Mguu wangu unaoza, nakufa huku najiona, naomba msaada maana nimekata tamaa. Naitwa Pascal James Mayalla, mkazi wa Kahama Shinyanga. Mwaka 2023 nilipata ajali ya pikipiki nikiwa Zanzibar nikielekea kazini. Kwa bahati mbaya nikavunjika mguu mara 2. Nikatibiwa Zanzibar na kuwekewa vyuma. Nilipopata nafuu niliomba kurudi nyumbani Kahama maana Zanzibar sikuwa na ndugu.
Hali yangu ikatengemaa kidogo na mwaka 2024 nikarudi Zanzibar kuendelea na kazi. Lakini kwa bahati mbaya mwaka jana, chuma nilichowekewa kilichomoka screw hivyo kikatoka sehemu husika na kuchoma nyama kwa ndani na kutengeneza kidonda kipya.
Nilipata maumivu makali sana. Nikaenda hospitali kikatolewa na kuwekwa kingine. Lakini Oktoba 2025 nilipata mtikisiko uliosababisha chuma nilichowekewa mguuni kukatika na kusababisha mfupa kuachana na mguu kupinda. Niliomba nirudishwe nyumbani Kahama. Hata hivyo sikuweza kwenda hospitali kutokana na kukosa pesa za matibabu.
Hali yangu inazidi kuwa mbaya kwani sehemu ya chuma kilichokatika imesababisha infection kwenye mfupa na kuendeleza kidonda kisichopona (Chronic Osteomyelitis).
Nimeelezwa kuwa hali hii inaweza kunisababishia kansa inayotokana na kidonda cha muda mrefu kisichopona (Squamous Cell Carcinoma).
Matibabu ninayohitaji kwa sasa ni operation ya kunyoosha mguu, kusafisha kidonda na kuweka chuma kingine. Gharama ni TZS 2.8M tu lakini nimelala kitandani mwaka mzima kwa kushindwa kumudu gharama hiyo. Naomba msaada niweze kupata matibabu mapema ili niepuke risk ya kupata saratani.
_____
Kama unaguswa kuokoa maisha ya ndugu Pascal Mayalla tuma sadaka yako kwenda M-PESA #0752581983, YAS #0719744954, CRDB #0150633516500, NMB #24110012109 Gifted Hearts Foundation | RudishaTabasamu | LetLoveLead
Kama ni mpaka usubirie Ibada ya pamoja au uende Kanisani ndo usali. Ni dalili za kufa kiroho mdogo mdogo. Agano jipya ibada ni popote. Ukuaji wa kiroho unaonekana kwenye maisha binafsi ya mtu.
Kama umekuwa hupati matokeo kwa muda mrefu kwenye maisha acha kusoma self help books, unapoteza muda.
Anza kusoma maandishi ya kale ya falsafa, saikilojia, quantum physics,na elimu ya kimungu.
Mafanikio kwenye chochote kile ni PRINCIPLES, mbinu hubadilika.
Soma Biblia hakuna mtumishi ataaamua uende mbinguni au usiende. Hili kipo mikononi mwako na Mungu. Ni siri yako na Mungu. Mjue Mungu kibinafsi. Mchungaji hatakuwepo wakati ule, Nabii, Padre wala Mwinjilisti hatakuwepo utaulizwa kwanini ulipewa akili. Kwanini ulipewa Roho Mtakatifu na kwanini ulipewa Biblia. Na fursa pekee ya Agano jipya kwamba kila mtu anaweza kusogea kwa Mungu. Anaweza kuhusiana naye na kuongea naye kibinafsi bila kupitia kuhani/mtumishi yeyote.
Kuna watu kwenye Biblia waliitwa kwenye finances/Mungu aliwabarikia utajiri kwa ajili ya utumishi kwa Mungu. Unakumbuka yule tajiri aliyeandaa kaburi na mazishi ya Yesu, Yusufu Armathaya. Biblia imeandika alikuwa akisubiria WOKOVU. So alipata ufunuo wa wokovu, akatembea na Mungu kwenye finances kuandaa mazingira ya wokovu kutokea Duniani. Alikuwa na assignment ya katika Ufalme wa Mungu kwa kutumia fedha na mali zake.
Mathayo 27:57-60
57 Hata ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;
58 mtu huyu alimwendea Pilato akauomba mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe.
59 Yusufu akautwaa mwili, akauzonga-zonga katika sanda ya kitani safi,
60 akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Kama unapitia hizi changamoto:
Kusumbuliwa na tamaa za ngono
Kurudi nyuma kila mara baada ya kupiga hatua fulani ya kimaisha
Migororo isiyoisha ndani ya ndoa
Kushindwa kupata watoto kwa baadhi ya watu
Kupata kipato kwa njia ngumu
Matumizi mabaya ya fedha
SOLUTION 👇
Habari za leo? Naomba utusaidie kutoa taarifa huenda ndugu zake watapatikana. Huyu kijana ameanguka ghafla maeneo ya Kimara mwisho. Alikuwa amebeba deli la maandazi anauza. Tumemkimbiza kituo cha afya Kimara kujaribu kuokoa maisha yake, lakini haikuwezekana. Madaktari wamesema tayari alishapoteza maisha kabla ya kufikishwa kituoni. Tumejaribu kuangalia kama ana kitambulisho chochote lakini hana. Tunaomba usaidie kupost ili ndugu zake wapatikane au kwa yeyote anayemfahamu afike kituo cha afya Kimara.!
