Kibongobongo utafundishwa sana Business Management au Business Administration
Very rarely utasikia watu wakifundishwa Business Establishment au Business Development
Unawafundisha watu ku- manage biashara ambazo hawana. Mwisho wa siku unatengeneza matapeli tu.
BINADAMU TUMEKUJA KUWA WANYAMA, MTU UMEMFUKUZA KAZI NA BADO NYOT YAKE UNAICHUKUA.
Kama unashindwa kutusaidia basi usiwe kikwazo kwenye njia yetu maana walionyuma ni wengi na wanategemea mapambano yetu ili WALE.
SOMA🧵
1). Wamezima Telegram
2). Wamezima X
Soon Wanafika—Instagram, Facebook & WhatsApp—Just a Matter of time
Maana yake Wale Wote waliojiajiri Online—Wanageuka Ma-JOBLESS
And…NOBODY Cares!
Tuna VIONGOZI wa Ajabu na Very Selfish!
KIBATALA NDIE WAKILI WA ASKOFU GWAJIMA KWENYE HILI LINALOENDELEA.
Picha linaanza KANISA WALILODAI LIMEFUNGIWA WAO HAWALITAMBUI.
Soma alichoandika WAKILI MSOMI.👇🏾
Peter Kibatala: Nimepewa rasmi maagizo na KANISA LA UTUKUFU WA KRISTO TANZANIA, linalojulikana kikanisa kama KANISA LA UFUFUO NA UZIMA, chini ya uongozi wa Askofu Josephat Gwajima, kulitumikia kama Wakili wake, na kuliwakilisha pamoja na watumishi wake wa madhabahuni na waumini wake katika masuala mbalimbali ya kisheria — jambo la awali likiwa ni suala linalodaiwa kuwa la kufutwa kwa usajili wa kanisa hilo (kama Jumuiya ya Kijamii ya Ndani), linalodaiwa kufanywa chini ya Sheria ya Jumuiya, Sura ya 337.
Nitahutubia vyombo vya habari katika muda utakaopangwa hivi karibuni kuhusu masuala yote ya kisheria yanayozunguka tukio hili la kusikitisha sana, na nitawasilisha hatua zote za kisheria zinazochukuliwa kupinga kile ambacho wateja wangu wanakiona kama unyanyasaji wa kisheria.
Baadhi ya wateja wangu, baada ya kukusanyika kwa utulivu, walikamatwa usiku wa tarehe 2 Juni 2025, na kwa sasa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar es Salaam. Nimemteua Wakili kutoka Ofisi yangu kuwawakilisha kikamilifu. Tutawatetea watu hawa wa imani kwa kiwango cha juu kabisa.
Tunaendelea, na tumeanza kuchukua hatua zote zinazowezekana kisheria.
Tunafahamu kuhusu kauli mbalimbali za hadharani zilizotolewa na mmoja au wawili wa maafisa wa serikali kuhusu ustawi wa kisheria na kidini wa wateja wangu; kama nilivyotangulia kusema, tutajibu kwa kina.
Hatutambui chochote kinachoitwa “GLORY OF CHRIST CHURCH”; wateja wangu wanajulikana kisheria kama THE GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH. Hivyo basi, karatasi yoyote inayosambazwa kwa jina hilo la awali ni suala linalomuhusu aliyedai kuiandika.
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Wako wapi watu wema? Yako wapi makanisa na misikiti. Wako wapi viongozi wastaafu…
Inakuwaje kukemea utekaji na mauaji kwenye Nchi hii ni kosa?
Kila mtu asimame ahesabiwe.
Waovu wanataka kuzidi watu wema nguvu, mimi katika hili nasimama na Askofu Gwajima.
Taarifa muhimu kwa @SuluhuSamia
Rome Statute inayotumika kushtaki @IntlCrimCourt iko wazi kuwa kuumiza kikundi cha dini ni kosa la jinai na unaweza kushtakiwa
Unachofanya kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima ni targeting la kikundi cha kidini
Hivi kuna busara yoyote imebaki ndani ya @ccm_tanzania - mmekubali Dola iendeshwe na kikundi kidogo cha hovyo?
#TutaelewanaTu
Mnaikumbuka ile kesi ya yule Binti ya Yombo ambaye alibakwa na wale maafande?
September 30, 2024 walifungwa jela maisha na kuambiwa kulipa Fidia ya milion 1 kwa kila mmoja.
Wakili wa hao Maafande alikata rufaa na kesho kesi itaanzwa kusikilizwa Mahakama Kuu Dodoma apo.
Aisee
Rais wa zamani wa Zambia, EDGAR LUNGU alipenda sana KUTUKUZWA na KUABUDIWA kama MUNGU. Ameacha SOMO kwa VIONGOZI wa Afrika kwamba; MAMLAKA HUJA NA KUPITA. Mwisho wa UDIKTETA ni AIBU na FEDHEHA.
@Hope2Others2024@swahilitimes Kwahiyo kama kanisa limefungwa Je na Yale matawi yake zaidi ya 2000+ nayo hayataruhusiwa kutoa huduma ya kiroho kwa waamini wao??
Nina uhakika GWAJIMA alikuwa na TAARIFA ZA KUTEKWA kwake leo ndiomaana hakuenda nyumbani kwake.
