Kuanzia kesho tutafanya maandamano ya amani nchi nzima, kuweka msimamo wetu kwa Tume ya Uchaguzi kurudisha wagombea wetu wote wa vyama vya upinzani walioenguliwa kwa sababu hizi za hovyo, tena kuwarudisha bila masharti yoyote!
#SasaBasi#NguvuYaUmma#NiYeye2020#TunduLissu2020
Rais Magufuli aliwaambia wasimamizi wa Tume ya uchaguzi, ambao ni wateule wake, “Siwezi kuwalipa mishahara mikubwa na magari mazuri, halafu mkatangaze wapinzani kuwa washindi kwenye uchaguzi.” Haya ni matokeo ya maelekezo hayo!
#NiYeye2020#SasaBasi#TunduLissu2020#NguvuYaUmma
Kabla hata ya kipenga cha kampeni za uchaguzi, wagombea wetu wa Udiwani na Ubunge wameenguliwa kwa sababu za uwongo, za kihuni na zisizokuwa na haki. Namna pekee ya CCM kushinda uchaguzi ni mezani!
#SasaBasi#NguvuYaUmma#NiYeye2020#TunduLissu2020
Hawa ni wagombea udiwani kata za Tunduma na viongozi wa Chadema ngazi ya Mkoa wa Songwe. Walituhumiwa Kwanza kwa kosa la Kuwa sio raia na sasa wamepewa Shitaka la unyanganyi wa kutumia silaha. Haya maonevu sio Mara ya Kwanza kufanyika Tunduma.Lengo ni wasigombee Udiwani.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitupangia ratiba ya kuwasilisha fomu za uteuzi kati ya saa 6 na 6:15 mchana huu. Tumefika Tume tangu saa 5:45 asubuhi. Hadi sasa tunasubiri kuitwa ndani kuwasilisha fomu zetu kwa Tume. Wagombea wa CUF ambao walikuwa nyuma yetu kwenye ratiba, wao ruksa!
It's a crazy and violent night in #Tanzania. Opposition candidates in different corners of the country are being invaded and robbed their nomination forms by ruling party hooligans.