Ukitembea vizuri na Mungu nakwambia mambo mengine kwenye maisha hufunguka yenyewe, utukufu wa Mungu ukifunika maisha yako, hakuna wa kuzuia baraka zako. As Jesus said
Mathayo 6:33
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Hata Yusufu alijaribiwa katika ahadi ya kusudi lake, lakini hakukata tamaa, ilikuwa hivyo kwa mfalme Daudi pia aliyepakwa mafuta akiwa na umri wa miaka 16, lkn alingoja majira ya BWANA. Jiandae pia.
Zaburi 105:19
[19]Hata wakati wa kuwadia neno lake,
Ahadi ya BWANA ilimjaribu.
Hutaki kuwajibikia makosa yako Hutaki kukiri mapungufu yako Hatutaki kuwa wawazi kwenye Makosa yako
Unajificha kwenye ombwe la laana na mikosi, Mwisho wa siku tutauziwa maji ya upako utakanyaga mafuta utauziwa stika utauziwa mandazi upako utauziwa leso
Utauziwa udongo au mchanga Kutoka Israeli ukiamini ni upako utatoa sadaka ya malango Kila mwezi utatoa sadaka ya kujilipua
Utatoa sadaka ya kujimaliza kama hii haitoshi utawamaliza mitume na manabii utamaliza makanisa yote ya mwendokasi
Hakuna kitu kinachobadilika kwa mtu anayekwepa uwajibikaji
HAWA NDUGU ZETU WANAHITAJI MSAADA WETU ILI WAWEZE KUPATA MATIBABU.
Hawa mnaowaona hapa ni Watanzania wenzetu ambao wamepata madhira mbalimbali.
Picha ya Kwanza anaitwa Kuringe Sawere huyu alitekwa na Maofisa wa Polisi Disemba 4, 2025 baada ya wiki mbili kupita kuna msamalia mwema alitujulisha kwamba Kuringe kafichwa kituo cha Polisi Chang’ombe Dar es salaam lakin alikuwa ameteswa sana kiasi kwamba alikuwa anatembelea tumbo maana alipigwa sana maeneo ya kwenye nyayo, magoti na mgongo.
Disemba 22 aliachiwa kwa dhamana ya Polisi lakin hali yake kiafya sio nzuri bado anapata maumivu makali ya miguu na mgogo hivyo anahitaji kufanya vipimo ili aweze kupata tiba.
Picha namba 2 ni Musa Ndile huyu alitekwa November 27, 2025 na maofisa wa Jeshi la Polisi, walimpiga sana na kumuumiza miguu yote miwili, Disemba 17 aliachiwa kwa dhamana lakin bado hawezi kutembea vizuri, anachechemea hivyo anahitaji matibabu zaidi ili aweze kuwa sawa.
Picha no. 3 ni Alex Mutembei yeye alipigwa risasi ya kwenye paja Oktoba 29 lakin mpaka Leo hawezi kunyoosha mguu wake lakin pia mguu huo umeanza kuwa mwembamba hivyo anahitaji matibabu zaidi.
Picha namba 4 anaitwa Martin Elia huyu alipigwa risasi Oktoba 29 hali ya mguu wake inazidi kuwa mbaya kwasababu anajiuguzia nyumbani, anahitaji msaada ili aweze kupelekwa Hospital kwa ajili ya matibabu ili aweze kupona.
Hivyo basi tunaomba mchango wako kiasi chochote ulichojaliwa na Mungu ili tuweze kuokoa maisha ya hawa ndugu zetu
Michango itumwe kwenye namba
Mpesa: 0744719187
Jina: Musa Ndile
Yakiwa yamebaki masaa MACHACHE kuelekea UCHAFUZI mkuu 2025 gazeti la “The Times” la UINGEREZA (UK 🇬🇧) limeweka hii habari inayoelezea upande wa pili wa SAMIA ambao dunia haijui.
Mpaka sasa media za bongo haziongelei kabisa ukandamizwaji wa HAKI unaofanywa na serikali hii ya Kidikteta wote wamenunuliwa na wanapost habari ambazo zinampamba SAMIA tuu.
Asante Kwa social media maana saizi kila social media imekuwa ni MEDIA huru. Habari hizi mbaya za ukandamizwaji wa haki zinazoendelea nchini zinarushwa na sisi wenyewe na zinafika DUNIANI.
Leo hii dunia inajua kuwa SAMIA kateka watu, kafunga watu majela, kazikamata media zote zinaandika habari zinazomsifia yeye tuu, yote haya ni kujihakikishia ushindi kuelekea UCHAGUZI mkuu 2025.
Unaweza kuenda kuisoma makala hii muda huu. Link: https://t.co/8E3ZHlDFp6
REPOST: 200
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Ukiwa msomaji wa Biblia hakikisha unaijua vizuri Mwanzo sura 1 hadi 11 ndiyo sura zenye Mwanzo wa Kila kitu hapa duniani ndipo utaelewa vitabu na nyaraka za Paulo.
Hizi sura 11 zimebeba karibu miaka 2400 ni sura chache lakini zina mambo yote hapa duniani.