@MwijakuBurton Sasa, ktk spirit hiyo hiyo, linganisha na pia linganua ( compare and contrast) kati ya mtazamo na mwenendo wa Boni yai na ule wa kwako km vijana wa kitanzania. Kisha jipigie makofi au ujidharau na kujilaumu.
@Lugongam@ezekiel_kamwaga Na kwa mtazamo wake huu, hatakiwi na kwa kweli hastahili kuwa mwandishi wa habari. Ni bahati mbaya sana kwamba miongoni mwa waandishi tuna waandishi wa kariba hii ktk taifa letu. Ptuu!
@Pollo_Dr@HecheJohn Wewe mwenyewe mbona hushughuliki na yale ya kwako tu? Kwa mfano hili linakuhusu nini? Maana ni Heche na Gambo; unahusikaje? Una chembe chembe za ubinafsi.
@IAMartin_ Kama kweli umelelewa kiimani sawa sawa kiasi cha kujua lipi ni sahihi na lipi si sahihi na madhara ya kutenda uovu, kuna mambo ukiyafanya roho inakusuta mno na kukushtaki. Utajikakamua, lkn wapi, utasutwa hadi ndotoni. Yawezekana sana, huyu ana chembe hizo hapo juu. Ila sasa!
@oficialfab2017@fatma_karume Unalinajisi pakubwa jina la mpigania uhuru halisi na heshima wa wakati wake "Steven Biko". Haina tofauti na "kunguru" kujiita au kujifananisha na "tai".
@ExaudWilly@manaal_ms Taifa gani linaruhusu utamaduni huo? Kwamba watu wakitofautiana wanaweza tu kuwindana na kuumizana, kupotezana na hata kuuana huku vyombo vya dola vikiangalia tu?
@lwaitama1 Hili na la bodaboda yaendeeni kwa uangalifu na umakini mkubwa, hasa namna mnavyotamka na kuyajadili. Bila shaka mna nia njema; lkn haya ndiyo yamekuwa kimbilio na msaada mkubwa kwa vijana wengi.
@viannnre@RealBishopsam@NalukwagoJudith You shln't waste your precious energy responding to such nonsensical reasoning. Implying that death is afraid of presidential motorcade?
@BrycesonUrio@IamLyenda Tupate uchungu weeeee, hadi tufike mahali tuchukue hatua. Kutotuonyesha hakuondoi madhara tunayosababishiwa. Yako pale pale na yanaongezeka mwaka baada ya mwaka. Tuonyeshwe pasipo kificho, tupate akili.
@emboya45@IAMartin_ Hii taarifa ya CAG inahusu mwaka wa fedha 2023/24. Deni la taifa linalojadiliwa hapa ni la hadi Juni, 2024. Tafadhali zingatia hilo.
@kaji_sijo@fumbokhanJr@Lizzie36021 Acha kupotosha. Jesus lizard sio "Mjusi Yesu Kristo". Ktk jina "Jesus lizard", sioni neno "christ" mbele ya Jesus, kwa mujibu wa andiko lako. Wewe neno "kristo" umelipachika tu kwa utashi wako jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na hatari, wenye lengo ovu.
@chiefodemba Kuna mambo hutokea kwa sababu ya kanuni za asili. Km kuna waafrika wananeemeka tokana na udhaifu wa waafrika wenzao, kwa nini tuone ajabu wazungu kufanya hivyo kwetu? Hii inashuka hadi ngazi ya familia. Vipi mienendo ya watu wanaopata madaraka miongoni mwetu ikoje kuhusu mali?