Hadi sasa saa 5 yupo kanisani kwake inamaanisha alikuwa na taarifa zote. WATEKAJI baada ya kumsubiri kwenye kona zao na kuona hatokei wameamua kutimba KANISANI.
Nadhani mpango wa WATEKAJI saizi ulikuwa ni kumpoteza kabisa. Hili la ASKOFU GWAJIMA lichukue kama somo kuwa “Hakuna alie SALAMA”.
Askofu wa MAKANISA 2,000+ nchi nzima anatekwa wewe Nani?
Ukae kimya UTAPOTEA, UONGEE UTAPOTEA, WOTE TUTAPOTEZWA.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
ACP Mushana Lugola Mujema.
Huyu ni mkuu wa POLISI JAMII, Mkoa wa Kipolisi Ilala, askari wa Cheo chake hatukutegemea anaweza kumpiga rungu Katibu Mwenezi wa BAVICHA.
HUYU anatakiwa kuwa wa mfano,
Ashitakiwe kwa jina lake, Tukamate Mshahara wake.
TARATIBU ZA KUFUTA AU KUSITISHA UFANYAJI KAZI WA JUMUIYA AU TAASISI YA KIDINI.
Nivema kutambua kwamba Katika muktadha wa Tanzania, utaratibu wa kisheria na kikanuni wa kufuta dhehebu au jumuiya ya kidini unategemea masharti yaliyowekwa chini ya sheria na kanuni husika na siyo hisia au msukumo wa kisiasa wa mtu na hasa kwa kuzingatia
1. Sheria ya Jumuiya za Kijamii (The Societies Act), Sura ya 337 (Revised Edition)
Sheria hii ndiyo inayosimamia usajili, uendeshaji, na uvunjaji wa jumuiya zisizo za kiserikali, zikiwemo jumuiya za kidini.
Mamlaka ya Msajili:
Msajili wa Jumuiya za Kijamii (katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) ndiye mwenye mamlaka ya kusajili na kufuta jumuiya, ikiwa ni pamoja na madhehebu ya kidini.Kwa hiyo kwa sheria hii anaweza kuonya,kuelekeza,au kusitisha lakini kwa kuzongatia masharti ya sheria na Katiba ya nchi.
Utaratibu wa Kufuata Kabla ya Kufuta Dhehebu:Msajili atatoa ilani au barua kuitaka dhehebu au taasisi
(i) Kuwasilisha Sababu za Kufuta (Section 12–14 of the Societies Act):
Msajili anatakiwa kuonesha sababu za kisheria zinazomfanya atake kufuta usajili wa dhehebu, kama vile:
1. Dhehebu limejihusisha na shughuli zisizo halali au za kuhatarisha usalama wa taifa;
2. Limeshindwa kufuata masharti ya usajili;
3. Linahatarisha amani, maadili au umoja wa kitaifa;
4. Limeshindwa kuwasilisha taarifa za kila mwaka kama inavyotakiwa.
Kuwasilisha Ilani
(Notice) ya Kufuta:
Kabla ya kufuta dhehebu, Msajili anatakiwa kutoa ilani rasmi ya maandishi (Notice of Intention to Cancel) kwa uongozi wa dhehebu husika, kwa kawaida kwa muda wa siku 30, akiwaeleza sababu na kuwapa nafasi ya kujibu au kujitetea.
Haki ya Kusikilizwa (Right to be Heard – Audi Alteram Partem):
Kwa mujibu wa kanuni ya haki ya kimsingi ya kisheria, dhehebu linapaswa kupewa haki ya kusikilizwa.
Msajili hana mamlaka ya kufuta bila kutoa fursa ya kusikilizwa kwa wahusika (fair hearing).
Mapitio au Rufaa ya Maamuzi (Judicial Review/Appeal):
Iwapo dhehebu linaona limefutwa isivyo halali, linaweza kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana na wasiporidhika kufungua shauri la mapitio (judicial review) katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga hatua hiyo,
Ufafanuzi wa Kikanuni (kwa baadhi yadhehebu):
Kwa madhehebu yanayohitaji kibali kutoka kwa taasisi nyingine (k.m. Baraza la Maaskofu CCT au Mufti Mkuu), Msajili pia hufuata taratibu za kushauriana na vyombo hivyo kabla ya kuchukua hatua.
Taratibu zingine za ndani:
1. Ukaguzi wa mali na hesabu;
2. Mkutano wa wanachama kujadili hatma;
3. Kufungwa kwa ofisi rasmi.
MUHIMU:
Kwa mujibi wa sheria Msajili haruhusiwi kufuta dhehebu kiholela. Lazima afuate mchakato wa kisheria unaojumuisha ilani, sababu za msingi, haki ya kusikilizwa, na fursa ya kupinga maamuzi yake.
Kufuta bila mchakato huo ni kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 13(6)(a) kuhusu haki ya Kusikilizwa
Maisha ya muajiriwa wa kawaida kabisa hapa Tanzania kwa mwezi.
1. Kodi - 200k
2. Usafiri - 200k
3. Chakula - 200k
4. Umeme - 30k
5. Maji - 10k
6. Matumizi binafsi - 200k
7. Savings 100k
Yani uyu ni mtu anayepata 940k as Net per month anaweza jenga kweli? 😂