Umechagua kupigania UKOMBOZI, si kujihusisha na UDALALI. Umechagua kusimama upande wa ukweli, haki na utu, hata pale ambapo kusimama huko kuna gharama kubwa.
Usikubali vitisho vikuyumbishe, wala upweke ukufanye utilie shaka msimamo wako. Safari ya ukombozi haijawahi kuwa rahisi, lakini dhamira ya kweli haizimwi na upepo wa upinzani.
Kumbuka: HAUPO PEKE YAKO. Wapo wanaoona, wanaoamini na wanaothamini ujasiri wako. Simama imara. Ukombozi si biashara, na dhamiri si ya kuuzwa! ✊🏽🔥
#FreeTunduLissu #HakiZaBinadamu #HumanRights #JusticeForAll #Democracy #UhuruNaHaki
TAL!
Baada ya kukutwa na hatia aliomba kuongea na mawakili wake, tukamzunguka kila mtu akawa anampa mitigation facts,
akasema kwani hamjui wana hukumu?, tukamjibu tunajua!,
akasema nikifanya mitigation itabadili hukumu yao?, tukajibu hapana!
Akasema let me speak my mind!
MWANASHERIA MKUU WA MOYO WA WATANZANIA, TUNDU LISSU ❤️🇹🇿
Tundu Lissu, wewe ni jasiri. Umesimama imara pale ambapo wengi wangeogopa kusimama. Umechagua kusema ukweli hata pale ambapo kusema ukweli kuna gharama kubwa.
Umevumilia vitisho, mateso, jaribio la kukuua na sasa unapitia kifungo na kesi nzito kwa sababu ya msimamo wako na mapambano yako ya kutetea haki, demokrasia na Katiba mpya.
Lakini fahamu jambo moja: Huwezi kufungwa sauti ya mtu ambaye ameamua kusimamia ukweli. Huwezi kuifuta ndoto ya taifa kwa kumfunga mtu mmoja.
Kesho, tunapokumbuka safari yako na kusimama pamoja nawe, tunataka ujue kwamba hauko peke yako. Kuna Watanzania ndani na nje ya nchi ambao hawajakata tamaa, ambao hawajasahau na ambao hawataacha kudai haki.
Tunakuombea nguvu, ujasiri na ushindi. Tunataka haki itendeke. Tunataka uhuru wako. Tunataka Tanzania ambayo hakuna mtu anayeadhibiwa kwa kusema ukweli.
TUNDU LISSU, SIMAMA IMARA. HISTORIA ITAKUKUMBUKA KWA UJASIRI WAKO.
FREE TUNDU LISSU!
HAKUNA HAKI BILA HAKI!
KATIBA MPYA NI LAZIMA! 🇹🇿💪🏾
Tanzanian opposition party chair Tundu Lissu has been detained 18+ months solely for peaceful exercise of his rights.
The European Parliament condemned his "arbitrary & politically motivated detention" & called for his immediate, unconditional release.
https://t.co/cmlpcQMztk
Imekuwa ni safari ndefu sana kwenye kuta nne za GEREZA.
Bado siku mbili dunia ijionee utawala wa WAKOLONI WEUSI ulivyokatili kuliko WAKOLONI WEUPE.
Tupo nyuma yako Mh Tundu Lissu na sisi wapenda HAKI DUNIANI kwote tunajivunia wewe.
#FreeTunduLissu
Repost 200
Hukumu kesi ya Lissu kipimo weledi wa Mahakama https://t.co/YxAjgqFQu3
Hukumu ya Kesi ya Lissu ni kipimo cha uhuru wa mahakama na uwezo wa mahakama zetu kutenda haki. Tunaisubiria kwa hamu.
Pumzika kwa amani, Wakili Alute Mughwai Lissu. Mchango wako na upendo wako kwa Jamii vitakumbukwa daima. Nenda Kiongozi.
