Kuna kipindi kwenye maisha ambapo unatazama nyuma na moyo wako unajaa huzuni. Unaona miaka iliyopita, maamuzi uliyofanya, sehemu ulizochelewa kuondoka, watu uliowapa nguvu zako, na versions zako ambazo ziliishi bila kuelewa thamani ya muda.
A THREAD 🧵
Minazi mifupi esp Malaysian Green Dwarfs ni investment nzuri sana shambani. Inavumilia hata ardhi yenye chumvi kiasi. Inawahi kukomaa na inatoa nazi nyingi. Nzuri sn hata kwa madafu. Ilipoingizwa pwani ilipondwa kuwa watoto, na kina mama wanaiiba. Siku hizi ni "Dili" sana
@zittokabwe Swali la msingi bado lipo, kama kutoka Rufiji mpaka Arusha tunapata transmission loss mpk 20%, kutoka Ethiopia to Kenya then Tanzania, je wanapata transmission loss ya kiasi gani, au ni none of our business, je Wana accommodate vp na kupata profit
"Iko tofauti ya kusikiliza na kusikia. Si kila mwenye uwezo wa kusikia anaweza kusikiliza. Kusikiliza ni kipawa na pia stadi (skill) ambayo mtu hujifunza." ~Togolani Mavura.
Kuna siku moja tutakuwa tunagombania kulipa bili.
Surprised ya birthday haitakuwa kumwagiana maji, Bali tutapeana mitaji ya biashara au viwanja kwaajili ya ujenzi..
Hatutakuwa na shida zinazouzidi kina mfuko wetu..
Tuendelee kukaza wanangu..👊
UAMUZI WA MAHAKAMA KUU
Tunamshukuru Mungu Mahakama Kuu DSM IMERUHUSU raia wa Tanzania kufungua shauri la kupinga Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kusimamia uchaguzi wa wenyeviti wa Vitongoji, vijiji na Mitaa .
Ipo siku watu waliokukataa kwenye maisha yako watarudi kwako baada ya kukatishwa tamaa na wale waliowaamini kuwa ni bora kuliko wewe. Usiwaamini tena waache waende✍
Gm fam 🙌 ❤
Thank you for the support. Nakusihi sasa ufuatilie haki za kijana aliyepigwa risasi Bariadi ili haki ikaptikana. Tupo tayari kukupa guidance as an upcoming human rights defender
#BIASHARA: Mara nyingi tunanunua bidhaa mitandaoni na mara nyingine kwa kuagiza kutoka nje ya nchi ambapo kuna wakati baadhi ya Wanunuzi hukutana na utapeli
Ununuzi mtandaoni unaweza kuwa si salama kama hautakuwa makini kwasababu unaweza kutapeliwa au kuletewa bidhaa ambayo hukuagiza
Je, umewahi kukutana na jambo gani la kitapeli wakati wa ununuzi mtandaoni na hatua gani unachukua kuepuka kutapeliwa?
Soma zaidi https://t.co/zzyvTujf96
#Jamiiforums #DigitalSecurity #DigitalSafety #JFDigital
@jaliluzaid Pale ilipotokea kupishana kauli na Baba alipaswa kuwa mtulivu, na kurudi kwa Mara nyingine kuomba rukhsa ya yeye kufanya kile anachokitaka. Na km inashindikana kwake Kuna baba mkubwa au mashangazi angewashirikisha kupata suluhu ya jambo lake.
MAAJABU YA NCHI ZA ZAMBIA NA MALAWI; #UZI🧵
~1. Nchi zote Malawi na Zambia zilipata uhuru mwaka 1964, na zote hutumia pesa aina ya Kwacha. Marais wake wote wa kwanza, Dk. Kamuzu Banda (Malawi) na Dk. Kenneth Kaunda (Zambia) walizitumikia nchi zao katika nafasi za urais kwa muda_
Jana nilikua namuambia Chando Jr' kuwa...
1. •Haturudii makosa kizembe, Tulipogundua uongo ndio nyimbo zao pendwa, Tukawategea sikio bovu..
2. •Tulivyowaonesha upendo kisha wakagoma kuuona na kuuthamini, tulienda kuwapa wenye macho..
3. •Waliosema hatuezi ishi bila wao, walipokwama sisi ndio tulikuwa kimbilio..
4. •Waliotuombea kifo, tuliwazika wao na rambirambi tukachanga..
5. •Wale waliotuambia hatuwezi kufika mbali, walitukuta kituoni tukiwasubiri..
6. •Waliotusema kwa madhaifu yetu, tuliwaomba watufundishe jinsi ya kuwa malaika kama wao.
7. •Waliodhihaki ndoto zetu, ndio haohao walijisifu kutujua pale tulipotoboa..
8. •Tulipochelewa kulipa kodi baba mwenye nyumba alitutumia picha za watu wanaolala barabarani.
9. •Na sisi tulimjibu kwa kumtumia video za nyumba za kifahari zikiungua moto..
10. •Walipotutupa baharini kwenye maji ya kina kirefu, walitushangaa tuliporudi na samaki kama kitoweo..
11. •Ukiwauliza ni nini walishindwa kufanya kwenye maisha yetu? Watakujibu kutabiri ukweli wa anguko letu..
12. •Wao walitaka. Mungu akapanga.
Cc @AziziKasese mwamba kabisa💪
..Pia kama bado sija ku ADD kwenye group la "ELIMIKA WHATSAPP" basi nitumie meseji apa, tujumuike wote...👇
https://t.co/834VkDb55p
Basi nita ku ADD ni free tunashare mambo ya muhimu tu kujifunza🙏
Na kama unaitaji laptop basi tuone @ChandoMaterials 💪
Kuuguza mtoto kwa muda mrefu ni moja ya mitihani mizito haswa.
Ukipata nafasi ya kumtua mzazi yeyote huu mzigo kwa uwezo wa Mungu aliokujalia, usisite, kuna ibada ndani yake 🙏🏻
Kuna pesa kama inakufanya utweze utu wako na unajiheshimu utazikataa tu. Nilipoingia humu nilikuwa Influencer mimi nikapiga kazi nyingi za hashtags nikafika wakati hadi nami napata kazi nagawa pande kwa washikaji.
Lakini mwaka 2019 nikaamua rasmi kuachana na hizi harakati baada ya vitu viwili; Moja: waliokuwa wanatoa madili kujihisi kama wananipa maisha na bila hizo kazi zao siwezi kufanya mambo mengine.
Pili: Niliweka msimamo kuwa kuna kazi siwezi kufanya kama niliwahi kujichanganya huko nyuma imepita ila sirudii mfano; Matangazo ya Betting, Viatu+18 au Pombe.
Nakiri kupitia kipindi cha kubeba kila kazi iliyokuja mezani, kilikuwa kipindi cha mpito na kujifunza. Kila mtu anacho hicho kipindi ni kuvumiliana tu. Siku akili zikimkaa vyema mtu naye anakuwa na misimamo yake.
Hapelekeshwi kufanya kazi yoyote hata kama inamshushia heshima. Riziki uloipata na usiache watu na masononeko ina raha yake katika kula na unakuwa na utulivu wa nafsi.