe. Lissu: Sasa halikuulizwa hilo nitoleee nini? Ningejibu angeniambia.
Katuga: Ulirejea Maelezo D15 ni maneno ambayo umeyaamini na yapo kwenye kielelezo chako?
Mhe. Lissu: Maneno yapi? Unauliza mambo jumla jumla. Eleweka.
Katuga: Baada ya kuunda timu mimi na timu tulisikia
Mhe. Lissu: Tulisikiliza sio tulisikia soma vizuri wewe
Katuga: Nina miwani siku hizi sioni vizuri.
Mhe. Lissu: Ukiwa na miwani ndio unasoma vizuri acha uongo.
Katuga: Yangu ni ya bei halisi
Lissu: Sasa unalipwa nini? Au unajitutumua bure tu hapa?
Katuga: Je haya maneno nimesoma ulirejea?
Mhe. Lissu: In relation na ushahidi wa PW1 ndio niliyarejea. Kuhusianisha na PW 16 alichosema.
Katuga: Kwahiyo ulikiamini kielelezo?
Mhe. Lissu: Nilikiamini kivipi? Nilikitumia kuonesha utofauti wa mashahidi wawili wa Jamhuri.
Katuga: Kwahiyo ulikiamini?
Mhe. Lissu: Mimi niwaamini Mapolisi hawa? Nilikitumia kuonesha utofauti wa mashahidi wawili wa Jamhuri.
Katuga: Sasa nijibu unayaamini yaliyomo humo?
Mhe. Lissu: Niamini nini?
Katuga: Uko sawa kweli?
Mhe. Lissu: Wee unanionaje?
Katuga: Naona uko sawa.
Mhe. Lissu: Sasa unaniuliza nini kama unasema niko sawa?
Jaji: Sasa wakili toka hapo. Tumeshapata majibu.
Katuga: Ulisema haya maelezo yote kuanzia D1 hadi D16 ulitaka yatumike kwa ajili yako?
Mhe. Lissu: Nilishajibu toka zamani. Kwa ajili ya kuonesha utofauti wa ushahidi. Contradiction ya ushahidi na ommission zilizofanyika.
Katuga: Kuna sehemu ulisema mahakama i exclude baadhi ya maneno yaliyopo humu?
Mhe. Lissu: Hiyo ni kazi ya submission.
Katuga: Narudia tena ulisema au hukusema?
Mhe. Lissu: Nimekwambia hiyo ni kazi ya submission.
Jaji Ndunguru: jibu tu swali shahidi umeiambia mahakama au hujaiambia.
Mhe. Lissu: Narudia tena nitawaambia wakati wa final submission nimemaliza.
Jaji Ndunguru: Haya sasa wakili wa serikali endelea mbele. Jibu ndio limeshatoka hilo na halitabadilika.
Kicheko kutoka kwa umma ๐๐๐
Katuga: Mheshimiwa Jaji naomba nirudishe kielelezo.
Anaendelea kupekua makaratasi yake. Kamaliza maswali ila anatupotezea muda tu hana lolote mshenzi huyu.
Part 295 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
@Baradhuli2 Wakati Mbowe akiwa mwenyekiti ilikuwa cdm ni Saccos ya wachaga, Nkurunzinza na upuuzi wa aina hiyo. Leo ule upuuzi ule umefikia mwisho chawa mnajifanya kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Bado hamjatoa milio wasenge wakubwa nyie.
Haiwezekani familia chungu nzima zina majonzi mmeuwa ndugu zao, miili haionekani, wamezika ktk makaburi ya halaiki, maelfu wako jela, Watz wamepigwa ban wasitoke ndani siku 5 bila mawasiliano, alafu mnaapishana kwenye karakana ya jeshi, mkitegemea muwatawale hao watu. Mna wazimu!
@TanzaniaAnalyst Hakuna tatizo kubwa wakati sasa mnatangazwa washindi kwa kuua watanzania? Chini ya huyu mama muuaji, Magufuli kafa, Majaliwa na Mpango wamegomea siasa kwa utata, Maspika wawili wametoka kwa milio, na Sasa Nchimbi kagomea siasa kiutata. Tunakaribia mwisho wa safari.