Mwenyezi Mungu aipe faraja familia. 🕊🕯
‼️🚨CATHOLIC PRIEST ABDUCTED IN #Tanzania ‼️
#EnforcedDisappearances
Father Josephat Misigaro the Parish priest of Nguruka parish in Kigoma has been abducted! He criticized the government for #TanzaniaMassacre last Sunday in his sermons! His whereabouts are unknown
Cc @WGEID @OHCHR_EARO @achpr_cadhp@hrw@HRF@SenateForeign@AmnestyEARO
Huyu ni Padre Josephat Misigaro paroio wa Nguruka wilaya ya Uvinza Kigoma ametekwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ameponzwa na mahubiri yake jumapili iliyopita
Ndo nchi imefika hapa utekaji njenje!
Huku ni kuchanganyikiwa big time
#SamiaMustGo
#FreeAllPoliticalPrisonersInTanzania #StopAbductionsTz
Ulikuwa mtu mwema, mkweli na mtu wa kupenda Haki tena mwenye upendo mkubwa kwa familia yako
Naitakia pole familia @TunduALissu katika kipindi hiki kigumu na chenye mapito yenye maumivu makali
Apumzike salama!
Her name is Colletha Ntidyicha.
She was abducted on the 14th of October 2026 by Samia Suluhu's killer militia.
Colletha's whereabouts are still unknown more than a week since she was abducted.
Where is Colletha ? Speak for Colletha. #FreeColletha#EndAbductionsEA#PASNet
Wananchi tuna deni kubwa sana tunalodaiwa na Tundu Lissu!
Lakini hebu tujiulize kwa unyoofu kabisa: Tundu Lissu anajitoa kwa ajili ya nani? Anajitoa kwa ajili yake? Familia yake? Anatafuta fedha, uteuzi au cheo?
Kama angeamua kuwa mwanasiasa wa maigizo na kujali tumbo lake, angeendelea kusimama kwenye msimamo huu? Angeendelea kubeba gharama kubwa kiasi hiki, gharama inayoweza hata kukatisha uhai wake?
Juzi, Agosti 21, 2026, Mahakama Kuu imeamua kwamba Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini, hatua inayompeleka katika hatua ya utetezi.
Lakini sasa swali si Lissu pekee. Swali ni sisi tulioko nje ya gereza.
Je, kweli tunaguswa na yale anayopitia? Je, tunayaishi yale anayoyapigania? Je, tunathamini uhuru, haki, Katiba bora na utawala wa sheria kwa kiwango kinachostahili gharama anayolipa?
Inaumiza kuona mtu mmoja akibeba mzigo mzito wa mapambano, wakati sisi tuko busy na udaku, maigizo ya "machawa" na wasanii waliopotea njia kwenye muziki na filamu, porojo za mitandaoni na soka letu la mchangani lisilo na mbele wala nyuma!
Tuna muda wa kujadili kila kitu, lakini hatuna muda wa kujadili maisha yetu wenyewe! Hili si suala la kumpenda Lissu. Ni suala la kujiuliza kama tunathamini kile anachokipigania. Kwa sababu kama mtu anajitoa mhanga kupigania haki zetu, lakini sisi tunaishi kana kwamba hakuna kinachoendelea, basi kuna pengo kubwa kati ya gharama anayolipa yeye anayepigania haki na thamani tunayoweka sisi tunaotetewa.
Na kama Tundu Lissu, mwanasheria mbobevu anayejua vizuri nguvu na udhaifu wa sheria, anaweza kufikishwa kwenye hali hii, basi tujiulize: Itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida asiye na jina, fedha, uelewa wa sheria wala uwezo wa kupata msaada wa kisheria?!
Huenda siku moja tukaja kugundua kwamba tulikuwa na mtu aliyekuwa tayari kupoteza uhuru wake na hata maisha yake kwa ajili ya misingi aliyoiamini, lakini sisi tulipoteza muda wetu tukishangilia vitu ambavyo havibadili chochote katika maisha yetu.
Lissu anaweza kuwa gerezani, lakini swali kubwa zaidi ni: dhamira yetu iko wapi?!
Tusiishie tu kumshangilia mtu anayeteseka kwa ajili yetu. Tujiulize tunafanya nini ili maumivu anayoyapitia yasiwe yake peke yake.
Kuna kitu cha pekee alichonacho Lissu, nadhani Mungu alimjalia, na anakitendea haki. Kwa kweli, ninatumaini ataishi kuiona Tanganyika au Tanzania ambayo amepigania kwa dhati.